Siku moja na Prof. Taji Ahmed Muhidin rafiki mkubwa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hazina ya kumbukumbu aliyonayo nyumbani kwake, ana mpango wa kuiweka wazi kwa hadhira?

Sent using Jamii Forums mobile app
Auz,
Mtu kama Prof. Muhidin ni msomi wa ngazi ya kilele na hapana shaka anajua umuhimu wa kuhifadhi ''machimbo,'' kama haya.

Hawezi kukubali kuyaacha yapotee.

Fikiria mtu nyumbani kwake ana friji inafanyakazi 24/7 ndani yake kahifadhi mikanda ya hotuba za Mwalimu kuanzia 1954.

Hizi ni hotuba za kudai uhuru.

Hotuba hizi ni zile alizokuwa akitoa Mnazi Mmoja.

Prof. Muhidin kanieleza vipi aliweza kufunguliwa hazina ya Baba wa Taifa na yeye wala si Mtanzania anaingia ndani ya chumba kile akawa anachukua na wakati mwingine kukomba kila alichokitaka tena ananambia kwa msaada wa Mwalimu mwenyewe.

Usuhuba huu kati ya Prof. Muhidin na Nyerere haukuwa wa kawaida.

Hawa walikuwa, "Two of a Kind."

Turejee kwenye mikanda yenye sauti ya Mwalimu wakati huo akizungumza Kiswahili kwa lafidhi ya Kizanaki.

Haya kanieleza Prof. Muhidin huku akicheka kwa kuwa anajua mimi ni Mswali khalis na anaelewa Waswahili huwaje tunaposikia mtu anakizungumza Kiswahili vingine.

Hii ni mikanda ya ''to reel,'' na mingine ni cassette.

Chukulia kwanza kuwa dunia hii leo hakuna ''reel to reel tape deck,'' kama vile hakuna leo gramophone.
Leo hakunaa cassette player.

Yeye Prof. Muhidin vyombo hivi anavyo.

Haya ya kwanza.

Hili la kutupia jicho naamini ikiwa mtu anataka kuangalia ''Machimbo ya Prof. Muhidin.'' kama nilivyofanya mie kisha akashika hamsini zake au ni kutafiti kwa muda mrefu bila shaka atamfungulia maktaba yake.

Msomi habanii elimu.

Mimi kanionyesha hadi chumba changu nitakachokaa ikiwa Insha Allah nitataka kwenda kufanya utafiti.

Prof. Muhidin ni msomi makini sana.

Nafikiria kuandika kitabu nikiite "Machimbo ya Prof. Taji Ahmed Muhidin."

Naamini sote tunakijua kitabu cha H. Rider Haggard, "Machimbo ya Mfalme Suleiman," (1885).

Rider Haggard alikuwa akiwaduwaza Wazungu wenzake wa karne ya 19 waliokuwa hawajui Afrika ilivyo kwa ngano za kusisimua na kutisha za Waafrika wanaoishi porini na watawala katili kama Twala na jicho lake la chongo na bibi kizee wake mchawi Gagula aliyemsaidia kuendesha serikali yake ya kidhalimu.

Prof. Muhidin nitamueleza katika Afrika inayojulikana ulimwenguni yeye akiwa kijana wa Mombasa aliyesoma Uingereza enzi za ukoloni na akaja kusomesha Chuo Cha Makerere chuo alichosoma utotoni na akasomesha na Canada.

Hakuna uchawi hapo wala ngano za kutisha hapo ni elimu pevu juu ya elimu pevu ndani ya bongo za vijana waliotaka kulikomboa bara lao la Afrika na wakimwangalia Julius Nyerere kama mfano wa kuigwa katika viongozi wa Afrika.
1659522929771.png
 
Don...
Huenda wewe hupendi chochote kinachoeleza historia ya Waislam.

Hakuna shida uhuru ni wako kuepuka kalamu ya Mohamed Said.

Hulazimishwi.

Wale wanaopenda kunisoma watanisoma kwa furaha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante mkuu, huwa kuna muda naogopa kukwaza mtu kwa comment ninayoweza kuitoa. Hivyo, ile mijadara nayohisi inaweza kuwa sensitive naikwepa sana.
 
Asante mkuu, huwa kuna muda naogopa kukwaza mtu kwa comment ninayoweza kuitoa. Hivyo, ile mijadara nayohisi inaweza kuwa sensitive naikwepa sana.
Don,
Kwanza nikufahamishe uelewe.
Unapozungumza kusema, ''sensitive,'' yaani nyeti mimi nitajiuliza nyeti kwa nani?

Mimi ninapoandika kitabu kinachoeleza historia ya Waislam wa Tanganyika jinsi walivyounda African Association (1929) kisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (1933) hadi kufika TANU (1955) kwangu hili si jambo nyeti ni historia kama historia nyingine.

Bahati nzuri ikasadifu kuwa hii ni historia ya wazee wangu.

Lakini huenda kwako kwa kuwa hufurahishwi na historia hii roho inakuuma kwa kuona mbona kwenu hakuna historia mfano wa hii?

Ukawa na hofu kuwa itakuwaje sasa historia hii imeandikwa huko kwenu kutaonekanaje?

Nini mchango wenu kwa nini kulikuwa hakuna kitu kama hiki?
Kwako hili lishakuwa tatizo.

Wewe unaona huu ni udini.

Lakini ukiingia Library of Congress catalogue ya kitabu changu ni ''Islam, politics...''
Lakini kwa ukweli na uhalisia wake hii ni historia kama zilivyo historia zote ulimwenguni.

Hii ndiyo sababu kwa kuwa ni historia kama zilivyo historia nyingine baada ya uandishi huu wa kusahihisha makosa katika historia mbayo wewe huioni nyeti wataalamu wa historia ya Afrika haraka sana wakajijongeza karibu na mimi wapate kujifunza zaidi.
 
Back
Top Bottom