Siku Mbunge Ally Kessy alipoambiwa kama anataka usultani, arudi kwao Yemen!

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
4,327
6,390
Wakuu, amani kwenu

Toka iingie awamu ya tano madarakani, tumekuwa tukiukosa uhondo wa vimbwanga kutoka Bungeni, kutokana na kutokuonyeshwa kwa Bunge mubashara.

Tumekuwa tukibahatisha kuona baadhi ya matukio, kwa vipande vipande vya clip vinavyokuwa vinarushwa kwenye mitandao ya kijamii, kama humu JF nk.

Naenda kwenye kusudio la bandiko langu -
Mbunge wa Konde huko visiwani Bw Khatib, hivi karibuni kabla ya Bunge kuvunjwa akitoa mchango wake, alimsifia Rais Magufuli kwa kusema ataheshimu Katiba kwa kukaa uongozini kwa matakwa ya Katba. Na kuwaponda wanaotaka Katiba ibadilishwe ili aongoze vipindi zaidi ya viwili vilivyopo.

Akajitokeza Mbunge Ally Kessy na taarifa, (tukumbuke kuwa huyu, ndiye aliyelishikilia bango hilo wazo) kuwa, Lipumba, Maalim Seif, Mbowe, kukaa kwao uongozini kwa muda mrefu, wanaifuata katiba?

Jamaa akamjibu kuwa, Katiba ya Nchi, si sawa na Katiba ya vyama. Zaidi, akamwambia, hii si nchi ya Kisultani. Kama anataka usultani, basi wazo hilo, alipeleke huukooooo kwao Yemen.

Kilichofuata… sikiliza mwenyewe!

 
Tanzania ni nchi wajinga sana,yani sijui tumelishana nini kuhusu usultani utafikiri usultani ni uhalifu, wakati nchi kubwa kubwa duniani zenye maendeleo kama U.K, Saudia Arabia, Brunei, U. A.E, Spain, Oman, zina tawala za kisultani.
 
Tanzania ni nchi wajinga sana,yani sijui tumelishana nini kuhusu usultani utafikiri usultani ni uhalifu, wakati nchi kubwa kubwa duniani zenye maendeleo kama U.K, Saudia Arabia, Brunei, U. A.E, Spain, Oman, zina tawala za kisultani.
Watu wamekariri waliyofundishwa darasani tu.Fikra zetu bado zimeshikiliwa na wazungu tuna utumwa wa fikra.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom