Niliwahi kuandika humu jamvini kuwa, kuzuia mikutano ya hadhara kutainufaisha zaidi kambi ya upinzani kuliko chama tawala.
Leo ni CCM pekee inayozunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara, wapinzani wamezuiwa, wananchi wanawasikia na kuwazoea pengine kuwachoka, sasa wana hamu ya kusikia upande wa pili.
Kujua mikakati ya upinzani ni silaha, utajuaje nguvu ya mpinzani wako kama umezuia mikutano ya hadhara, utajuaje unakubalika kwa kuangalia upande wako tu.
Pamoja na mikutano ya hadhara kuzuiwa vyama vya upinzani havikubweteka, tumeona jinsi vyama vya Chadema na ACT wazalendo vilivyokuwa vikifanya makongamano, mikutano na waandishi wa habari, semina mbalimbali za ndani kwa viongozi na wanachama wake.
Akili zimenolewa zimepumzika vya kutosha tayari kwa mapambano siku mikutano itakapoanza, wenzao kina Polepole akili zitakuwa zimechoka maneno yameisha wataanza kurudia yale yale.
CCM na mgombea wa CCM watambue kuwa kuna takriban watu milioni 8 waliojiandikisha kupiga kura 2015 hawakupiga kura, vile vile itambue kuna kundi kubwa na vijana waliofikisha umri wa kupiga kura ambao 2015 walikuwa na miaka 13,14,15,16 na 17 wako tayari kupiga kura. Hawa wanatakiwa kufikiwa.
Haya makundi yanaweza kuwa na wapiga kura wengi zaidi ya waliopiga kura 2015, wengi wao ni vijana wenye uelewa, kama umezuia mikutano ya hadhara lini utawafikia, kipindi cha kampeni hakitoshi kuwafikia vijana wote na huwa kimetawaliwa na mihemko zaidi ya uhalisia. Kushindwa kufanya hivyo, matokeo yake ni CCM kubaki na kundi la wazee waliozaliwa miaka ya 60, 70 inaowategemea kundi ambalo linazidi kupungua siku hadi siku.
Kwa kuzuia mikutano Chama cha Mapinduzi kimekosa fursa muhimu ya kuijua nguvu ya upinzani, kumjua mgombea wa upinzani siyo kwa jina bali nguvu iliyo nyuma yake. Ni mahesabu haya ndiyo yananifanya niseme, kwenye uchaguzi ujao upinzani utanufaika zaidi na zuio la mikutano ukilinganisha na chama tawala.