Siku Nilipomsikia Nyerere Akilitangazia Taifa Kifo Cha Edward Moringe Sokoine

Nilikua tumbon mwa mama yangu,hiyo miezi,nilizaliwa mwez waTisa 84,
ILA LEO UKINIULIZA KUHUSU SOKOINE
1.Huyu alifunika watanzania kwa kupendwa na zani ata baba wa taifa hamfikii,akua mbinafsi,nyerere anamzid jambo moja sokoine,kua muasisi tu(eshimu mawazo yangu)
2.nilisoma kitabu cha historia ya marehem nikiwa darasa la nne,machozi yalinitoka sana

Usilolijuwa ni usiku wa kiza. Hao vilaza, ndio walioifikisha Tanzania kuwa maskini wa kila kitu, kuanzia elimu mpaka akili.
 
Namkumbuka kama mtu aliyethubutu kuliko yoyote yule katika historia nzima ya uongozi wa Taifa hili. Alifanya kile alichoamini kingekuwa msaada kwa watanzania bila kuogopa wala kumuangalia mtu usoni. Yule bwana alitangulia mapema mno mbele ya haki. Angelitusaidia kufahamu vizuri ina maana gani kutakiwa kujenga Taifa.Maana tumeua kila kiwanda...tumeua hata uzalendo...tumeanza na kuhalalisha kijiibia wenyewe kwa maneno mengi yasiyo na tija. Infact we are in shit and big mess now by the choices and decisions we have been making since his death.
 
Usilolijuwa ni usiku wa kiza. Hao vilaza, ndio walioifikisha Tanzania kuwa maskini wa kila kitu, kuanzia elimu mpaka akili.

Sio nyinyi mlio katika system baada ya kifo chake? Maana nyinyi mko paradiso bwana...mnakula hata msipopanda na kuhalalisha hata visivyo halali. Ndio maana Cheyo alishangaa juzi inakuwaje serikali inatumia hela ambazo hazijapitishwa wala kupata kibali chochote kile na bunge. Hili ndio Taifa ambalo nyinyi mnaojiita "system at work" mnalijenga kwa nguvu zenu zote. Taifa linalowawezesha nyinyi wachache tu kula na kuvimbiwa.
Ndio maana mtoa mada na wengine ambao hawako ndani ya system hii muflisi tunamkumbuka mtu kama Sokoine. Maana aliwadhibiti watu ambao wako ndani ya system ili kuneemesha matumbo yao tu.
 
Nilikua drs la kwanza mwaka huo. Nakumbuka aliachia uwaziri mkuu ili aende kusoma nje ya nchi. Hivi ni kiongozi gani (kati ya waliopo madarakani) anayeweza kuthubutu kufanya hivi!!!!!! Sasa hivi hata wabunge wanajipendekeza ili wapate kuteuliwa!!!
 
Sio nyinyi mlio katika system baada ya kifo chake? Maana nyinyi mko paradiso bwana...mnakula hata msipopanda na kuhalalisha hata visivyo halali. Ndio maana Cheyo alishangaa juzi inakuwaje serikali inatumia hela ambazo hazijapitishwa wala kupata kibali chochote kile na bunge. Hili ndio Taifa ambalo nyinyi mnaojiita "system at work" mnalijenga kwa nguvu zenu zote. Taifa linalowawezesha nyinyi wachache tu kula na kuvimbiwa.
Ndio maana mtoa mada na wengine ambao hawako ndani ya system hii muflisi tunamkumbuka mtu kama Sokoine. Maana aliwadhibiti watu ambao wako ndani ya system ili kuneemesha matumbo yao tu.

Hakuna alichodhibiti Sokoine, Nyerere ndio aliokuwa kinara wa kila kitu, Sokoine was just a vuvuzela, mechi wanacheza wengine.

Hakuna anaestahiki sifa, si Nyerere si Sokoine, wao ndio walioigaragaza Tanzania. Ukipenda usipende, hivyo ndivyo ilivyo.
 
