Siku hizi Rais Magufuli amekuwa mpole. Ni bora zaidi akiwa hivi

Nachomkubali Raisi wangu huwa hafanyi kazi kwa Mazoea bali kuendena na wakati na mazingira hivyo porojo kama hizi huwa hazimpi tabu.

Endelea kupiga kazi Mh. Raisi kumbe wanafiki wanakuponda ila moyoni wanakukubali kiaina, na mtanyooka tu.

#Viva Magu 2015-2025
#DG
Kwani aliyemtuma Rais wako mtukufu aanzishe operations ya vyeti feki alifanya kazi kwa mazoea? Wale waliofukuzwa kazi kisa vyeti feki wana tofauti gani na Bashite? au kutofanya kazi kwa mazoea ni kukataa kuona mapungufu ya kipenzi chake Bashite? aendelee kupiga kazi ya nini? Visasi kwa akina Hanspope na wenzao? Apige kazi kujenga kiwanja cha ndege kijijini chato? au apige kazi kununua wapinzani kurudia chaguzi kwa gharama huku pesa za walipa kodi zikiteketea kwa mambo yasiyo na Tija kwa Taifa? Nani atanyooka kwa mapungufu hayo? Utanyooka mwenyewe unayeishi ghetto kwa le mutuz na kukariri zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM mpaka umejitoa fahamu zote.
 
Lakini DC OCD wa Tarime yeye yupo against na magufuli, yeye masikini ndiyo hufanywa chochote na tajiri kwake hulindwa na Polisi na kamati yake ya Ulinzi na usalama ya wilaya na cha ajabu na cha kushangaza Dunia ni hiyo kauli ya magufuli dhidi ya matajiri kufanywa chochote ilitamkwa huko huko Tarime mbele yake na kamati yake lakini yeye na OCD wanekuwa wa kwanza kuitengua na kwenda na Polisi kuwapiga wananchi wachimbaji wadogo wadogo masikini wanyonge wakawapora maki zao pesa kisha kuwabambikia kesi ili pindi wakiwa jela wale matajiri rafiki zake DC na OCD wanatumia fursa hizo kuiba madini yao kisha wanagawana Faida wenyewe, Sio kila RC wala DC anatekeleza maagizo ya magufuli wengine hutumia hizo kauli kama fursa za kuwatisha matajiri kisha kuwapiga pesa yafaa magufuli aunde tume ya kimya kimya kuwachunguza ma RC na DC kwani wengi hulindwa na Takukuru na usalama waliopo nao huko wilayani na mikoani.
Mkuu huyo DC anaonekana kakukwaza sana maana muda sasa ukiingia jf lazima umtupie mawe
 
Back
Top Bottom