Siku mganga maarufu alipowaumbua maafisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku mganga maarufu alipowaumbua maafisa

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by vukani, Mar 18, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yule Mganga wa ndumba maarufu kwa kunywa damu ya Paka, ili kuimarisha ndumba zake al maarufu kama Manyaunyau aliwaumbua maafisa wa chama cha kutetea ukatili kwa wanyama pale walipofanya ziara ya ghafla huko ofisini kwakwe maeneo ya Tabata.

  Inasemekana maafisa hao ambao walifika ofisini kwa mganga huyo wakiwa na gari dogo waliomba kuzungumza na mganga huyo faragha.

  Huku akijua kuwa wale walikuwa ni wateja ambao walikuwa wakihitaji tiba, aliwaomba wateja waliokuwepo pale ofisini kwake ili awasikilize maafisa hao.

  Msimulizi wa habari hii alibainisha kuwa mara baada ya kutoka faragha, wale maafisa walimuonesha vitambulisho vyao na kujitambulisha kwake. Mganga huyo aliwauliza sababu ya wao kumtembelea pale ofisini kwake na ndipo walipomuuliza kuwa kwa nini anafanya ukatili wa kuchinja Paka na kunywa Damu yake hadharani? Walimweleza kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za chama hicho, huo unahesabiwa kama ukatili kwa wanyama kitu ambacho wao wanalo jukumu kubwa la kulikemea.

  Maafisa hao walimwambia mganga huyo aache mchezo huo mara moja kwa kuwa ni ukatili kwa wanyama ambao hawawezi kuuvumilia.

  Akionekana mtulivu Mganga huyo aliwauliza maafisa hao, “Hivi hayo mabucha yote yaliyoenea hapa nchini ambapo mifugo kama Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na nini sijui wanaochinjwa na kugeuzwa vitoweo kila uchao hamuoni isipokuwa hawa paka wachache ninaowachinja?

  “Sikilizeni kama mnataka niache kuchinja Paka Basi kuanzia leo tangazeni kuwa ni marufuku watu kula nyama ya aina yoyote kwa kuwa huo nao ni ukatili kwa wanyama pia”

  Maafisaa hao waliposikia hivyo waliinamisha vichwa vyao chini, kisha wakaaga na kuondoka bila kusema lolote.

  Msimuliaji aliyekuwepo kwenye eneo la tukio alibainisha kuwa mganga huyo alirudi ndani na kuendelea na tiba zake ambapo siku hiyo alichinja paka wawili ili kufanikisha shughuli zake za tiba…………
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Are you a great thinker??
   
Loading...