"Siku hizi uko wapi?" ni swali linalonikera. Chini ya Rais Samia, huenda nikapata jibu lake

Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo miaka 3 iliyopita, nilibahatika kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye taasisi moja.

Wakati wa hayo mafunzo nilizoeana vyema na watumishi wa pale hasa wale wa kwenye Idara niliyokuwamo. Ukaribu, maelewano, ushirikiano katika kazi ulikuwa ni wa kushibana, ulikuwa kama familia.

Baada ya muda wangu wa mafunzo kwa vitendo kukamilika niliondoka kuingia mtaani, kusaka ajira. Kama tulivyokuwa tunajua utawala wa awamu ya 5 na ajira ulivyo, nilibatizwa kwa moto mtaani. Nilikiona cha mtema kuni.

Kuna siku nilipata wasaa wa kuitembelea hiyo taasisi niliyofanyia mafunzo, nilifika hadi kuwajulia hali wana Idara kwenye Idara niliyokuwemo kipindi cha mafunzo. Ilikuwa ni furaha kwangu na kwao kuonana tena baada ya kuachana kwa muda mrefu.

Katika kupiga stori mimi nikiwa nawauliza jinsi wanavyoendelea na kazi, swali lao kwangu ambalo kila mmoja wao anashauku ya kutaka kujua jibu ni "Siku hizi uko wapi?'' Hapa wakiwa wanamaanisha nafanya kazi wapi baada ya kumaliza mafunzo, kwa kuwa sina kazi naendelea kupambana huwa nakereheka sana nikiulizwa hizi swali. Naishia kuwajibu nipo tu mtaani, ila hawaamini wanadhani huenda nina kazi/kuajiriwa sehemu ambapo wanapenda kuifahamu.

Hongera Mama katika awamu yako ya Sita, bila shaka nitaweza kupata jibu la swali langu hili linalonikosesha amani. Kikubwa naomba Mungu haki itendeke huko kwenye mamlaka husika maana figisu huwa hazikosekani
mkuu nikajua niko pekee yangu kumbe niko na wewe yani mtu ukimjibu nipo tu haamini anajua kuna sehem flani nzuri kumbe wapi sijui kwanini hawaamini
 
mkuu nikajua niko pekee yangu kumbe niko na wewe yani mtu ukimjibu nipo tu haamini anajua kuna sehem flani nzuri kumbe wapi sijui kwanini hawaamini

Ramani bado haisomeki na hili swali bado linaendelea kushamiri, vipi kwa upande wako mkuu
 
Pambana mkuu waje kukukuta juu,sa hivi wakigundua una Mishe inakuingizia senti mbili tatu umekwisha KWA vizinga na kutatua kero za watu.

Walioajiriwa wanapata tabu sanaaa,Namuona mke wangu anavyopata tabu na kisent chake kiduchu ambacho hakina mchango saaana nyumbani lakini Familia ikifika tarehe29 kila mtu kaweka order zake,Mi kimyaaa nakusanya vimilioni vyangu tu KWA mwezi,si nimeachana na kazi za watu banaaa.So sina kazi
Hongera sana mkuu kwa hatua nzuri uliyofikia
 
mkuu nikajua niko pekee yangu kumbe niko na wewe yani mtu ukimjibu nipo tu haamini anajua kuna sehem flani nzuri kumbe wapi sijui kwanini hawaamini
Kule kwetu nikumuambia Niko dsm au ddm wanajuwa nineshatoka nikula maisha sas huwa Mara nyingi nawapiga sound kuwa Niko singida ili Hali Niko jiji dsm au nawambia Niko ddm kwa kak angu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom