Siku Musa alipoikataa nyumba ya Farao na Siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku Musa alipoikataa nyumba ya Farao na Siasa za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 11, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Kwa imani, Musa alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. Akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi kwa kitambo kidogo tu. (Waeb. 11:24,25)

  Mojawapo ya masimulizi ya vitabu vya dini za Kikristu na Kiislamu ambayo yanakubaliana sana na kulingana kwa kiasi kikubwa ni lile simulizi la Nabii Musa. Jinsi gani alizaliwa, wapi alizaliwa, kwanini alitelekezwa, na jinsi gani mama yake alipata nafasi ya kumnyonyesha kwa ruhusa na baraka ya nyumba ya Farao (Firauni – nitatumia maneno haya kwa kubadilishana) yote yanalingana sana.

  Na pia jinsi ambavyo ilimlazimu Musa kuikimbia nyumba ya Farao na fahari zake zote, utajiri wake na elimu yote ambayo aliipata kule na kwenda kuunganika na Wanawaisraeli waliokuwa Utumwani kule Misri na kwa uamuzi wake huo kujiweka kuwa ni adui wa kudumu wa Farao.

  Haya yote yanaonekana katika Agano la Kale la Biblia Takatifu na katika Qurani Tukufu. Hata hivyo, kwa namna ya pekee mwandishi wa kitabu cha Waebrania anatueleza kwa namna ya pekee kabisa ni kwa sababu gani Musa aliicha nyumba ya Firauni. Mwandishi anasema "Kwa imani, Musa alipokuwa mtu mzima".....


  .....Watanzania wenzangu, mnaweza kufikiria nazungumzia habari za dini. Kwa namna fulani inaweza kugusa dini lakini hayo nitawaachia wachungaji, mapadre, mashehe na walimu mbalimbali wa dini.  Mimi nazungumzia haja na ulazima wa watoto wa Tanzania kukataa kuitwa wana na mabinti wa Utawala wa Kifisadi! Simzungumzii Musa wa Biblia wala Farao wa Misri; siwazungumzii wana Waisraeli wa Mashariki ya kati. Nazungumzia mahusiano kati ya watawala na watawaliwa wa hapa Tanzania....


  Makala hii imetoka kwenye Tanzania Daima.
   

  Attached Files:

  Last edited: Jun 11, 2009
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Asante MMKJJ kwa simulizi mwananana ya Siku Musa alipoikataa Nyumba ya Farao na Maamuzi ya Mtu Mzima.

  Niko na wewe katika maamuzi ya Musa alipokuwa mtu mzima akaamua kuikataa nyumba ya Farao, ila siko na wewe katika Watu wazima wetu unaodhani wamekuwa Watu wazima ukiamini watakuwa tayari kuikataa nyumba ya Farao, umepotea.

  Enzi za Musa kulikuwa na genuinity na drive behind ni uchungu wa dhati dhidi ya nduguze Waebrania. Watu wazima wenu ni wanafiki na drive behind sio uchungu kwa Watanzania, bali wana agenda zao, na amini usiamini the drive behind ni njaa zao, hata kama kiranja anaonekana ni mtu wa shibe, tajiri na msamaria mwema lakini pia ana lake jambo, the bottom line ni njaa. Sio lazima njaa ya tumbo, hata njaa ya madaraka ni njaa. Njaa ya kutaka kuabudiwa ni njaa, njaa ya kulalamika kila siku kuwa unaonewa pia ni njaa.

  Unafiki ninaouna hapa ni kujidai umekuwa mtu mzima kutaka kuondoka nyumba ya Farao huku unamkumbatia huyo huyo Firauni. Hivi anayeongoza Misri ni nani?. Ni Farao, maroroso yote yanayotokea Misri kuwanyanyasa wana wa Israel, yanabaraka za Farao, Musa alimkataa Farao na mambo yake yote. Watu wazima wetu, wanamkubali Farao ila wanayakataa mambo yake yote kama alivyofanya Mrema 1995. Hawa waliobaki ni wanafiki tuu na hili litathibitishwa with time.

  Mzee Mwanakijiji nakuaminia kwa insight uliyonayo, lazima unaweza kuona ajenda ya kiranja wao anayepiga kelele za ufisadi huku ana ajenda yake akimpaka mafuta Farao kwa mgongo wa Chupa, eti "ni rafiki yangu mkubwa"?!. Kwa vile saa hizi ni kelele za ufisadi zimepamba moto, tuwe wote kwenye hili, ajenda zitakapoibuka, tutafarakana maana kitakacho fuatia ni anguko la wanafiki.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jun 11, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Surely MKJJ tatizo ni kuwa kabla Mussa hajaenda kwenye jengo la kifalme alizaliwa huko 'tandale' akatupwa mtoni na kama zali akaingia Ikulu.

  Baadae alijijua kuwa yeye ni mwebrania na akawatetea watu wake.

  Lazima tukae chini kutafakari je, ufisadi unaanzia mara tu mtu anapopata uwaziri au urais?? au unaanzia huku kwenye kata, mashuleni, kwenye taasisi za umma, michezo....then tunawachagua mafisadi wakubwa zaidi kuwa viongozi!

  Tunakazi tunatakiwa kupigwa shule ya Mungu! Jangwani Miaka 40! hili watanzania hatutaki kulisikia!
   
 4. F

  Felister JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee MM what if you would try to be David and not Moses? Chukua kombeo achilia jiwe kwenye paji la uso wa Goliat na sisi wakike tutakupokea kwa kelele za Mfalme aliua elfu lakini Daudi ameua makumi elfu. Alafu unajua nini ile technology ya Musa ya kugawa bahari ya Sham kwa fimbo imepitwa na wakati ipo hii ya 21st century ya mwanaume wa wanaume yeye anaenda against natural forces hahitaji kugawa maji na kupita nchi kavu yeye anatembea juu ya maji bila kuzama. Unaionaje hii kwanini utumie analogy (sp?) technology wakati ni enzi za electronics hizi. Enzi hizo za Musa walitakiwa kusoma mbao za mawe kuzijua sheria siku hizi tunatembea nazo ndani mwetu na tunauwezo wa kuinfluence hata wasio penda kwasababu tunazo funguo. "All the powers and authority is given to me and I am giving them to u to go and make my desciples!" But why are the sons and daughters of the King live like slaves? Because they are hold captive at the will of the devil; for these they dont need prayer they need the knowldge of their father for they resist themselves; but with them I command u to instruct them humbly with patience and all deligence as they are not like Yambre and .... who withstood Moses for these I tell u turn away from them as they are always searching truth while denying it and because of their nature they will never find it; they covet; sleeping inside the widowed houses, Idiolators; people of no faith; hypochrites, wicked and witches...for them the end is near for they will not continue for so long before they fall.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Watoto wa tanzania wakubali kuwa ufisadi na mafisadi, na si kitu kingine, ndicho kincholeta umasikini wa nchi hii, halafu waendelee bila kumtazama mtu usoni, In ballot box kusema SASA BASI... INATOSHA.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Off tangent, ku attribute hizi story kwenye bible ni sawasawa na ku-attribute "The Merchants of Venice" kwa wasemaji wa kiswahili kwa J.K Nyerere, bila kumtaja William Shakespeare.

  Hizi story zilikuwapo kabla ya Musa na Webrania walikuwa wasanii tu walio zi plagiarize na kuzifanya zao.

  I get your deeper meaning, though I am appalled by the level of miseducation carried by the his-story behind, although the intentions are good, the effect is further miseducation.

  A 4.6 BILLION YEAR OLD PROPHECY

   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jun 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Aaaah wewe na hii mi conspiracy theories yako bana....
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hakuna conspiracy theory unapoiona, hiyo niliyotoa hapo ni expose ya conspiracy theory, the conspiracy theory being the bible.

  The bible authors conspired to monopolize world culture and religion by plagiarizing and faking these story as their own.

  Who is giving a conspiracy theory now?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jun 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  The one saying the bible is a conspiracy....
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wabongo ndivyo tulivyo; Bluray, ukitaka kuzungumzia the history of the bible, the conspiracy and whatever have you why not start a thread kule kwingine bila ya kulazimika kuhijack mada nyingine?

  Haya ya kusema kuplagiarize mbona hadithi zetu nyingi za sungura na fisi ambazo tuliamini ni za kiafrika kumbe msingi wake ni hadithi za Hisopo (Aesop). Sasa ndiyo ulimwengu ulivyo na mfano wa Musa hapa hauna lengo la kuzungumzia bible authorship (kama ni ya kiungu au ya kibinadamu).

  Ndio maana nimesema hapo juu "mimi nazungumzia...".

  Mfano niliotumia wa Musa was not intended to be "all inclusive" na kufananisha kila kitu kwa kila jambo kama wengine wanavyochukulia.

  Kwamba Musa aliweza kuikataa nyumba ya farao yawezekana kulisababisha na hali halisi iliyomkuta na bila ya shaka haikuwa jambo jepesi lakini alijua ni la lazima.

  Ujumbe ni kuwa kuna wakati mtu mzima anatakiwa kuchukua
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,999
  Trophy Points: 280
  Tusubiri Mh Zitto na yeye achangie,naona amepotea sana hapa forum,nadhani atakuwa anaifahamu torati kwani yeye kama Muslim,anashare torati na christians.
   
Loading...