Siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,459
6,024
Hii kauli imenishutua, ni kauli kutoka kwa rafiki yangu ninayemfahamu kwa muda mrefu. Ndoa yao ina miaka 5 sasa na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike, kwa haraka haraka unaweza kuiona ndoa yao kama ni ndoa imara na yenye upendo mkubwa na kutamani kujifunza kutoka kwao.

Majuzi nilikutana na huyu rafiki yangu tulikuwa na maongezi ya kikazi, katika maongezi yetu tukawa tumeingiza mambo ya familia, ndipo nilishutushwa na kauli ya rafiki yangu "Siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula"

Nikamuuliza, kwanini? "Tangu apate hii kazi aliyonayo sasa yapata miaka miwili sili chakula kilichopikwa kwa mikono yake angalau mara moja moja, kwa siku chache za mwanzoni alijitahidi lakini haikudumu kwa muda mrefu akaacha kabisa binti wa nyumbani akawa ndiyo muhusika kwa 100%.

Imenichukua muda mrefu kila nimalizapo kula chakula hasa umwambia mke wangu asante kwa chakula, kilikuwa ni kitamu.

Kwa sasa nimegundua kuwa ninachokifanya ni unafiki tu wa kumfurahisha mke wangu, huku nikiwa na manung'uniko moyoni. Kwa sasa nikimaliza kula nasema asante aliyepika chakula, kilikuwa kitamu sana, naona hii kauli imemshutua na kumchanganya kidogo".

Nikamuuliza kwanini anatumia njia hii badala ya kukaa naye wakaliongelea hili tatizo, akasema "Nimekwisha ongea naye mara nyingi ila amekuwa na sababu nyingi mara kuchoka, mara ubize wa kazi, sababu nyingi tu. Natamani angalau mara moja moja nile chakula chakula kilichopikwa kwa mikono ya mke wangu".

Wanawake jitahidi waume zenu wale chakula kilichopikwa kwa mikono yenu angalau mara moja moja.
 
mmmm Balaa mwenyezi mungu atunusuru mimi na wanawake wenzangu,ndoa zinatafrani zake jamani,lakini hata kama unafanya kazi weekend unaweza ukapika na hata siku za kawaida unaweza kumwambia dada akutayarishie wewe ukifika una
changanya kwanza sikuizi sio kama zamani unapika na mikaa Gas unaivisha mara moja,unaweza kubiwa mume kwa vitu vidogo kama hivi halafu unatafuta mchawi..
 
Mwambie jamaa aanze kumshukuru dada mbele ya mkewe, aongeze na kusifia hicho chakula juu, hata kama hakistahili sifa. Missus asiposhtuka na kurekebika, basi tena.

Au aache tu kabisa kula home, kwa condition mpaka uwe mkono wa mama mwenye mji.
 
Mkuu, sikuhizi katika mabinti waliofika vyuo vikuu, ukimpata atakayekupikia chakula, kukuchemshia chai au hata kukuandalia maji ya kuoga ni mmoja kati ya elfu1.

NA UMSHUKURU MUNGU WAKO.

Sikuhizi binti kabla hata ya kuolewa anamwambia mamaye amtafutie binti wa kazi na wazazi wanafanya hivyo.
 
wanangapi tuna kazi na chakula cha usiku lazima tupike ..nikutokujua Tu wajibu wake

ukishajua wajibu Wako na ukau appreciate wala hutaona km ni utumwa kutoka kazin nakuanza kupika
Umeongea kitu cha msingi.
 
Mkeo Ni mvivu wanangapi tuna kazi na chakula cha usiku lazima tupike ..nikutokujua Tu wajibu wake

ukishajua wajibu Wako na ukau appreciate wala hutaona km ni utumwa kutoka kazin nakuanza kupika
Sema mke wa rafiki yako mvivu.... Na rafiki yake mwenyewe ni Mimi sasa..... Kumbe ninakwambia mambo yangu unakuja kunianika huku...
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom