collezione
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 352
- 178
Sokoine akifufuka leo... Moja kwa moja anaenda kuchukua kadi ya uanachama CHADEMA
Dead men don't count.
well they don't need to be; they've already been counted!
M M Mwanakijiji, hujajua hiyo ni mawazo ya majambazi? Huwa wana usemi "dead people dont talk" ukiona mtu anachangia hivyo jua ana element za kijambazi!
Kivipi wameigaragaza Tanzania? Ina maana hata baada ya miaka yote hii ambayo hawa watu wawili wamekuwa nje ya uongozi hatujapata dawa ya kutibu matatizo tuliyonayo? Kwani Nyerere ndio aliuza na kugawa bure rasilimali za nchi na akaleta siasa uchwara za kujuana na kulindana hata kama ni wahalifu? Inatusaidia nini tunapojaribu kusukumia matatizo yetu sisi watanzania wa leo kwa wakoloni, na Nyerere wakati tunaofanya maamuzi na kuendesha nchi ni sisi tena bila ushawishi wao?
Mkubwa tupende tusipende nyinyi mnaojiiita "system at work" ndio mnatugaragaza watanzania. Mko kimaslahi zaidi kuliko kikazi. Mna njaa za kupitiliza! Mnataka kuvuna msipopanda! Mnalea hata yasiyolelewa popote pale ulimwenguni. Hayo ni matatizo ya Nyerere na Sokoine au ni ya kwetu?
Yes, Nyerere ndio alioitia Tanzania umaskini kwa kutokuweka misingi mizuri kwa miaka 24 aliyukuwa Rais. Kwa miaka 24 kila alichofanya kimekufa kabla ya yeye hajafa, kwa sababu alikuwa hajui akifanyacho.
Alidhulumu kwa kutaifisha mali za wanyonge wachche lakini magwiji walioijuwa dunia aliwashindwa, kesi nzuri ni ya LONRHO na Tiny Rowlands, alijaribu kumtaifisha huyu, akkakikwaa kisiki, ilibidi mwenyewe arudishe mali zake bila kupenda.
Tanganyika ilikuwa ni mchi ya kwanza katika Afrika kuuuza mazao nje, baada ya kuja Nyerere na siasa zake mbovu ikawa nchi maskini duniani na ikawa inaomba omba nje hata kula ikawa shida. Kaachia madaraka, mchi hii haina hata senti mbovu ya kigeni, viwanda vinakufa kwa kuliwa, ukabila idara zote za Serikali na Umma. Kila kitu hohehahe. Ardhi kubwa ya Tanzania kaigawia kanisa katoliki.
Unajuwa kuwa mmiliki mkubwa wa Ardhi Tanzania baada ya Serikali ni kanisa katoliki? Kwanini?
Jambo la ajabu sana ni kuwa mavuvuzela ya CCM ya sasa hayataki kabisa sifa za uadilifu za Nyerere na Sokoine ziwe zinatajwa.Lakini hao viongozi wao wakiwa kwenye public wanajidai kusema viongozi hao wazamani ni mfano wa kuiga.Unafiki mtupu.
Pls come up with supportive arguments kuonesha kwamba it was really nyerere who made us poor and not our ignorance uje na uthibitisho wa kisayansi na si porojo kama hizi unazopiga ambazo kila anayejisikia anaweza kuja nazo.Hakuna alichodhibiti Sokoine, Nyerere ndio aliokuwa kinara wa kila kitu, Sokoine was just a vuvuzela, mechi wanacheza wengine.
Hakuna anaestahiki sifa, si Nyerere si Sokoine, wao ndio walioigaragaza Tanzania. Ukipenda usipende, hivyo ndivyo ilivyo.
Unajuwa maana ya uadilifu au unajisemea tu? Anti Corruption ya Tanzania ilianzia awamu ya kwanza ikendeshwa na Maftah. Viwanda na mashamba alivyodhulumu Nyerere kwa mabepari vilianza kuliwa na kuuliwa wakati wa Nyerere. Viwanda alivyojengewa Nyerere na wachina, vilianza kuliwa na kuuliwa wakati huohuo wake. Mpaka anang'atuka, nchi iko hohehahe kwa uzembe na kutokuwajibika kwake na kwa viongozi aliowaweka madarakani, huo uadilifu unaousema wewe ni upi?
Kweli ni huzuni sana. NA kama ulivyosema kuwa akifufuka leo anaweza kuzimia tena ndani ya siku saba kutokana na hali ilivyo na aliyoiacha 1984.
Nakumbuka siku ile nilikuwa Shuleni pia, na majira ya saa SABA KASORO; tulikusanyika wote na Mwalimu Mkuu kwa huzuni alitangaza taarifa ya Kifo cha PM mpendwa Sokoine.
Nakumbuka wakati ule magazeti yalikuwa ni ya Chama na Serikali tu (Uhuru, Mzalendo, Daily News, Sunday News) KWa jinsi wananchi walivyoguswa na ule msiba nakumbuka kulikuwa na Foleni kubwa sana kila asubuhi katika vituo vya kuuza magazeti, na wengi walikuwa wanakosa.
Nakumbuka siku ya kusafirisha kwenda Arusha - Tulikuwa tunaishi Mbezi juu DSM, hivyo RTD walipotangaza kuwa ndege ndio inapaa uwanjani, na sisi ambao hatukuwa uwanjani tuliishuhudia ndege ya JESHI ikipaa hivyo tuliipepea mikono kwa huzuni kubwa ile ndege ikipaa na kuondoka.
NI HUZUNI SANA!!!!!!!!!!
Nashindwa kuendelea kwa uchungu!!!!
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!