Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,908
- 30,249
- Thread starter
- #21
Mazindu...Pamoja na kumkubali sana Sheikh Ponda lakini jambo moja najiuliza, kiwanja cha kujenga chuo kikuu kinabadirishwa na kujengwa msikiti? Hivi Morogoro misikiti imejaa kiasi kwamba chuo kikuu kiwe hakina maana tena badala yake pajengwe msikiti? Hi inanifikirisha kidogo
Kuna kisa ambacho hukijui.
EAMWS ilikuwa inajenga chuo kikuu mwaka wa 1968.
Bahati mbaya sana ikatokea fitna.
Pakawa na hofu kwa nini Waislam wawe na Chuo Kikuu?
Ukazushwa mgogoro mkubwa ndani ya EAMWS na serikali ilihusika katika fitna hii kwa kiasi kikubwa.
Serikali ikaipiga marufuku EAMWS na ikawaundia Waislam BAKWATA.
Mradi wa Chuo Kikuu na miradi ya ujenzi wa shule yote ikafa.
Kiwanja hiki kikawa sasa BAKWATA wanawauzia matajiri.
Pale Sheikh Ponda alipofikia kuchukua kiwanja katika hilo eneo ili ujengwe msikiti kiwanja chote kilikuwa kimemalizika kuuzwa.
Ponda alichukua sehemu ile ndogo ili angalau pawe kumbukumbu kwa ajili ya Sheikh Hassan bin Ameir.
Rudia kusoma kisa hiki utaelewa vizuri.