Siku nilipotoa rushwa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Najua baadhi ya watu hawajawahi kutoa rushwa wala kupokea rushwa, sitashangaa kuna watu ambao hawajawahi kuona mtu akipokea au kutoa rushwa na hivyo kwao rushwa ni kitu wanachokiangalia kutoka mbali na kwa kutumia mantiki tu.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa rushwa ni adui ya haki na hivyo tuipige vita; lakini nikiwa nimetulia na kujaribu kujiuliza kama nimewahi kutoa rushwa na nilijisikiaje nilijikuta narudishwa nyuma miaka kadhaa hadi siku ile nilipojikuta natoa rushwa na yote yalipomalizika sikuhisi au kuona kuwa rushwa niliyotoa ilikuwa ni "Adui" ya haki yangu na kimsingi nilioona ni rafiki, msaada, na njia rahisi ya kupata haki yangu.

Kuna kiwanja ambacho nilikuwa nakipania kwa muda mrefu sana lakini watu wa Halmashauri hawakutaka kuniuzia. Eneo lenyewe wakati huo lilikuwa halijajengwa sana na bado jipya na viwanja ndiyo vimepimwa tu. Tayari hapo mtaani kulikuwa na viwanja vya majaji wawili, kamanda mmoja wa JWTZ na Daktari wa Mkoa fulani... sasa nilipotoka kiwanja ambacho kilikuwa karibu na huyo jaji ndiyo ilikuwa kasheshe na jamaa walijua kuwa eneo hilo lilikuwa "hot" hasa huko mbeleni (liko karibu za ufuko wa bahari)... Sasa viwanja vilikuwa vinauzwa kwa wakubwa hawa kwa kati ya milioni 3 hivi na kuendelea lakini hakuna kilichozidi milioni tano (at that time).

Lakini kwa sababu wanazozijua hao jamaa wakawa wananizungusha kweli kukipata wakati waliniquotia Shs milioni 3.5. Ikawa ni kuzungushana kila kukicha na kunipoteza muda wangu mwingi. Nikawa najitahidi kuwa mwadilifu na nikisema kuwa sitatoa rushwa... bahati mbaya muda wangu wa kurudi kijijini ukawa umefika na pressure ilikuwa kubwa nikamilishe hilo kabla ya kuondoka. Ndipo nilipojikuta nikichukua uamuzi wa "kupenyeza rupia pale penye udhia" na matokeo yake kesho yake nikapigiwa simu kuwa kibali na makaratasi mengine viko tayari. (nilipenyeza shs 500,000 ingawa mwanzoni walitaka kama 200,000).

Tangu wakati huo hadi leo, nimekuwa nikijiuliza kama rushwa kwa watu wengi inaonekana kweli ni adui wa haki au inaharakisha haki kupatikana. Nimetumia neno kuonekana kwa sababu kama adui haonekani kama ni adui basi yawezekana kuwa ni rafiki.

Swali langu, je wewe umewahi kujikuta unalazimika kupenyeza rupia ili upate unachostahili au ulifanya nini kukwepa kufanya hivyo na ukapata unachotaka katika muda na namna unavyotakiwa? Je, wale wanaopokea rushwa na wanaotoa rushwa ni nani hasa anachochea vitendo vya rushwa? Je, mfanyakazi wa Tanzania anaweza kweli kuishi kwa kipato chake bila "njia" hizi za pembeni na kufanya kazi kwa uadilifu? Je tufweza twa asante baada ya kufanikiwa au kupewa unachotaka kunachochea rushwa?

Je, ni mazingira gani yanaweza kukufanya kweli ukubali kutoa rushwa kidogo hata kama wewe mwenyewe hukubaliani nayo?
 
Duh nishawai hadi kupewa biznezz card na ndata nikambiwa siku nyingine nikiwa na matatizo yoyote madogo madogo ni mbeep tu...lol!!!