Kivipi wameigaragaza Tanzania? Ina maana hata baada ya miaka yote hii ambayo hawa watu wawili wamekuwa nje ya uongozi hatujapata dawa ya kutibu matatizo tuliyonayo? Kwani Nyerere ndio aliuza na kugawa bure rasilimali za nchi na akaleta siasa uchwara za kujuana na kulindana hata kama ni wahalifu? Inatusaidia nini tunapojaribu kusukumia matatizo yetu sisi watanzania wa leo kwa wakoloni, na Nyerere wakati tunaofanya maamuzi na kuendesha nchi ni sisi tena bila ushawishi wao?
Mkubwa tupende tusipende nyinyi mnaojiiita "system at work" ndio mnatugaragaza watanzania. Mko kimaslahi zaidi kuliko kikazi. Mna njaa za kupitiliza! Mnataka kuvuna msipopanda! Mnalea hata yasiyolelewa popote pale ulimwenguni. Hayo ni matatizo ya Nyerere na Sokoine au ni ya kwetu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Heri yenu nyie ambao hamjaigaragaza Tanzania, haiwezekani 38 years baada ya mtu kufa bado watu wamwone wa maana wewe umwone kichaa, ukweli haujifichi,

ngoja Hawa wa sasa wafe kama kuna mtu atakaye hata hiyo ndege,sana sana tutaenda makaburini kwa wingi to make sure kafa kweli mana wanatupeleka mpera mpera kweli!

I still doubt 2 things though!
1. Siamini kama kweli Sokoine alikufa kwa natural accident au ilitengenezwa! Haven't we found out till date?!
2. Ni kweli Sokoine Alimgroom Lowasa?
 
Sokoine hakuna chochote ambacho alichofanya kwa Watanzania mpaka hakumbukwe...nakumbuka wakati wake hata mitumba ilikuwa marufuku.
 
Sokoine hakuna chochote ambacho alichofanya kwa Watanzania mpaka hakumbukwe...nakumbuka wakati wake hata mitumba ilikuwa marufuku.
Kwa hali yoyote mkuu natofautiana na wewe kimsingi.

Nafikiri aidha ulikuwa mtoto au ulikuwa mhujumu uchumi mpaka usione umuhimu wa Edward Sokoine.
Sokoine was a leader of all seasons.
 
Kivipi wameigaragaza Tanzania? Ina maana hata baada ya miaka yote hii ambayo hawa watu wawili wamekuwa nje ya uongozi hatujapata dawa ya kutibu matatizo tuliyonayo? Kwani Nyerere ndio aliuza na kugawa bure rasilimali za nchi na akaleta siasa uchwara za kujuana na kulindana hata kama ni wahalifu? Inatusaidia nini tunapojaribu kusukumia matatizo yetu sisi watanzania wa leo kwa wakoloni, na Nyerere wakati tunaofanya maamuzi na kuendesha nchi ni sisi tena bila ushawishi wao?
Mkubwa tupende tusipende nyinyi mnaojiiita "system at work" ndio mnatugaragaza watanzania. Mko kimaslahi zaidi kuliko kikazi. Mna njaa za kupitiliza! Mnataka kuvuna msipopanda! Mnalea hata yasiyolelewa popote pale ulimwenguni. Hayo ni matatizo ya Nyerere na Sokoine au ni ya kwetu?

Yes, Nyerere ndio alioitia Tanzania umaskini kwa kutokuweka misingi mizuri kwa miaka 24 aliyukuwa Rais. Kwa miaka 24 kila alichofanya kimekufa kabla ya yeye hajafa, kwa sababu alikuwa hajui akifanyacho.

Alidhulumu kwa kutaifisha mali za wanyonge wachche lakini magwiji walioijuwa dunia aliwashindwa, kesi nzuri ni ya LONRHO na Tiny Rowlands, alijaribu kumtaifisha huyu, akkakikwaa kisiki, ilibidi mwenyewe arudishe mali zake bila kupenda.

Tanganyika ilikuwa ni mchi ya kwanza katika Afrika kuuuza mazao nje, baada ya kuja Nyerere na siasa zake mbovu ikawa nchi maskini duniani na ikawa inaomba omba nje hata kula ikawa shida. Kaachia madaraka, mchi hii haina hata senti mbovu ya kigeni, viwanda vinakufa kwa kuliwa, ukabila idara zote za Serikali na Umma. Kila kitu hohehahe. Ardhi kubwa ya Tanzania kaigawia kanisa katoliki.

Unajuwa kuwa mmiliki mkubwa wa Ardhi Tanzania baada ya Serikali ni kanisa katoliki? Kwanini?
 
Sokoine hakuna chochote ambacho alichofanya kwa Watanzania mpaka hakumbukwe...nakumbuka wakati wake hata mitumba ilikuwa marufuku.
Jambo la ajabu sana ni kuwa mavuvuzela ya CCM ya sasa hayataki kabisa sifa za uadilifu za Nyerere na Sokoine ziwe zinatajwa.Lakini hao viongozi wao wakiwa kwenye public wanajidai kusema viongozi hao wazamani ni mfano wa kuiga.Unafiki mtupu.
 
huyu jamaa alishushwa kwa ajili ya kazi moja tu ya kutuongoza watanzania.
viongozi wa sasa ni uharo mtupu.
 
nilikuwa std 2 na shuleni tulikuw tumeingia saa sita na tunatoka saa kumi. mwalimu mkuu alipotuaga jioni alitutangazia. tulishangaa sana sisi tuliokuwa wadogo kwani wale wakubwa darasa la saba walikuwa wanalia.
home wazazi walikuwa hawana raha utafikiri wamefiwa na wazazi wao. jaman enzi zile ilikuwa huzuni sana.

R.I.P Edward Moringe Sokoine
 
wanaosema sokoine groom lowassa wanamkosea adabu sokoine. sokoine wakati anakufa alikuwa na jozi tano tu za viatu. alikuwa anaishi nyumba ya kawaida kijijini kwake monduli juu, sidhani kama alimfahamu lowassa zaidi ya kusikia kutoka usalama wa taifa jinsi lowassa alivyokuwa anaponda mali kufa kwaja pale AICC kama mkurugenzi mtendaji. never even in his dead body could sokoine think of promoting or grooming the national LOOTERS
 
Ndugu zangu,

KUNA wengi tunaokumbuka tulikuwa wapi siku ile ya tarehe 12 Aprili, 1984 wakati Mwalimu Nuyerere alipolitangazia taifa kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine kilichotokana na ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi waliozaliwa baada ya 1984 hawajui sana habari za Edward Moringe Sokoine . Mimi nilikuwa Kidato cha Pili tu pale Sekondari ya Tambaza. Nakumbua ilikuwa majira ya saa kumi jioni. Nilikuwa natembea kwa miguu kutoka Kinondoni ’ A’ kuelekea nyumbani Kinondoni Biafra. Nilipofika maeneo ya jirani na Msikiti wa Mtambani nikasikia wimbo wa taifa unapigwa.

Nilihisi haraka kuna jambo kubwa la kitaifa limetokea. Nikasogea kwenye duka la jirani. Wapita njia wengine nao walisogea mahali hapo. Wimbo wa Taifa ulipomalizika, nikamsikia Mwalimu akianza kutamka kwa sauti ya huzuni; ” Ndugu Wananchi, leo hii…” Kilichofuata ni historia ambayo hapa nashiriki kuiandika.

Naam, Sokoine alikuwa kiongozi wa kweli ambaye daima alisimama upande wa umma. Ni Sokoine aliyetufanya hata tuliokuwa sekondari wakati huo, tuwe na imani na uongozi wa nchi. Tuwe na matumaini ya maisha bora kwa siku za baadae.

Ndio, ukitoka kwa Mwalimu, ni Sokoine pia aliyechangia katika kutufanya watoto wa wakati huo, tuamini na tuipende siasa. Alikuwa mfano wa kuigwa. Alishi kama alivyohubiri. Siyo tu hakujilimbikizia mali, halipunguza hata mali zake ili apate nafasi zaidi ya kututumikia Watanzania.

Itakumbukuwa, kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Aprili, 1984, Sokoine alikabiliana n ahoja za wabunge kutaka kuongezewa posho na marupurupu yao. Sokoine alitamka;

” Ndugu Spika, niko tayari kuwaongezea wabunge posho ya chakula chao, lakini kamwe sitakuwa tayari kuwaongezea mishahara na marupurupu mengine.” Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye Edward Moringe Sokoine. Alikuwa kiongozi wa kanuni na mwenye msimamo usioyumba.

Sokoine alielewa, kuwa ukiwalinganisha na wananchi walio wengi, wabunge walikuwa na hali bora zaidi kimaisha. Alikuwa tayari kuchukiwa na wabunge kwa kutetea maslahi ya wanyonge, kuliko kupendwa na wabunge kwa kujali zaidi maslahi yao.

Baada ya kikao kile cha Bunge, Edward Sokoine, badala ya kupanda ndege ya Serikali kumrudisha Dar es Salaam, aliamua kurudi Dar Es Salaam kwa njia ya barabara, afanye hivyo ili mle anamopita apate nafasi ya kuona shughuli za maendeleo zifanywazo na wananchi. Sokoine hakufika Dar Es Salaam, mauti yakamchukua kwa ajali ya gari pale Wami- Dakawa, Morogoro.

Leo tuna viongozi wa wananchi wenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi. Viongozi wasiotosheka na posho ya elfu sabini ya kikao. Viongozi wenye kufikiria tu ’ kamuhogo kao’. Wanafikiri magari na marupurupu yao badala ya masuala yenye kuwahusu wananchi wa kawaida.

Je, Sokoine angefufuka leo ingekuwaje?
Bila shaka angefufuka na kufa tena ndani ya siku saba. Maana, Sokoine angeshangaa kuwaona wabunge wa leo wakichukua posho ya kikao cha siku moja sawa na mshahara wa miezi miwili au mitatu kwa Watanzania walio wengi.

Sokoine angeshangaa kuona wabunge hawatembelei tena Landrover za bei nafuu bali magari ya kifahari huku wananchi walio wengi bado wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi. Kwamba bado kuna wanyonge wengi wasio na hakika ya kula yao ya leo na kesho huku wananchi wakiambiwa, tena na Spika wa Bunge, kuwa Bunge ni eneo la umasikini!

Sokoine angeshangaa kusikia kuwa uongozi siku hizi unanunuliwa, na hata yeye akijaribu tena kuingia Bungeni atalazimika agawe ’ Vimuhogo’ kwa watakaompitisha kwenye kura za maoni. Sokoine angeshangazwa pia kusikia, kuwa kuna mawaziri na watendaji wakuu serikalini wanaokaa mahotelini kwa kukosa nyumba za serikali kwa vile umepitishwa uamuzi wa kuziuza, kisha kujenga nyingine na kuziuza tena!

Lakini, Sokoine angeshangaa zaidi kuona Watanzania aliowaacha mwaka 1984 wamechelewa sana kuamka na kupambana kuibadili hali iliyopo.

Naam, Sokoine angefufuka leo, angesononeka sana kuona pengo pana lililopo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kati ya viongozi na wananchi.

Edward Moringe Sokoine, Daima Tutakukumbuka.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Maggid,

Umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka wakati huo nikiwa darasa la saba. Nilikuwa ndiyo nafika nyumbani nikiwa bado sijabadili hata unifomu zangu nilisikia wimbo wa taifa na baada ya hapo Rais J. K. Nyerere alitamka maneno yafuatayo na nakuu ''Ndugu wananchi leo hii saa saba na nusu mchana, ndugu yetu na kijana wetu, Ndugu Edward Moringe Sokoine alipokuwa safarini kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam gari lake lilipata ajali. Amefariki Dunia''.

Nakumbuka baada ya hapo nyimbo za maombolezo za jeshi zilianza kupigwa mfululizo na siku hiyo sitaisahau kwani Mama yangu mzazi alilia na nakumbuka hata chakula cha jioni hakushiriki. Kwa kweli ilikuwa ni majonzi makubwa sana na kamwe sitasahau kifo cha shujaa wetu wa kweli.
 
Sokoine hakuna chochote ambacho alichofanya kwa Watanzania mpaka hakumbukwe...nakumbuka wakati wake hata mitumba ilikuwa marufuku.

Ulishaona wapi nchi ya wavaa mitumba iliyoendelea? Yaani fikra zetu ni mbofu mbofu sana....kama tungekomaa na textile industry yetu wakati ule leo hii tungekuwa mbali sana. Kwa mfano Lesotho na Uganda walinufaika sana kwenye ule mpango wa AGO wa kuuza bidhaa marekani. Sisi tulikuwa tunauza nini? Mitumba? Hivi nchi gani iliyoendelea kwa kutoa hotuba na maneno mengi yasiyo tekelezeka kweny dunia yetu ya leo? Lets be serious...maendeleo hayaji kwa kuiba mali ya umma na kugawana UDA au kwa kuanzisha kampuni ya ujenzi inayoitwa TAKOPA.
 
wengine tulikuta historia yake tu! Ila nakumbuka wakati nipo darasa la nne tulipata mwalimu wa uraia mzuri sana, alikuwa haishi kutusimulia matendo ya edward sokoine! Na ilikuwa ikifika tarehe aliyotoweka, tunaimba nyimbo nahisi zilizoimbwa wakati wa kifo chake! Huwezi amin, kwa ile tu kuoneshwa picha zake na kusimuliwa historia yake, wengi wetu tulilia kama vile ametoweka siku hiyo! Eee mungu, ibariki tanzania izae mbegu za kina moringe na nyerere!
we mtoto mwogope mungu hapakuwa na somo la uraia wakati huo acha kabisa kulikuwa na somo la elimu ya siasa au ukipenda siasa uraia mmeleta juzi na elimu za mawaziri wenu wanaobadili mitaala kuwa mara tatu kama dozi ya asprini
 
wanaosema sokoine groom lowassa wanamkosea adabu sokoine. sokoine wakati anakufa alikuwa na jozi tano tu za viatu. alikuwa anaishi nyumba ya kawaida kijijini kwake monduli juu, sidhani kama alimfahamu lowassa zaidi ya kusikia kutoka usalama wa taifa jinsi lowassa alivyokuwa anaponda mali kufa kwaja pale AICC kama mkurugenzi mtendaji. never even in his dead body could sokoine think of promoting or grooming the national LOOTERS

Mwikimbi,

..miaka hiyo karibu viongozi wote walikuwa waadilifu.

..wanasiasa wengi sana walibadilika wakati wa awamu ya pili.

..kwa mfano, Horace Kolimba alikuwa msaidizi wa Sokoine lakini ktk awamu ya pili akawa kiongozi wa hovyo-hovyo.

..Mkapa naye amefanya kazi muda mrefu chini ya Mwalimu Nyerere lakini ameishia kwenye ufisadi.

..binafsi sioni ajabu kusikia kwamba Lowassa aliwahi kufanya kazi na Sokoine.

NB:

..Sokoine alikuwa akiishi ktk makazi ya Waziri Mkuu Ikulu ya DSM.

..Monduli Juu ilikuwa ni kijijini alipozaliwa.
 
Unajuwa maana ya uadilifu au unajisemea tu? Anti Corruption ya Tanzania ilianzia awamu ya kwanza ikendeshwa na Maftah. Viwanda na mashamba alivyodhulumu Nyerere kwa mabepari vilianza kuliwa na kuuliwa wakati wa Nyerere. Viwanda alivyojengewa Nyerere na wachina, vilianza kuliwa na kuuliwa wakati huohuo wake. Mpaka anang'atuka, nchi iko hohehahe kwa uzembe na kutokuwajibika kwake na kwa viongozi aliowaweka madarakani, huo uadilifu unaousema wewe ni upi?
 
Back
Top Bottom