Siku nikiwa Rais wa Tanzania nitafanya zaidi ya Magufuli

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Tanzania ni nchi kubwa sana kwa maana ya eneo lake na idadi ya raia wake ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika na hata Ulaya na Asia.
Ni ukweli ulio wazi kwamba rais Magufuli kafanya mengi mazuri sana yenye tija na maamuzi magumu kwa nchi.
Pamoja na hayo yote mazuri lakini siku nikiwa rais wa Tanzania nitafanya mengi zaidi ya aliyofanya Magufuli ili kyifanya Tanzania kuwa bora zaidi kwa maana ya maisha yao kuwa bora zaidi kuliko sasa.
Nitafanya yafuatayo kumzidi magufuli:

Kwanza nitaanzisha sera maalum ya kulinda viwanda vya Tanzania yaani PROTECTIONISM kama walivyo fanya mataifa ya Ulaya na Marekani wakati wa mwanzo wa ubepari
Kwenye hili nitapiga marufuku kuagiza nguo za mitumba kutoka nje ili viwanda vyetu vya nguo viweze kutengeneza nguo za kutosha kwa soko kubwa la Tanzania.

Pili nitapiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje. Tena hili nitalifanya kwa kujua kabisa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye mito mingi sana isiyo kauka mwaka mzima hivyo uwezo wa juzalisha sukari utakuwa guarantee. Kwa kufanya hivyo viwanda vya sukari vitazalisha ajira nyingi sana lakini pia wakulima watapata masoko ya kuuza miwa na hivyo kuwa na pesa nyingi mifukoni mwao.

Mafuta ya kula itakuwa ni marufuku kuagizwa kutoka nje ya nchi.
Huwa sielewi kinachotufanya kuagiza mafuta yote safi na ghafi kutoka nje huku michikichi ya Kigoma na alizeti ya Singida na karanga za Tabora vikikosa watu wa kuvifanyia kazi. Nitaifanya mikoa hiyo kuwa wazalishaji wakuu wa mafuta ya kula kwa Tanzania mpaka nje ya nchi.

Nitabadilisha mfumo wa elimu ili uwe Tanzania oriented. Mazingira ya Tanzania ndiyo yata determine nini watoto wasome. Utasomaje topic ya Glaciation kwenye mazingira ya Dodoma ambayo hata siku moja hayawezi kukusaidia wala kusaidia nchi.

Sintoruhusu bidhaa za nyama, maziwa na ngozi ziagizwe kutoka nje. Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu Afrika zenye mifugo mingi sana lakini cha kushangaza bado tuna agiza maziwa, nyama na viatu vya ngozi toka nje?
Nitaweka Embargo pia kwenye bidhaa za samahi. Huwa naudhika sana kuona samani za ofisi nyingi za umma na hata ofisi binafsi wakitumia bidhaa toka nje wakati Tanzania ina misitu mingi sana ya asili na ya kupanda.

Nitapiga marufuku kuagiza chakula kutoka nje kwani Tanzania ina ardhi nzuri sana kwa kilimo lakini pia tuna mabonde mengi yanayofaa kwa kilimo wakati wa kiangazi.

Lakini pia utalii utakuwa kipaumbele kwani Tanzania kwa Afrika inaongoza kuwa na vivutio vya utalii ikiwemo mlima mrefu kuliko yote Afrika ambao uko kwenye Tropic lakini bado una barafu licha ya kuwa katika hali ya hewa ile, kuna Serengeti, Ngorongoro na Ruaha.
Nitaanzisha miradi mikubwa ili itoe ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu na kati ili kupunguza tatizo la ajira. Hapo reference yangu itakuwa Marekani wakati wa anguko la uchumi la miaka ya 1930s

Nitahakikisha kila mji hapa nchini unapata maji safi na salama lakini pia uhakika wa umeme. Nitaanzisha kampeni ya nyumba bora kwa kila raia wa nchi hii. Hapa kipaumbele itakuwa ni vijijini.
Kusema kweli nimejipanga kuivusha nchi hii kwenda mbali kabisa kwa kila nyanja.
 
Nearly an old man can withstand adversity but If u want to test the man's character,give him power!
 
Hahahaa, nitakupa kura ila hayo ni machache ongeza zaidi, mfano, vipi suala la demokrasia, vipi kuhusu haki za binadamu?
 
Protectionism na hayo ma Embargo usawa huu wa soko huria huoni utaitenga nchi na dunia nyingine! Wanachofanya sasa kuongeza kodi kwenye bidhaa za nje ambazo si za msingi na pia zinazopatikana ndani ya nchi bado ni sera nzuri kwa mtazamo wangu.

Mambo ya karne ya 18, 19 na 20 ni tofauti kabisa na haya ya karne ya 20 tuliyopo. All in all, kwa aina ya utawala tunao ushuhudia awamu hii, kila mtu ana sifa ya kuwa rais, Rc, Dc, DED, nk. Ni tofauti kabisa na hapo awali.
 
Endapo nikiwa Rais ninafanya yafuatayo
1.Kila kata inakuwa na chuo cha ufundi, na kila tarafa inakuwa na sekondari moja, Yaan wanaofaulu daraja A, Wanaenda shule zetu za vipaji kama MINAKI, TABORA, PUGU, ILBORU , KIBAHA , MZUMBE, wanaofaulu daraja B wanaenda hizo za Tarafa, hii inaondoa kuwachanganya watu wenye interest tofaut kwnye darasa moja, wenye uelewa tofauti kwenye darasa moja, alafu sasa wale wa Daraja C na D wanaenda kwenye shule za ufundi hizo zilizopo kila kata, Hapa lazima tukubali kwanza wekezaji wa wachina na mabeberu kwenye mitambo ya kufundishia, ELIMU YEYOTE LAZIMA IWE NA PYRAMID STRUCTURE, CHUO KIKUU ISISWE FASHENI LAZIMA WAFIKE WACHACHE,

2.Elimu ya chuo kikuu, na mikopo ya bodi.
Hapa kwanza waliokopa mwanzo lazima warejeshe, pili kila kiongozi mstaafu au mwenye dhamana awe na fund raising system ya kuchangia elimu, haiwezekani akina Mkapa , Kikwete , walioba wasome tu free then hawajaacha mazingira sahihi kwa wanaofuata ,wanachofanya ni kutengeneza mazingira ya watoto wao,

3.KILIMO NA MAZAO
Wananchi wote wanatakiwa kujua kwamba mazao yao yatanunuliwa na serikali na kuuzwa kwa bei kulingana na soko lilivyo, pia wajue kwamba pembejeo na kila uwezeshwaji kwenye ishu ya kilimo lazima iwe solved na serikali

4.RUSHWA NA UFISADI
Walioiba huko Nyuma siwagusi nawaambia wakiri tu makosa ila atakayeiba kwenye uongozi wangu namnyonga , sina simile

AISEE NI MENGI SANA


Britanicca
 
Huna akili ndio maana hujawa Raisi Hadi Sasa ungekuwa na akili ungekuwa raisi
 
Hujasema pesa utazipata wapi au utaendelea kuwanyonya wanyonge kupitia kodi?

Binafsi sitakuchagua make mikakati yako ni ya kufikirika tu.
 
Back
Top Bottom