Siku mbili baada ya kukutana na mwana wa Malkia wa Uiengereza Rais Kikwete apata ujio toka Songas!

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Kwenye michuzi blog kuna picha zinazoonesha wakurugenzi wa Songas wakionana na Rais Ikulu. Songas ni wawekezeji toka Uiengereza na hivi karibuni walionesha 'unyonyaji wao' pale walipoandika kutokufurahishwa na hatua ya serikali ya Tanzania kujenga bomba lenye uwezo mkubwa wa kusafirisha gesi toka Mtwara. Bomba hili kubwa linajengwa kwa makubaliano ya kibiashara kati ya Tanzania na China lakini hawa Songas kwa kuhofia 'competition' walijaribu sana kukatisha watu tamaa. Hawataki ushindani, wanataka wawe na monopoly!

Kwa wale waliokuwa wanafikiri kuwa ujio wa mwana wa mfalme ni kwa sababu ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wafikirie tena. Sherehe za uhuru ni mwanya mzuri wa kuchomeka mambo, na kwa sasa kuna 'scramble for Tanzanian resources' kubwa to kwa mataifa ya magharibi. Hawa mabwana wa Songas wameonana na Pinda wiki hiyo (nadhani ilikuwa juzi) sasa leo wanakutana na Rais! kulikoni? Ni kitu gani cha muhimu hivyo kinacholazimu wakuregenzi hawa waonane na viongozi wakuu wa nchi within days?

Wiki nzima watanzania wamekuwa wanajadili ushoga lakini kumbe wenzetu wako busy 'wanasalimiana'!
 
Lets see how strong our presidaa is kwenye mambo ya tija au kufurahisha malkia, I am hopeful kwamba atawapiga songas chini
 
Back
Top Bottom