Siku Moja bila Mzee Kawawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku Moja bila Mzee Kawawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shaycas, Jan 1, 2010.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kifo cha mzee Kawawa kimeacha simanzi na huzuni kubwa si kwa familia yake tu bali hata kwa Taifa letu ambalo tuna utamaduni wa kuwatunza na kuwaenzi wazee wetu.Pamoja na hayo sijaona manti ya Rais wangu kuacha kuhutubia Taifa ktk siku hii muhimu na kwa utaratibu aliojiwekea wa kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na msimamo wa serikali kuhusu baadhi ya mambo.
  Kama sababu ni msiba wa Mzee Kawawa,bado alikuwa na nafasi ya kuhutubia japo hata kuwapa wananchi moyo wa uvumilivu na ujasiri wa kuishi kwa AMANI bili KAWAWA..hakufanya hivyo,je huko ni kukosa ujasiri kwa RAIS?JE KAWAWA alikuwa/ni muhimu kuliko Watanzania wote ambao kwa kudra za Mwenyezi Mungu aliwaacha hai ili pamoja na kumtumikia YEYE wapate kusikia Hotuba ya Rais Wao? Au Rais alikuwa hajaandaa hotuba yake na au hakukuwa na la maana sana kuongea na Wananchi?
  Sasahivi tunazo NYERERE DAY,SOKOINE DAY,INDEPENDENCE DAY,REVOLUTIONARY DAY,UNION DAY PLUS SIKUKUU ZA KIDINI.JE TUNAHITAJI TENA KAWAWA DAY?
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kwani rais bado ana utaratibu huo wa kutuhubia mwisho wa mwezi? (seriously sikumbuki last time nimemsikia)

  kwani vigezo gani na sifa gani zilitumika kuteua siku za kuwakumbuka hao? If he fits in why not??? (ameshika nyadhifa muhimu serikalini na amefanya mengi sana ya kukumbukwa)
   
 3. n

  nzala Member

  #3
  Jan 1, 2010
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ilibidi ahutubie taifa, na kueleza mipango yake kwa mwaka huu wa 2010. rais wetu hii is serious at.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Atatumia kifo cha Kawawa kama scapegoat!
  Hana jambo jipya la kuwaambia wananchi so far, wala hakuna dira ya mwaka huu, zaidi ya uchaguzi na matisheti ya "chagua Kikwete"!
  Hakuna ishu yoyote ya kitaifa iliyofanikiwa, sanasana ni matatizo yamezidi.
  Mabalaa ya maajali, vifo na shida za umeme zenji yote ni mizimu inayomla, atalieleza nini taifa?
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  kaka chuki ni mbaya kuliko cancer maana kwako inakuwa kila kitu kina rangi moja [ile uitakayo] ikiwa si hivyo basi inakuwa nongwa. Ukiendeleza chuki utakatishwa tamaa na uwezekano wa kufa upesi kutokana depression utakuwa mkubwa sana. Idumu tanzania
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu waislam napenda kuwahuswia pamoja na kuihuswia Nafsi yangu katika kumcha Allah na kufata maamrisho yake na kucha yale aliyokataza.

  Nikirejea katika Quran imeweka wazi kabisa kuwa sisi ni Umma Bora sana na sababu za sisi kuwa Umma bora ni tatu tu. 1. Tunaamrishana mambo mema 2. Tunakatazana mambo mabaya 3. Tunamuamini na kumtwii Allah Subuhanau wataala.

  nawahuswia Muweke Husia.

  Ni lazima mjue mambo muhimu kwa maiti wa kiislam. Mola amesema bayana Mtu anapofariki tu tunatakiwa haraka sana kumzika.

  Kumbukeni Shart za maiti wa kiislam ni
  1. Kumfunika (kumsitiri) pale anapofariki tu
  2. Kuoshwa
  3. Kuvikwa Sanda.
  4. Kulipa madeni yake na kupokea zile anazodai ( kuwakabidhi wadeni/ wadaiwa kwa mtu maalum katika familia)
  5. Kumswalia.
  6. Kuzika.


  hakuna kipengele katika Dini kinachosema kuwa kuna issue ya Kuaga maiti. Huo ni UKRISTO MTUPU na tutaangamia kwa mambo haya ya kuiga ukristo.

  hakuna mambo ya kuchanganyika wanaume na wanawake katika misiba hususan kuaga au hata kwenda kuzika.

  Mungu atunusuru sana na mambo haya ya kinaswala.

  nawahusia muweke Usia msije fanyiwa mambo kinyume.

  Dr Hamza Yousuf Al nammani
  Doha
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  maneno yako sawia kabisa.

  hayo ndio yanayojiri kwenye msiba wa Rashid kawawa. Leo amepelekwa Karimjee hall ili watu wauage mwili wake. Cha kushangaza sura haijafunuliwa.

  Na mufti wa Bakwata na Shehe wa Bakwata wa mkoa wapo pale kutoa dua. Kuna mchanganyiko mkubwa sana wa wanawake na wanaume na ushabiki wa vyama umepamba mote.

  Wallahi utafikiri ni pahala pa mipasho.

  Eeh Allah mlaze mzee wetu pahala panapo stahiki
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Marehemu Rashid Mfaume Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa letu na kati ya wazalendo kwelikweli wachache ambao taifa letu limebahatika kuwapata.

  Duku duku langu ni moja; mbona sijamsikia hata siku moja katika miaka hii michache ya mwisho ya uhai wake kukemea vitendo viovu vya viongozi wetu vya kujilimbikizia mali na ufisadi?

  Nini kilimfanya asite kukemea maovu haya??
   
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  sina chuki na kawawa wala rais.nimehoji ni kwanini rais hajahutubia taifa japo hata kwa salamu za mwaka mpya kama ameshindwa kutimiza kwa mara nyingine ahadi yake ya kuongea na wananchi kila mwezi.pia nimedokeza kuhusu kuanzishwa kwa kawawa day,je kuna umuhimu wowote?kumbuka nyerere day ilianzishwa kumkumbu na kuenzi fikra zake,lakini sasahivi wameziunganisha na shughuli ya kuzima mwenge.hii sio kwamba maandalizi yake yanagharimu sana bali maana halisi ya kumuenzi inapotea kwani kinachoongelewa ni mwenge na miradi iliyozinduliwa nao na wakati mwingine miradi hiyo haina mwelekeo wa kitaifa bali kichama.
   
 10. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ...kaka hapo hamna UKRISTO WALA UISLAMU BALI NI UTARATIBU WA KISERIKALI KTK KUWAPUMZISHA WALIOTANGULIA MBELE ya haki.Kawawa hakufanya kazi ya waislam pekee bali aliwatumikia WATANZANIA WOTE.
  Hata kama angeacha wosia bado serikali ingeuangali vyema kwa kuzingatia serikali haina dini.
  Kuna afisa mmoja wa JWTZ alikuwa ameacha wosia kwamba,akifa mwili wake ukaushwe na utumike kama kifaa cha kufundishia(teaching aid) kwa sababu yeye ndio muanzilishi wa viwanja vya mazoezi ya viungo jeshini.wosia ulipelekwa makao makuu ya jeshi na ikulu,sehemu zote walimkubalia kwamba itakuwa hivyo lakini alipofariki mwaka jana hakuna kilichofanyika kwani sio utaratibu wa serikali.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kama umeisoma Vizuri katiba ya Tanzania, imeweka wazi kuwa Serikali haina Dini ila watu wake wana dini zao.

  Suala la maziko ni suala binafsi la kifamilia. Mara nyingi Familia ndio inayotoa mwongozo kwa Serikali nini kifanyike lakini Serikali inawajibika kugharamia gharama za maziko yoye.

  Ndi maana unapotokea msiba wa kiongozi wa Kitaifa, mara myingi kiongozi mzuri wa nchi anawaarifu wananchi kuhusu msiba huo na mwisho lazima atasema Taratibu za maziko tutazipata toka kwa wanafamilia. na Serikali itagharamia maziko yote.

  Sasa famili inapopanga basi serikali inaangalia namna ya kushirikiana nao.

  Sasa katika Uislam hakuna kipengele cha kuithalilisha maiti kwa kuiweka pahala eti watu waiage. Huo ni utamaduni wa Kikristo na wakristo huwa wanaifunua maiti ile ili kila mtu aione na kuiaga.

  Haj Hafif ameshangaa Mzee kawawa hajafunuliwa hiyo ni kwa sababu si utamaduni wetu.

  Wosia siku zote ni lazima ufatwe lakini unachokiandika ni lazima kisivunje sheria za nchi,

  Huyo Mwanajeshi angeweza kusema maiti yake anataka ichomwe na majivu yake yamwage labda baharini ingefanyika. lakini kutaka ikaushwe na kuwekwa maabara ya serikali hiyo ni kinyume cha sheria.

  ndugu yangu Wosia ni muhimu sana na kama hujui kuandika muone mwanasheria akusaidie kuandika for your own good
   
 12. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Waislamu tunaamini kuwa Mayahudi ni Makafir, je wewe unaamini hivyo?
   
Loading...