Siku kama ya leo 26/5/ miaka 131 iliyopita Ufaransa ilianza kuikoloni nchi ya Tunisia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku kama ya leo 26/5/ miaka 131 iliyopita Ufaransa ilianza kuikoloni nchi ya Tunisia.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, May 26, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Leo ni Jumamosi tarehe 4 Rajab mwaka 1433 Hijria, inayosadifiana na terehe 26 Mei mwaka 2012 Miladia.
  Siku kama ya leo miaka 131 iliyopita Ufaransa ilianza kuikoloni nchi ya Tunisia. Kabla ya hapo Wafaransa walikuwa wamejiingiza nchini humo kupitia shughuli za kiuchumi na kibiashara.

  Kwa miaka kadhaa Tunisia iliendelea kuungwa mkono na Ufaransa. Hata hivyo katika kipindi cha muongo wa 1930 Miladia, zilianza harakati za kudai uhuru zilizoongozwa na Habib Bourguiba na mwaka 1957 Miladia utawala wa kifalme uliokuwa ukiongoza Tunisia uling’olewa na Habib Bourguiba akawa rais wa nchini hiyo.


  Bourguiba aliiongoza nchi hiyo kwa udikteta na mabavu hadi kufikia mwaka 1987, ambapo aling’olewa madarakani na Zainul Abidin Ben Ali aliyekuwa mkuu wa polisi kipindi hicho. Hata hivyo baada ya Ben Ali kutwaa madaraka aliendeleza siasa zilezile za udikteta wa Bourguiba katika kuiongoza Tunisia hali iliyowapelekea wananchi wa nchi hiyo kushindwa kuvumilia na mwezi Juni 2011 naye akang’olewa madarakani na wananchi hao, ambapo alikimbilia Saudi Arabia.


  Miaka 841 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, alifariki dunia malenga wa Kiislamu Muhammad ibn ‘Ali al-Wasiti maarufu kwa jina la Ibn Muallim. Alizaliwa mwaka 501 Hijiria. Mashairi ya malenga huyo yalibeba ujumbe wa maadili na tabia njema na masuala mengine yahusuyo jamii huku mengine yakihusiana na maudhui za irfani.

  Athari pekee ya Ibn Muallim ni kitabu cha tungo za mashairi ya malenga huyo.
  Na siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 mtafiti, mwandishi na mwanasaikolojia dakta Ali Akbar Siasi.


  Alizaliwa mjini Tehran mwaka 1273 Hijiria Shamsia na baada ya kumaliza masomo yake aliekea Ufaransa. Baada ya Ali Akbar Siasi kupata shahada ya udakta katika chuo kikuu cha mjini Paris alirejea nchini Iran. Alipata kuwa Waziri wa Utamaduni na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tehran.


  Miongoni mwa athari za msomi huyo ni pamoja na kitabu kiitwacho “Ilmun Nafsi, au Ravan Shenasi Jadid”, “Ravan Shenasi Parvareshi”, “Mabani Falsafeh”, “Ilmu Akhlaq” na “Mantik Ravan Shenasi.”


  Yericko Nyerere:

  Tembelea Yericko Nyerere
   
Loading...