Siku kama ya leo April Fool ilivyonifanya nizembee uhai wa mtu muhimu kwangu

relato

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
689
986
Ni miaka kadhaa imepita lakini Jamani siku kama ya Leo sitaisahau,nilikuwa nipo hostel mwaka wangu wa mwisho wa masomo chuo fulani hapa dar,nilikuwa najiandaa kwenda darasani,nakumbuka nilipigiwa simu na rafiki wa mpenzi wangu akaniambia babe wangu yupo eneo la lakini kazimia amepoteza fahamu nikacheka saana nikakata simu.

Baadae Dada ake akanipigia akaniambia umesikia doctor anaumwa nkamwambia Leo siku ya wajinga WiFi,akagutuka akasonya akasema pumbavu zao,akakata simu.

Nikaingia zangu darasani. Baadae mdogo wake akanipigia ambae anasoma maeneo ya muhimbili hapohapo akaniambia hivyo hivyo jamaa anaumwa nikamwambia Leo siku ya wajinga buana.

Akasema yaani nilishafka Hadi nje hapa ya jengo la emergence,ngoja nirudi alionekana kumind kiasi Fulani,sasa ile anageuka pale emergence wanataratibu za kutangaza majina ya wagonjwa kwa ajili ya ndugu zake waingie ndani. Si ndio akasikia ndugu wa doctor Fulani Fulani.

Akasema wameniona nipo hapa ndio wananiita. Akasepa,lakini akafika sehemu kabla hajatoka eneo la muhimbili akakutana na mfanyakazi mwenzie wa department moja akauliza ndio unatoka kumchek kaka yako anaendeleaje?

Akauliza vizuri,ndio akastuka kumbe kweli,ikabidi anitext Shem ni kweli anaumwa yuko emergence ndio naenda kumuona. Nikamuulza umejuaje?Una uhakika hauchezewi akili? Akaniambia Fulani kaniuliza hivi. Duh!!nilipagawa halafu nikachukia ujinga wa hii siku.

Ikanibidi nitoke darasani nianze safari to Muhimbili yaani namkuta unconscious kweli..duh!!nikijikuta nalia tu,nikafeel guilty kwa kuwaambia watu cha lipuuzi April fool wakati mtu yupo serious sick.

Kama dakika kumi nimesimama pale pale pembeni ya kitanda machozi yananitoka,nikaona mtu ananishika mkono Ndio akawa anarudiwa na fahamu ananiuliza mbona unalia.

Ikabidi nitoke niwapigie ndugu zake wengne niwape taarifa. Sitaisahau hii siku na ujinga wake,ambao watu tunaweza kufanya jambo lenye madhara makubwa kwa ajili ya hii siku.
 
Pole sana.

Siku hii ya wajinga ni kwaajili wajinga kujitungia na kusema uongo huwa simuelewi mtu anayedanganya kisa siku hii. kati ya siku ambazo habari huwa ni nyingi ni siku ya leo ndipo wajinga wakiadhimisha siku/sikukuu yao.

Inakuwaje siku zote unajizuia kusema uongo halafu uje useme leo huoni kama ndio ujinga wenyewe?

Maadhimisho mema ya sikukuu ya wajinga.
 
Ha ha ha haaa.. Pole sana Mkuu.

Mimi nimewahi kuchomwa jua sehemu sitokaa nisahau.

Ilikua hivi; Ilikua jumamosi kama leo yaani, Nilikua nasoma day(Azania secondary) hapo, halafu rafiki yangu toka enzi za utoto alikua anasoma st. Anne Marie Mbezi kwa Msuguli ila alikua anaishi Boarding.

So mara nyingi tulikua tukikutana tunapiga story sana sometimes mpaka midnight, kipindi cha likizo na visiting day kilikua kipindi kizuri sana kwetu, tulikua hatukumbuki hata kula just stories za hapa na pale coz hata primary tulisoma wote Mbuyuni Primary pale.

Sasa ilikua ikijitokeza chance ya kuonana bila kutarajia ilikua ni kipindi cha msisimko sana, Basi bwana siku yenyewe palivyokucha tu, akanipigia simu, "Oya nimekuja home(mikocheni) fasta kuchukua pocket money, Kama vipi sogea hapo drive-inn- zantel nitakupitia hapo coz bro atanirudisha na gari so tutaenda wote halafu utarudi nae", Dah nilifurahi sana nikajicock fasta nikatoka, nikaenda stendi pale "Dry" bwana kumsubiri, kila saa namcheck ananiambia tunatoka muda sio mrefu subiri.

Nilikaa pale mpaka saa 4 na dk 20 hivi nikaona simu inaita,kupokea ananiambia " Happy Fool Day" , Nilichukia sana, nikakata simu.

Since then sijawahi kuipenda hiyo siku.. Hata nikimkumbushaga yeye anachekaga sana. Halafu na yeye yuko humu humu JF.
 
Katika siku ambazo naona mods wanapata shida kukimbizana na "threads mfu" ni leo. Yani mpaka nawaonea huruma lakini nabanwa na kicheko pia. Kuna threads kama 3 wametembeanazo kama hawana akili timamu. Kila nilipokuwa nataka kuifungua nakuta Hola.
 
Yaani duh!!sijui imekuaje hii siku kwa kweli..sasa inasababisha watu potezea mambo ya msingi tukijua kufanywa wajinga
 
Mi siipendagi hii siku kwa sababu nilibebeshwa matofali shule wakisema adhabu katoa second master kumbe sio kweli,since then sitakigi kufanywa mjinga hii siku.
 
huruma kweli
 
Mi siipendagi hii siku kwa sababu nilibebeshwa matofali shule wakisema adhabu katoa second master kumbe sio kweli,since then sitakigi kufanywa mjinga hii siku.
Ha ha ha ha haaaa.. Hiyo ya tofali noma zaidi.. Khaaaa... Kuna watu hawana huruma kabisa.
 
Yaani duh!!sijui imekuaje hii siku kwa kweli..sasa inasababisha watu potezea mambo ya msingi tukijua kufanywa wajinga
Siku wala haina tatizo, tatizo ni jinsi watu wanavyoipa usiriaz...kiasi kwamba watu walijiandaa na kuisubiri kwa hamu siku hii
 
Ha ha ha haaa, tena wewe unaonekana mwepesi sana, issue ni kwamba inapotokea inakua sio rahisi wewe kugundua. Yaani anaekufanyia hivyo ni mtu ambaye mnajuana vizuri sana, so anajua ili akupate kirahisi akuanzie wapi.
mkuu me hata familia yangu wanajua mpole sana na wanatabiaya kunionea huruma na hawapendi ni kwazike hata kidogo.. sababu siongei.. marafiki hawanielewagi wengi huwa wapo na mi kimachale ha hahaha
 
Pole. Ndiyo matatizo ya kuiga tamaduni za watu (wazungu) bila kujua maana halisi, na sisi (ngozi nyeusi) tukiiga kitu tunaiga kikweli kweli kuwazidi hata wenyewe.
 
Back
Top Bottom