Siku hizi mimba ndio kigezo cha kuoana

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,559
Hadi kufikia siku ya jana nimehudhuria harusi 6 ndani ya mwaka huu, kitu kilichonishangaza na kunifanya nije na mada hapa ndani ya hizo 6 nimeshuhudia harusi 5 bibi harusi yuko ndani ya shela na kimimba tena kimimba cha maana sasa sijajua siku hizi ni fasheni kwamba mpaka kitumbo ndo uoe au ndo ile ukimpa mtoto wa watu kibendi basi unalazimishwa kuoa
 
Kuthibitisha uzima wa mitambo ni muhimu Mkuu. Mambo kabla ya kukutana huwa ni mengi sana. Usikute walisha korokochoa na kizazi huko.... wewe uje kupambana tu bila mafanikio. Hapana Aisee. Test Mapema ndio ubebe.
 
Hiyo ni torati kujua kama mwenza wako mayai yapo au kakaangia chips vumbi,wadada wa siku hizi mayai hayana nguvu kwa kumeza madawa,kutoa mimba kwahiyo lazima umjaze kwanza
 
Sababu
1.imani na maadili yetu yanakataza kuzaa nje ya ndo hivyo wengi wanaolewa na mimba zao kukwepa majukumu
2.mwanaume analazimishwa kuoa ili avikwe jukumu lake la kumlea mjamzito na mtoto pindi akizaliwa
 
Back
Top Bottom