Siku niliyomuona Nyerere live nilisikitika sana

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze katika mada husika.
Nakumbuka siku 1 mimi na mjomba wangu tulikuwa tunatoka feri kula samaki, tukijielekeza mnazi mmoja kupanda basi turudi nyumbani. Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 1995, kabla ya uchaguzi mkuu.

Basi bwana wakati tunatoka feri kufika maeneo ya post mpya, tukaona magari yamesimama foleni kuashiria kuwa kuna kiongozi mkuu anatarajia kupita muda huo. Kwa vile kulikuwa na watu wengi wakishangaa shangaa ili waone ni kiongozi gani atakaepita, ikabidi na sisi tujiunge na ule msururu wa watu kuangalia kinachojiri. Wengi walihisi ni raisi Mwinyi alikuwa anatoka ikulu kuelekea sehemu tusioijua.

Lahaula, ghafla tukaona pikipiki moja zile zinazotumika kushindikiza viongozi ikichomoza, huku ikiwa imeambatana na benzi moja ambalo lilionekana ni la kawaida sana, kwani raia wengi tu walikuwa wanamiliki mabenzi tena ya maana kuliko lile, na nyuma ya benzi kulikuwa na land rover inayofanana muundo na hiyo picha niliyoambatanisha na uzi wangu hapo chini (watu wakawa wanapepea mikono) kuashiria kufurahishwa na yule aliekuwa anapita.

Sasa baada ya ule msafara wa pikipiki, benzi na land rover kupita, ndiyo magari mengine yakaruhusiwa yaendelee na shughuli zao. Ikabidi mimi nikamuuliza mjomba wangu, vipi mbona magari yanaruhusiwa na wakati kiongozi mwenyewe hajapita, mjomba akaniangalia kisha akaniuliza, kwanini wewe haukuuona ule msafara wa piki piki na magari mawili yakifuatana, nikamwambia niliona, akanijibu sasa ule msafara si ndo ulikuwa na kiongozi mwenyewe, nikamuuliza huyo kiongozi mwenyewe sasa alikuwa nani?

Mjomba akacheka kidogo kisha akanambia kwani wewe haumjui baba wa taifa mwl Nyerere, nikasema namjua vizuri sura yake kupitia tv, magazeti na vitabu mbali mbali, kisha mjomba akasema basi ndio yeye yule aliepita akiwa ndani ya benzi, alikaa siti ya nyuma, amevaa suti ya kijivu na juu alikuwa na kofia ya balaghashia. Dah kwa kweli alivyonambia vile sikuamini macho yangu. Nikamuuliza tena mjomba unauhakika kuwa yule ni baba wa taifa kweli, akasema bila shaka ni yeye kijana, kwani ulitegemea kumuona Nyerere bonge ya mtu au? Nikamwambia hapana simaanishi hivyo, ila kwa heshima aliyonayo katika nchi yetu, sikutarajia kumuona akiwa na msafara wa kichovu namna ile.

Mjomba akasema Nyerere ni mzalendo wa kweli, ndio maana maisha yake yote amekuwa akiishi ya kizalendo. Pia akanambia kwamba nchi yetu toka uhuru ilikuwa na wazalendo watatu tu, ila kati yao wawili washafariki amebaki yeye Nyerere. Nikamuuliza unasema toka uhuru nchi yetu ilikuwa na wazalendo watatu tu na Nyerere akiwa mmoja wapo, sasa hao wengine ni kina nani mbona mimi au sisi hatuwajui. Mjomba akasema wazalendo waliokuwa na Nyerere na sasa wametangulia mbele ya haki ni aliekuwa raisi wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi marehemu mzee Abeid Amani Karume, na mwingine ni aliekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Hapo nikawa nimeelewa, basi tukafika mnazi mmoja tukakuta watu wamejazana karibu na stand wakiangalia mchezo wa karata tatu, na sisi tena maongezi yakahama na kujikuta tumeingia katika maongezi mengine nje na yale na Nyerere. Ila ki ukweli siku ile nilisikitika sana kumuona baba wa taifa kubwa kama Tanzania anazunguka mjini na msafara wa gari mbili tu na piki piki moja. Huyu ndio baba wa Taifa na mzalendo wa kweli kabisa toka moyoni hayati Julius Kambarage Nyerere. Kama kuna mungine ashawahi kukutana mwamba huyu katika mazingira ya kawaida kama yale niliyomuona nayo mimi, aje atusimulie kidogo ili tujifunze uzalendo wa kweli kupitia kwake.

Asanteni sana.

images (94).jpeg
a244a8a2c8d81d0ac2c13a629ccdd577.jpg

Hapa chini ni raisi wa wakati huo mzee wetu alhaji Ally Hassani Mwinyi, akiwa ameenda kumtembelea baba wa taifa hayati mwl Julius Kambarage Nyerere, pembeni ya Nyerere kushoto ni mama Maria Nyerere, na wazee wawili ambao walikuwa majirani wa Nyerere majina yao siyafahamu. Hakuna watu waliowazunguka hao viongozi na mabunduki kama ilivyo sasa.
 
Ndivyo msafara wa Nyerere ulivyokuwa hata akiwa madarakani. Hakuwa na msafara mkubwa barabarani naona alijiamini mashushu aliowasambaza nchi nzima wanafanya kazi nzuri...
Hahaha kweli mkuu, naona mlinzi wake katinga na shati la kitenge 😀😀😀
 
Ndivyo msafara wa Nyerere ulivyokuwa hata akiwa madarakani. Hakuwa na msafara mkubwa barabarani naona alijiamini mashushu aliowasambaza nchi nzima wanafanya kazi nzuri.


Sema protokali za zaman kavu sana yani red-carpet inakua kwa aajili ya gari afu muhusika anadunda nyasini😂😂😂.....Afu nani kamuona msaidizi mwa Mwl ambaye pia ni ndugu wa aliyekua msaidizi wa Hayati JPM?
 
Back
Top Bottom