Rushwa ni adui kwa maendeleo ya taifa kwahiyo ni adui kwa mtoa rushwa pia ingawa kwa wakati ule anakua hajui...kwahiyo ni rafiki kwenye short term.. sasa kama hapo umenunua kiwanja kizuri lakini inawezekana huduma muhimu kama barabara, maji nk. zichelewe kukufikia kwasababu ya ujumla wa madhara yakutoa rushwa pale inapofanya fedha za huduma hizo kupotea kwenye mifuko wa wala rushwa...kusema ukweli rushwa inaletwa na hali ngumu ya maisha na umasikini lakini inaendelezwa na tamaa na mazoea... mazoea yakutoa na kupokea, inakua ni hali kawaida ya maisha na wala sio kitu cha kushangaa tena... kusema ukweli ni shida sana kuishi TZ bila kutoa kidogo, iwe ni Traffic barabarabi au bouncer mlangoni...

Rushwa haiwezi kuondoka lakini inaweza kupunguzwa (hadi vatican city rushwa kibao).. Cha kwanza inabidi kufundisha kwavitendo... ofisa hawezi kukubali "kupunguza" kula rushwa kama bosi anakula vichwa kama hana akili nzuri therefore it does start at the top and not otherwise (viongozi), cha pili ni kwamba hauwezi kumshauri mtu mwenye watoto sita na mke nyumbani kutochukua rushwa kama mfukoni ana- buku mbili hadi mwisho wa mwezi... kwahiyo lazima viwango vya mishahara viwe reviewed kikamilifu (sio tu mining contracts)..Na mwisho ni kujaribu kuelewesha wananchi kwa njia zingine kwamba wanajinyima haki zao na huduma za maendeleo pole pole kwa kutoa rushwa...

Kumalizia utoaji au upokeaji wa rushwa ni mtu...lakini saa nyingine pale home tatizo lakutatua kwa shilingi mia tano lina weza kuku-cost siku nzima kwa hiyo inaeleweka temptation yakufanya hivyo...
 
CEJ, unachosema ni kweli ndio maana wakati mwingine tunapolalamikia rushwa tunaangalia from an intellectual stand point.. lakini kwa mtu ambaye ametoka kijijini au nje ya mji na amekuja mjini kwa siku moja kukamilisha mambo yake na wajanja wakajua huyu ni wa kuja si ndio watamkamua?

Hivyo utakuta mtu anapanga bajeti yake ya kufuatilia jambo fulani na ndani yake kwenye Miscelleneous anaweka na "chai" kidogo. Lakini najiuliza hivi wazungu wakienda kuomba huduma hizi hizi huwa wanakamuliwa pia..?
 
CEJ, unachosema ni kweli ndio maana wakati mwingine tunapolalamikia rushwa tunaangalia from an intellectual stand point.. lakini kwa mtu ambaye ametoka kijijini au nje ya mji na amekuja mjini kwa siku moja kukamilisha mambo yake na wajanja wakajua huyu ni wa kuja si ndio watamkamua?

Hivyo utakuta mtu anapanga bajeti yake ya kufuatilia jambo fulani na ndani yake kwenye Miscelleneous anaweka na "chai" kidogo. Lakini najiuliza hivi wazungu wakienda kuomba huduma hizi hizi huwa wanakamuliwa pia..?


It is one thing to acknowledge the depth of the problem, quite another to endorse the habit.

Here Mwanakijiji is on the record endorsing rushwa and passing it off as a "reality" of life.
 
It is one thing to acknowledge the depth of the problem, quite another to endorse the habit.

Here Mwanakijiji is on the record endorsing rushwa and passing it off as a "reality" of life.

Jamaa huwa anaandika mada zenye utata, kama sio zenye kutatiza!

Inabidi uwe makini kweli kweli kushtukia alichokifanya pale, yani inabidi "ndoo" yako iwe imetulia kisawa sawa wakati unamsoma. Swali analouliza limeficha dokezo, kama sio hitimisho, kwamba rushwa inaweza kuwa ni poa!

Ni kama Larry Summer alivyofukuzwa Ukuu wa Chuo, Harvard, kwa kuuliza kama Wanawake wameumbwa na uwezo wa kumudu Hesabu na Sayansi. Kuuliza, wakamwambia, ni sawa na kusema unakubali uwezekano huo!

Hapa, Jamaa anauliza kama haya mahusiano kati ya watoa haki na wapokea haki, haya mahusiono ya kupeana bakshishi ili wapeane haki, kama yasingekuwepo, watu wangepata haki kutokana na ukweli wa maisha?

Anasema kama watu wanafanya kitu ambacho huwa tunaambiwa kinatakiwa kiwe "adui," basi hicho kitu inawezekana ni "rafiki." Ambacho ameficha kukisema - kwa sababu kina matundu ya mantiki - ni kwamba kimsingi anadhani kitu ambacho ni "rafiki," kwa hapa rushwa, basi ni chema.

Utata mkubwa, kama sio machukizo!
 
Mzee wa Summa Theologica anaelewa vizuri ideals ni nini na umuhimu wake katika society.

Nashangaa anavyochokoza maada kama haelewi.
 
Mzee wa Summa Theologica anaelewa vizuri ideals ni nini na umuhimu wake katika society.

Nashangaa anavyochokoza maada kama haelewi.

Sio kwamba haelewi. Jamaa sio mtupu kihivyo hata kidogo. Ni kwamba haweki 'qualifiers' kwenye mada zake. Akisema kitu kinachoweza kuleta maana X, Y, Z, wakati anamaanisha X, huwa hasemi, jamani eeh, hapa simaanishi Y na Z. Hasemi, "hapa si condone rushwa." Anaiacha inaelea elea juu juu, kwa sababu Wananchi wakiona utata huwa wanaiacha kama ilivyo. Bongo watu wanatafuta kupeleka Bondo kinywani, hawana muda wa kufuatilia subtleties bwana!
 
Ningetaka kusema ambacho nadaiwa kusema nisingesita kukisema; sasa ukisoma kitu ambacho nimesema halafu ukasema kuwa nimemaanisha nisichosema basi yawezekana mtu hakusoma nilichosema kwani anafikiri nimesema nisichosema.

Sasa kama sikusema ambacho nadaiwa kusema itakuwa ni makosa makubwa kudai nimemaanisha nisichosema wakati uwezo wa kusema ninachomaanisha ninao. Kile nisichosema yawezekana ndicho hasa nimemaanisha. Hivyo ni jukumu la mtu kusoma na kugundua nimesema nini na katika hilo nimemaanisha nini. Pamoja na hayo ni vizuri watu kujaribu kutafuta hasa nimemaanisha nini katika kile nilichosema.

But in what I have said, I categorically deny that I have endorsed corruption.. not me sir.. kwani ningetaka kusema hivyo nisingesita.
 
Halafu ukisema usichosema kuwa ulisema unakuwa hukusema umesema kama ulivyosema.

Au usiposema umesema kuwa hukusema unakuwa umesema hukusema kama usivyotaka kusema?
 
Perhaps in being unnecesarily obscure, the received inferrence is justified.

There are a lot of things that one can't control.. how other people infer things is one of them.. Among the things that I can control is what I do and say...

So, I'm sorry to cause such an ambiguity..
 
Tukiridi kwenye mada
I hate rushwa, I hate it!!!! I hate it!!!!!! with all I have.
However................
Huwa inabidi saa ingine nitoe, wala si mara moja wala mbili
Mikono yangu imegoma lakini kutoa moja kwa moja au kujadili uso kwa uso, najionea aibu, najichukia wakati napojikuta kwenye mazingira hayo. Natamani kama vile nikimbie, huwa naprefer kutumia mtu wa tatu. Nahisi najipunguzia responsibility ya ukweli rushwa ni rushwa tu.
Mfano,
1. kiwanja, ilibidi hela zipelekwe na mtu, mimi nilipewa taarifa kuwa jamaa anataka laki mbili, basi nikampa huyo anaenisaidia akalipa nikaletewa makaratasi yangu nyumbani.
2. umeme, nilitoa hela kwa mtu ambaye alidai ni za kuharakisha, basi maadam nilipata risiti zoke halali, hiyo kwangu ilikuwa kama agency fee
3. kutoa mizigo bandarini, ndio usiseme, wanakuambia fulani anataka hiki au kileukikataa mizigo inalala huko,
4. police lost report nililetewa nyumbani mwenzio.
Hospitali sijawahi nashukuru mungu. Japo kuna mtu aliwahi kuniambia waziwazi anaomba nikamkatalia wazi wazi tena kwa ushari. (najua ni unafiki, kwani labda angetuma mtu anaenijua ningekubali)


Ila kupokea NEVER, NEVER!!
Rushwa ni kitu kibaya sana, ila tunakizoea na ndio mbaya zaidi.

Mwenzenu napata shida sana, kutoa natoa kukataa siwezi ila najisikia vibaya sana, nifanyeje?
 
Tukiridi kwenye mada
I hate rushwa, I hate it!!!! I hate it!!!!!! with all I have.
However................
Huwa inabidi saa ingine nitoe, wala si mara moja wala mbili
Mikono yangu imegoma lakini kutoa moja kwa moja au kujadili uso kwa uso, najionea aibu, najichukia wakati napojikuta kwenye mazingira hayo. Natamani kama vile nikimbie, huwa naprefer kutumia mtu wa tatu. Nahisi najipunguzia responsibility ya ukweli rushwa ni rushwa tu.
Mfano,
1. kiwanja, ilibidi hela zipelekwe na mtu, mimi nilipewa taarifa kuwa jamaa anataka laki mbili, basi nikampa huyo anaenisaidia akalipa nikaletewa makaratasi yangu nyumbani.
2. umeme, nilitoa hela kwa mtu ambaye alidai ni za kuharakisha, basi maadam nilipata risiti zoke halali, hiyo kwangu ilikuwa kama agency fee
3. kutoa mizigo bandarini, ndio usiseme, wanakuambia fulani anataka hiki au kileukikataa mizigo inalala huko,
4. police lost report nililetewa nyumbani mwenzio.
Hospitali sijawahi nashukuru mungu. Japo kuna mtu aliwahi kuniambia waziwazi anaomba nikamkatalia wazi wazi tena kwa ushari. (najua ni unafiki, kwani labda angetuma mtu anaenijua ningekubali)


Ila kupokea NEVER, NEVER!!
Rushwa ni kitu kibaya sana, ila tunakizoea na ndio mbaya zaidi.

Mwenzenu napata shida sana, kutoa natoa kukataa siwezi ila najisikia vibaya sana, nifanyeje?


Haika,

Kwanza asante sana kwa kuwa muwazi kama mimi nilivyojaribu. Na situmaini wewe kukiri kwako kutoa rushwa ina maana unaiendorse.

Pili, umeonesha kile ambacho nimekizungumza, kuna wakati mtu anatakiwa atoe rushwa ili kufanikisha kitu fulani ambacho pasipo hiyo hakitafanikiwa kwa haraka, ufanisi au muda unaotakiwa.

Lakini kubwa zaidi kwangu linahusiana na mapambano dhidi ya rushwa; kwa muda mrefu tumeimba wimbo wa "rushwa ni adui wa haki" lakini kama mtu anapata haki yake kwa kutoa rushwa, kwa mtu huyo inakuwaje rushwa adui? Na jambo ambalo nimeliona mara nyingi ni kuwa hata wale wanaopinga rushwa au vitendoo vya rushwa wanaweza kujikuta kwenye mazingira fulani wanakubali kutoa rushwa. Nitakupfa mfano:

a. Umemkimbiza nduguyo hospitali kwa dharura; unafika pale kweli anachukuliwa lakini kila kitu kinaenda pole pole kana kwamba hakuna dharura. Unajaribu kuulizia nesi/daktari unazungushwa zungushwa... moyoni unajua ukipenyeza rupia inakuwa kama umebonyeza "fast forward". Ndugu yako amekaa pembeni analalamika na wewe ni mpiga vita rushwa. Unajiuliza usiku wa saa saba, uite TAKUKURU au Polisi waje kuwakamata hao wafanyakazi au upenyeze rupia halafu ulalamike mbele ya safari?

Unavyoendelea kujiuliza uliza na uadilifu wako nduguyo anaanguka chini na kuanza kutoka povu kichwani; manesi wanajizungusha zungusha kuona kama utafanya lolote...

Mwisho unamuendea matron na "unampenyezea" elfu 25.. na mara mgonjwa wako anaanza kuwekewa drip, daktari anatokea, na ndani ya nusu saa mgonjwa wako hali yake inakuwa stable na matibabu yanaanza, na unanong'onezwa ukijitolea 25,000 nyingine basi atapatiwa hata chumba private...

Je utajilaumu kutoa rushwa hiyo? Je ungeweza kugoma kutoa rushwa na mtoto wako/ndugu yako anakufa kwa wewe kushindwa kutoa elfu 25,000 ambayo unayo mfukoni. Je utajisikia shujaa kwa kuacha afe na wewe umegoma kutoa rushwa?

Tukifikira utaona napendekeza kutoka mbali sana kuwa tunavyopigana na rushwa tunapigana vibaya; tumeshika makali na wala rushwa wameshika mpini..!
 
Hivi MKJ tuseme umetoa huduma safi kwa msukuma mmoja wa Mwanza na baadae akarudi ofisini na kukupatia burungutu safi tu ukakataa katakata kupokea lakini akakurushia juu ya meza yako na yeye akatokomea kusikojulikana, je hapo hujapokea rushwa au umepokea lakini bado unaichukia rushwa?
 
Hili swala la rushwa kwa TZ,liko kama limehalalishwa flani hivi!!!

Kwa sababu ukienda sehemu nyingi sana hapa bongo zinazotoa huduma kwa jamii sana sana hizi za bure rushwa iko wazi wazi, just infront of your face, pale unapoingia tu!!
Na usipotoa basi ndo siku yako nzima itaishia hapo au jalada lako litapigwa dana dana.

pia sisi wananchi tunaipromote kwa mfano unakuta mtu kavunja sheria labda ya barabarani, kuepuka zile "fine" anamuoffer polisi rushwa tena yeye mwananchi ndo anaanza kucall utamsikia 'sasa mzee nikupooze na ngapi uniachie'

hawa mapolisi nao vipato vyao ni vidogo sana hivyo bila rushwa maisha yao ni magumu,so to me i see this rushwa thing "imeshakua" yaani ina mizizi mirefu sana kiasi kwamba now kila mtu inabidi haitegemee in some ways either anataka or not ili mambo yake yaende smooth
 
Wajameni,

Hii inaonyesha kuwa sasa rushwa imerasimishwa rasmi kwenye mila na tamaduni zetu...imekuwa sasa ni sehemu ya sheria zetu zisizo rasmi....na kuzibadili itachukua muda........na sehemu hii ya sheria inarutubishwa ua uwepo wa vichochezi vingine, kama vile mfumo wa ugawanaji mapato katika jamii...tusiposahihisha namna tunavoigawa keki ya taifa....basi hizi 'sheria' zitaendelea kuwepo hata kama nafsi zitatusuta pale tunapobidi 'kuzitekeleza'.
 
We just need to break the cycle.
I know sometimes I need to shout to be served,
or to seem rude,
But most of the times I try
People think I am crazy to go against the system, and sometimes they tell me to swear if I never give it, offcourse I cant swear.
I is a battle of wills,
Some times I do not get what I want.

Wote tunajua jinsi dhambi inavyonoga, na kupumbaza, ni raha, mwili unapenda, tamaa inapenda, vitu tunavyotaka vinatokea.
Kufanya dhambi ni raha kwa kweli ya mwili, lakini faida yake ni ndogo sana ukilinganisha na hasara yake.
 
We just need to break the cycle.
I know sometimes I need to shout to be served,
or to seem rude,
But most of the times I try
People think I am crazy to go against the system, and sometimes they tell me to swear if I never give it, offcourse I cant swear.
I is a battle of wills,
Some times I do not get what I want.

Wote tunajua jinsi dhambi inavyonoga, na kupumbaza, ni raha, mwili unapenda, tamaa inapenda, vitu tunavyotaka vinatokea.
Kufanya dhambi ni raha kwa kweli ya mwili, lakini faida yake ni ndogo sana ukilinganisha na hasara yake.
C=P+D-T-A - I
Corruption = Power +Discretion - Transparency - Accountability -Intergrity
Ukishakuwa na hali hii......ujue rushwa will be there to stay.Tanzania imejaliwa kuwa na mazingira haya katika taasisi nyingi.Rushwa itaishaje? Ukihitaji huduma hata kama ni haki yako... discretion itakufanya uombeombe hadi utoe rushwa.Rushwa wanatolewa mpaka wale wenye kusimamia taasisi za kupambana na rushwa sembuse yakhe mie nisiye na madaraka yotote!
I agree that we need to do something.... je tutabadili vipi hii equation?
 
Back
Top Bottom