Siku Mwanakijiji atakapokutana uso kwa uso na Lowasa..Itakuwa Vipi?

Swali hili lilikuwepo siku za nyuma,wakati bwana mkubwa akiwa anaongozana na ma-body guard kibao. Leo hii yeye kama Mbunge wa Monduli tu (na sio Waziri Mkuu msaafu maana kaachia ngazi)hana hao wakinga mwili itakuwaje?
Maana EL anajuwa kuwa mchango wa Mkjj ktk habari umechangia kwa kiasi fulani yaliyojitokeza ndani ya jengo na kujenga historia mpya ya nchi yetu.
Nahisi EL atapanisha mori na patakuwa hapatoshi hivyo Mkjj anza mazoezi ya riadha ili yakusaidie siku hiyo ikifika.
 
Ataanza kumsomea hiyo otuba ya rais uku akilia kama mkewe,,,kwa kuwatesa watanzania wasio hatia....na kumshukuru kwa kungatuka
""Hotuba ya Rais Kikwete

Leo asubuhi nimepokea barua ya Waziri Mkuu ya kujiuzulu kwa masikitiko makubwa kwani tumefanya naye kazi muda mrefu na nilitegemea atumie vipaji vyake vingi kuongoza serikali yangu kwa muda mrefu. Wengi mtakumbuka enzi za Boyz2Men. Nasikitika sana kwa hatua taifa letu lilipofikia.

Aidha, nimepokea na kusoma ripoti ya Dr Mwakyembe kwa masikitiko maradufu ya yale yaliyonipata kwa barua ya ndugu Lowassa. Sina mengi ya kusema, ila jioni hii naomba wananchi mnipe ridhaa yenu kuanza mchakato wa kina wa kuondoa taifa hili kwenye dimbwi la ufisadi, ubadhirifu, wizi, utawala wa ki-imla, na kutojali matakwa na malalamiko ya wananchi.

Awali ya yote nikiri kwamba kwa miaka yote niliyokuwa kwenye shughuli na uongozi wa uma, lazma kuna nyakati chache ambazo nami niliwahi kuterereka kimaadili. Pale matendo yangu hayakukidhi mategemeo ya wananchi naomba msamaha wao. Hata hivyo inafika wakati nchi kusafishwa kwa manufaa ya umma. Bila hivyo nchi yetu itasambaratika kama majirani zetu na nchi nyingine kama USSR, Yugoslavia nk. Nimenuia kuiokoa nchi yetu toka kwenye hatma hii, na kwa hili nitaomba na kuhitaji msaada wenu. Hatua za awali.

Kwanza, nakataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kama hakuandamani na kujiuzulu kwa baraza lote la Mawaziri ili nianze upya kuomba kibali cha kuwaongoza wananchi bila fununu za ufisadi na bila dharau kwa serikali yao.

Pili, natangaza kugandisha (to freeze) akaunti zote za mali za wale waliohusika na shutuma za Richmond, na BoT, pamoja na kushika rehani mali zao zote zisizohamishika kwa nia ya kurudishia serikali mali yoote ambayo inaweza kuwa iliibiwa na washutumiwa. Ili wasife njaa serikali itaendelea kuwalipa nusu mshahara hadi uchunguzi au mashtaka kumalizika.

Tatu, nawahimiza viongozi wote waliojihusisha na ufisadi wowote wa kimsingi kama kwenye mikataba ya madini, Netgroup Solutions, Uuzaji wa Mashirika na Raslimali za Umma, Ununuzi wa rada na ndege ya Rais, Ununuzi wa vifaa vya Jeshi, Mikataba na TANESCO kama IPTL, Kiwira, nk, wakiri kwangu kimaandishi kushiriki kwao na kuorodhesha mali walizopata kutokana na matendo hayo. Wakifanya hivyo sitawachukulia hatua za kisheria ila nitawasimamisha kazi ya umma na kurudisha mali ya wananchi panapohusika.

Wasiojitokeza kwa hiari naagiza vyombo vyote vya uchunguzi vya dola kufuatilia kwa undani na waletwe mbele ya sheria mara moja.

Ndugu wananchi, hii vita dhidi ya wabadhirifu itahitaji ushirikiano wenu na naomba mniunge mkono kwa kila namna.
Nimeagiza vyombo husika kuhakikisha watuhumiwa hawawezi kutoroka au kutorosha mali hadi uchunguzi umalizike. Aidha nimeagiza vyombo vya dola viwe macho kudhibiti wakorofi wachache watakojaribu kuleta ghasia.

Mungu ibariki Tanzania.

Asanteni.

(Anavua miwani, anafuatwa kwenye jukwaa na Makamu wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Chadema, CUF, UDP na kuzingirwa na Chief Justice, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Polisi na Mkuu wa Magereza. Wanatoka nje ya Bunge kwa hatua kakamavu za kijeshi. Wabunge wanasimama na kumshangilia kwa nderemo na vifujo)!!!!!!

Hii kazi kweli kweli. Watu ni lazima wajisalimishe

hIIIIIIIII HUUUWIIIIIIIII WEWE BABA UMETULETA HAPA ULIPO HIIII
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom