"Siku hizi uko wapi?" ni swali linalonikera. Chini ya Rais Samia, huenda nikapata jibu lake

Natafuta matibabu

JF-Expert Member
Aug 1, 2020
234
250
Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo miaka 3 iliyopita, nilibahatika kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye taasisi moja.

Wakati wa hayo mafunzo nilizoeana vyema na watumishi wa pale hasa wale wa kwenye Idara niliyokuwamo. Ukaribu, maelewano, ushirikiano katika kazi ulikuwa ni wa kushibana, ulikuwa kama familia.

Baada ya muda wangu wa mafunzo kwa vitendo kukamilika niliondoka kuingia mtaani, kusaka ajira. Kama tulivyokuwa tunajua utawala wa awamu ya 5 na ajira ulivyo, nilibatizwa kwa moto mtaani. Nilikiona cha mtema kuni.

Kuna siku nilipata wasaa wa kuitembelea hiyo taasisi niliyofanyia mafunzo, nilifika hadi kuwajulia hali wana Idara kwenye Idara niliyokuwemo kipindi cha mafunzo. Ilikuwa ni furaha kwangu na kwao kuonana tena baada ya kuachana kwa muda mrefu.

Katika kupiga stori mimi nikiwa nawauliza jinsi wanavyoendelea na kazi, swali lao kwangu ambalo kila mmoja wao anashauku ya kutaka kujua jibu ni "Siku hizi uko wapi?'' Hapa wakiwa wanamaanisha nafanya kazi wapi baada ya kumaliza mafunzo, kwa kuwa sina kazi naendelea kupambana huwa nakereheka sana nikiulizwa hizi swali. Naishia kuwajibu nipo tu mtaani, ila hawaamini wanadhani huenda nina kazi/kuajiriwa sehemu ambapo wanapenda kuifahamu.

Hongera Mama katika awamu yako ya Sita, bila shaka nitaweza kupata jibu la swali langu hili linalonikosesha amani. Kikubwa naomba Mungu haki itendeke huko kwenye mamlaka husika maana figisu huwa hazikosekani
 

Natafuta matibabu

JF-Expert Member
Aug 1, 2020
234
250
Jaribu kulima kiukweli, unaweza kuibukia huko! Mambo nako kumenoka hasa kilimo cha maparachichi, mbegu hass.
Mimi kwa asili ni mkulima, sitaki kurudi huko kichwa kichwa, nikitaka kurudi nitarudi kwenda kulima kilimo chenye ubora kuliko cha mwanzo.

Sasa inanibidi nitengeneze mazingira ya kuendea hicho kilimo chenye ubora.
 

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Apr 16, 2018
1,501
2,000
Mimi kwa asili ni mkulima, sitaki kurudi huko kichwa kichwa, nikitaka kurudi nitarudi kwenda kulima kilimo chenye ubora kuliko cha mwanzo.

Sasa inanibidi nitengeneze mazingira ya kuendea hicho kilimo chenye ubora
Sawa mkuu, jaribu kilimo hicho cha maparachichi(hass), Kama upo mikoa ya Arusha, Ruvuma, Njombe, Mbeya nk, Wakati unafuatilia ajira uwe bize na kilimo hicho. Hata kama utapata kazi bado utakuwa hujapoteza chochote. Bali ni faida tupu kwako na kwa familia yako mbeleni.
 

dora

JF-Expert Member
Jun 5, 2010
365
500
N wasipouliza pia wataonekana kama hawajali. Ni kawaida watu mliokuwa pamoja aidha shuleni or kazini/mafunzoni kutaka kujua baada ya pale ulienda wapi or unafanya nini. Kuwa tu mkweli, kwa case kama yako hapo ilikuwa ni sehemu ulifanyia mafunzo huwezi jua wanaweza kukuungisha ukapata ajira.
 

Natafuta matibabu

JF-Expert Member
Aug 1, 2020
234
250
N wasipouliza pia wataonekana kama hawajali. Ni kawaida watu mliokuwa pamoja aidha shuleni or kazini/mafunzoni kutaka kujua baada ya pale ulienda wapi or unafanya nini. Kuwa tu mkweli, kwa case kama yako hapo ilikuwa ni sehemu ulifanyia mafunzo huwezi jua wanaweza kukuungisha ukapata ajira.
Nina namba za baadhi yao niliwahi kuwaambia wanitafutie connection ila hadi sasa kimya
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,870
2,000
Swali hili sijui lipata jibu lini
Pambana mkuu waje kukukuta juu,sa hivi wakigundua una Mishe inakuingizia senti mbili tatu umekwisha KWA vizinga na kutatua kero za watu.

Walioajiriwa wanapata tabu sanaaa,Namuona mke wangu anavyopata tabu na kisent chake kiduchu ambacho hakina mchango saaana nyumbani lakini Familia ikifika tarehe29 kila mtu kaweka order zake,Mi kimyaaa nakusanya vimilioni vyangu tu KWA mwezi,si nimeachana na kazi za watu banaaa.So sina kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom