Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kuna watu unaweza ukadhani wana akili ila utashangaa wanamlinganisha Mwalimu Nyerere na hawa viongozi 'wakuja' ambao hata historia ya miaka 20 iliyopita hawaijui achilia mbali ya miaka 100 iliyopita.
Niliwahi kuambiwa kuwa kuna siku, nadhani itakuwa miaka ya mwishoni ya 1970s, kuna ujinga ujinga fulani Saddam alikuwa anafanya, Nyerere akafunga safari hadi Baghdad, akamfokea Saddam (yes, Saddam huyu huyu ambaye kuna baadhi ya viongozi wetu wanatuambia alikuwa mzuri sana), halafu akapanda ndege akarudi zake Tanzania.
Nyerere akamwambia dawa yake iko jikoni. Nadhani haikupita muda vita ya Ghuba ikaanza.
Nitawatafuta watu wanaoijua hii story halafu nitarudi niijazie nyama zaidi ila kama kuna wanaoijua waweza kutuhabarisha zaidi.
MASAHIHISHO: Nilichanganya miaka ya kabla ya vita vya Ghuba nikasema mwishoni mwa 1970s badala ya mwishoni mwa 1980s. Hii ni kwa sababu nilikuwa nawaza vita mbili tofauti (Vita ya Ghuba vs Vita ya Iran na Iraq) huku nikiwa sina uhakika ni vita ipi iliyofuata baada ya tukio nililotaja.