Siku Mikutano Ya Siasa ikiruhusiwa!

mululu

JF-Expert Member
Nov 7, 2014
749
406
Siku jeshi la polisi likija kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa NATABIRI watanzania tunaenda kushuhudia MAFURIKO ambayo ni zaidi hata ya yale ya mwaka jana ya kuzungusha mikono ya MABADILIKO.

Kwanini? kwa niwajuavyo wabongo wanapenda sana kuona kile kilichokuwa KIKIKATAZWA, pia wanasiasa wa upinzani watakuwa wamejikoki kutoa hotuba za kuvutia na zenye mashiko kwa maslahi mapana ya taifa, kwanini? kwa sababu hii kamatakamata imewaboresha munoo....

Je, wanzangu munahisi itakuwaje?
 
Siyo watanzania tu, mtu yeyote angependa kujua hicho kilichokuwa kimezuiliwa, na sababu hasa ya kuzuiwa. Yaani kuzuiwa na kuruhusiwa itakuwa kick kwa waliokuwa wamezuiliwa.

Mbaya zaidi( kwa Wengine Nzuri zaidi) vyama vya upinzani vitaaminiwa hata vikisema uongo. Watu watasema "Kumbe ndiyomaana walizuiliwa ili tusiyajue hay!"

Na kwa namna hiyo amani inaweza kutoweka, kwa msingi wa uchochezi. Hivyo basi hakuna haja ya kuruhusu mikutano hii kwa haraka. Inapaswa kuwe na majadiliano na makubaliano juu ya uendeshwaji wa mikutano hii ili kutohatarisha amani.
 
Kimya :) :) Watu wamefungwa kimawazo na kimatendo. Ni fikra za mwenyekiti wetu wa chama ndizo zimetawala. Zidumu :) :)
 
Hahahahahaha Hahahhahahaaa Hahahaahhaha no that day... I say I will be there!
 
unaowataja hawajakataza mikutano na wala hawama iyo power kwa kuwa mikutano ipo ki katiba na kwenye sheria ya vyama vya siasa bali hao unao wataja wanatekeleza maagizo toka juu(mbinguni from gods)
 
Back
Top Bottom