Siku ikifika....

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Pamoja na upole wa mtz alionao, je, nini kitatokea iwapo watz tutaweka upole pembeni? Ikulu kweli kutakalika na huyo Mkwere mwizi wa kura ataufurahia ushindi wake?
 
Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA
Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pm



Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.




Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook


NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi


Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search


Zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.


Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.


Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principles



Tukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.


Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.


Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

http://georgiandaily.com/index.php?o...2829&Itemid=68
 
jamani mimi nakumbuka kusoma barua moja iliyoandikwa na mtanzania mmoja kwa rais ikiwa na kichwa cha habari " SIKU YETU YA KENYA ITAKAPOFIKA..." Sikumbuki maneno yote lakini alikuwa akimuasa rais kuwa Tanzania inakaribia Namanga njiani kwenda Kenya kwa hiyo tafakari nini kitatokea siku hiyo .. kama yupo mweny nakala atusaidie

Sungurampole
 
Pamoja na upole wa mtz alionao, je, nini kitatokea iwapo watz tutaweka upole pembeni? Ikulu kweli kutakalika na huyo Mkwere mwizi wa kura ataufurahia ushindi wake?

Unazungumza kuhusu tz? Siyo vizazi vilivyopo tz sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom