RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,423
- 7,124
Siku hizi kumezuka tabia ya wafuasi wa kiongozi mtarajiwa wa malaika kuwatuhumu watu wanao mkosoa kiongozi huyo ya kwamba wanatumwa na mabeberu kumhujumu.
Mimi huwa ninacheka sana kuona mfuasi wa kiongozi huyo wa malaika anasema kwa kujiamini eti mabeberu hawaitakii mema nchi yetu. Hivi ngoja niwaulize nyinyi wafuasi wa kiongozi wa malaika mtarajiwa.
Hivi siku mabeberu wakiamuwa kumhujumu kweli kama mnavyodai, kiongozi huyo atakuwa na ubavu kweli wa kukabiliana na hujuma hizo?
Hivi siku mabeberu wakiamua kuiadhibu nchi yetu tutakuwa na ubavu wa kukabiliana nao? Au mnashinda humu mnaongea ili kujifurahisha?
Ngoja sasa niwaambie, nguvu ya mabeberu ni kubwa mno na hatuna uwezo wa kukabiliana nao hata kidogo. Mabeberu wakiamua wana uwezo wa kuigeuza pesa yetu kuwa makaratasi yasiyo kuwa na thamani, yaani unaweza kuwa na milioni mia ndani lakini hiyo hela haina uwezo hata wakununulia mkate watoto wako wale.
Wana uwezo wa kuwafanya muishi gizani na msisafiri kwa kuzuia mafuta kuingia nchini. Wana uwezo wa kuzuia dawa za mahosipitalini mkafa kama wadudu. Yaani wanauwezo wa kuyafanya maisha ya baadhi ya mataifa kuwa magumu na yasiyovumilika.
Kwa hiyo, muachage kushabikia mambo msioyajua ili kumfurahisha kiongozi wa malaika, hao mnao sema ni maadui zenu siku wakiamua kuwa maadui zenu ndiyo mtajua dunia ina wenyewe na hao mnaowaabudu na kuwasifu hata wakifanya maovu ni takataka.