Siku niliyokabidhiwa picha halisi ya mapenzi yetu

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Dunia ya Mapenzi haijawahi kuwa rafiki namoyo wangu.. Ndio maana kila siku nimekuwa mtu wa kuuguza majeraha ya kutendwa.. Kuna wakati nikikaa huwa nawaza hivi huwa nakosea wapi?!!!!!! Laiti kama Mapenzi yangekuwa boda boda.. Kabla ya kupanda ningevaa element ya moyo..

Mwanzo wa hadithi zangu zote za mapenzi huwa ni wakuvutia mno.. Lakini hitimisho lake huwa nimoyo wangu kubaki kwenye dunia ya mateso na maumivu.. Sijawahi kuwa na hadithi yoyote ya Mapenzi, ambayo mwisho wake ilikuwa mimi kubaki kwenye mbingu za furaha..

Ubongo wangu umehifadhi hadithi lukuki za Mapenzi.. Leo nimeamua kuichomoa moja kati ya nyingi nilizonazo .. Ili kuieleza dunia jinsi December 24 ilivyonipora furaha...

December 24 imebeba kumbukumbu na huzuni hisiyosimulika ktk maisha yangu ... December 24 huwa naidanganya dunia kuwa nina furaha ndani ya nafsi kwa kutengeneza Tabasamu bandia kwenye paji la uso wangu... Lakini ndani ya moyo huwa ni hadithi tofauti kabisa.. Ndani ya moyo makaburi ya majonzi ujifunua .. Nakuufufua upya msiba wa maumivu niliowahi kuupata ktk maisha yangu ya Mapenzi ..

Tarehe 24 December miaka kadhaa iliyopita,.. Ndio siku niliyokabidhiwa picha halisi ya,mapenzi yetu .. Na binti ambaye niliyekuwa nampenda sana...Kipindi hicho... Nilikuwa kwenye dunia ya ujana ..Damu ilikuwa inanichemka isivyo mfano.. Na nlishindwa kabisa kuyahimili mawimbi ya Mapenzi kwenye ile bahari ya ujana..

Nilipoanza safari ya Mapenzi nahuyu binti, nilidhani mwisho wa ile safari yetu ingekuwa mimi nayeye kuishia kwenye milango ya kanisa tukiwa ndani ya suti na shela...Kwa tulivyokuwa Tunapenda na.. Sikuwahi kufikili mwisho ya Mapenzi yetu ingekuja kuwa msiba wenye maiti hisiyo onekana..Kwa kila mmoja wetu kati ya mimi na yeye

Ila nashukuru kwa kuwa alinipa heshima .. Na utamu wa simulizi ya Mapenzi kati yamimi nayeye... ULIANZIA DECEMBER 24.
 
Endeleza tu mapenzi ya kifilipino kwenye ardhi ya bongo utaendelea kuumia tu jan up december. Penda kiasi ishi nao kwa akili......
 
Endeleza tu mapenzi ya kifilipino kwenye ardhi ya bongo utaendelea kuumia tu jan up december. Penda kiasi ishi nao kwa akili......
Hahah anataka kuleta mapigo za kina Anjelo na Iyna Makaspak kwenye ardhi ya wadangaji
 
Back
Top Bottom