Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 17
************************
Nikiwa pale naishi kwa salome niliweza kuishi vizuri sana niliweza kuokoka na kuanza kumjua mungu mungu alinibadilisha sana nilifurahia maisha yangu mapya ya kidini siku zilienda zilienda nakumbuka usiku mmoja tupo na salome tumetoka kanisani tulikuwa tunakula chakula salome aliniambia kuwa mungu kanibadilisha nimekuwa kijana mzuri sasa,
Salome alikuwa akiniangalia macho ya kimahaba pale sebureni tukajikuta rasmi tumeanza mahusiano niliweza kulala na salome kwa mara ya kwanza toka niachane nae enzi hizo za shule usiku huo tuliweza kuenjoy sana mahaba yetu salome ni mwanamke mtamu mno na anaejua nn mwanaume anataka aiseee usiku huo ulikuwa usiku mtamu kwangu licha ya kuwa na mahusiano na jini fetty ila hakuwahi kunipa mapenzi kama haya ya salome,
Mahusiano yetu na salome yalipamba moto huku pia nikiendelea kuzidi kumtumikia mungu sasa kanisani nikawa maarufu kutokana na upigaji wangu wa kinanda pale kanisani kwa wakati wote sikuwahi kukutana tena na jini fetty hadi nikahisi huenda atakuwa ameniacha huru,
Ulipita kama miezi sita nipo na salome mke wangu maisha mengine yanaendelea huku mimi pia nikiendelee na shughuli za ufundi wangu kama kawaida maana sasa nilikuwa nishapona nilikuwa naweza fanya kazi,
Nakumbuka siku moja nilikuwa natoka zangu kivule narudi mombasa nilikuwa nipo kwenye piki piki yangu ndugu msomaji mungu alinibariki nikaweza kununua na mimi ka usafiri kangu piki piki,
Tuendelee na stori sasa nipo njiani natoka kivule na rudi kwangu mombasa ghafla nikamuona mdada mmoja ananipungia mkono kuomba lifti na mda huo ulikuwa kama saa moja kasoro ka jiza bado hakajaanza kuingia nilisimama akaniambia kaka samahani naomba lifti nikamuuliza unaelekea wapi ni mdada mzuri mweupe flani hivi akaniambia anaenda mombasa,
Nikajikuta na mwambia woow na mimi naenda mombasa basi wacha twende basi hao safari ikaiva kuelekea mombasa sasa katika kupiga piga stori yule binti alinishangaza sana alikuwa ananijua mimi kuliko mimi ninavyomjua yeye alianza kwa kuniambia naona siku hizi umeokoka? swali ambalo lilinipa shaka nikajiuluza kajuaje nikamjibu umejuaje? Akasema unaonekana tu ni mtu wa mungu nikacheka tu huku nikizuga kwa cheko la kinafiki ila nilishtuka na swali lake,
Sqsa tulipofika mombasa pale akaniambia nimshushe yeye anaelekea mtaa x lakini wakati tunaagana akaniambia kitu kingine kilichonipa mashaka zaidi aliniambia msalimie mkeo salame hii kitu kilinifanya nimuite lakini akaendelea kuondoka nikataka ninfuate nimuulize ww ni nani na unaoekana unanijua mimi vizuri ila nikasita ikabidi na mimi nirudi tu nyumbani usiku wa siku hiyo ulikuwa wa mawazo kwangu ikabidi nimwambie mke wangu salome kile kilichonikuta leo mke wangu akanipa hope akasema usimuwazie sana pengine labda anakufahamu si unajua ww siku hizi unavyofahamika pale kanisani huenda nae ni mshirika mwenzetu pale kanisani nikasema sawa sasa wakati tunapiga stori na mke wangu salome,
Ghafla simu yangu ujumbe wa sms ukaingia ujumbe ambao ulinishtua sana ulikuwa ukisema ongera kwa kunipa lifti leo by mkeo wako wa muda wote fetty sms hii ndio iliyonitoa gizani nikahatamaki sana niliweza kumuelezea mke wangu na kumuonyesha hiyo sms nae akashangaa akasema mume wangu kama jini fetty kaqanza tena kukukufuatilia bqsi hii vita ni kubwa mno inatupaswa tuzidishe maombi kwa mungu wetu suala ambalo nililiona ni la msingi ila asubuhi niliweza kwenda kwa mchungaji wetu pale kanisani sasa nyumbani kwake kumuelezea mambo yamezidi kubwa mabaya mchungaji akanitia hope kuwa leo tutapiga swala nzito na mambo yatakaa sawa kweli usiku wa siku hiyo mchungaji alikuja pale kwetu tukafanya maombi mazito tulifanya maombi kama masaa matano mchungaji akaondoka ila alinishauri kesho tufunge mimi na mke wangu huenda mungu ataepusha ili balaa la jini fetty kunirudia,
Wakuu itaendelea
Inaonekana salome alikuwa ni mtumishi mwenye imani kubwa kali,swali langu je iliwezekanaje akaruhusu mzini kabla ya ndoa maana ninavyojua kwa mtu wa kaliba yake isingewezekana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom