Siku hizi mbona hakuna dawa hospitalini tatizo nini?

Mimi Pia nimeshangaa hili swala Kuna zahanati nne niliwahi fika zote hazina dawa, cha kushangaza mpaka panadol hakuna
 
Oooh Kuna daktari nilimuuliza alinijibu kama hivi.....
 
Mkuu kongole kwa huu ufafanuzi, hili swala la dawa kwenye mahospitali ya umma limekuwa ni kitendawili kigumu, wanasiasa wanasema wameongeza bajeti, ukienda saiti unakutana na paracetamol tu!
 
Tatizo la ukosefu wa dawa katika hospital za umma ni la kiufundi sana(very techinical issue). Ni kwamba sera ya wizara au agizo la serikali awamu ya tano ni kwamba wanunue dawa MSD kwa pesa taslimu, ni marufuku MSD kukopesha dawa hata kwenye taasisisi za serikali. Serikali hiyo hiyo haipeleki pesa kwenye taasisi zake kwa wakati na kama inapeleka inakuwa imechelewa sana ili taasisi hizo ziwezo kutumia pesa hizo kununua dawa MSD kwa pesa cash.

Matokeo yake MSD dawa zimejaa, mahospitalini hasa ya serikali dawa hakuna kisa wanakuwa hawajapewa pesa za kununua dawa MSD Kwa hela cash.
Asante ndugu kwa ufafanuzi lakini hebu samahani hivi msd inamilikiwa na nani na ni kwanini hela icheleweshwe kumbe serikali wenyewe wameshaweka no kukopa?
 
Hujui mitishamba mkuu...ulishaambiwa nenda kanywe na usiizarau si kwa ajili ya covid tu hata magonjwa mengine.....Kanywe mwa40..uso utakuparama lakini baada ya siku wiki unarudi kwenye hali ya kawaida..haya ndio maendeleo tuliyonayo sasa hv..
Vipi na kwa tusiojua/tusioelewa tiba za mitishamba?
 
Asante ndugu kwa ufafanuzi lakini hebu samahani hivi msd inamilikiwa na nani na ni kwanini hela icheleweshwe kumbe serikali wenyewe wameshaweka no kukopa?
Hata yule mkurugenzi wa msd aliyeko gerezani sasa hivi alisema tunaidai serikali pesa nyingi(billions) baada ya hapo hakuchukua round akatumbuliwa na kesi juu.
 
Habari wadau...

Kuanzia ishu ya korona ikolee nimefika baadhi ya hospitali na zahanati katika mikoa kadhaa (takribani minne) lakini sijawahi kuona mtu apate palepale hospitalini dawa zote anazoandikiwa (hususani dawa ndogondogo).

Lazima mtu upatiwe dawa moja nyingine unaambiwa ukanunue maana hapo hazijaletwa/zimeisha. Mwanzo niliona kawaida lakini naona sasahivi hali inachanganyia maana mtu anaandikiwa dawa lakini zote yawezekana akalazimika kwenda kununua

Dawa ambazo ni adimu haswahaswa ni Paracetamol, Diclofenac, Amoxicillin, mabomba ya sindano na baadhi ya dawa nyingine nyingi ndogondogo yaani mtu unasema kwajili nina bima nijikakamue nauli tu matokeo yake akiba ya kununua chakula yote inaishia kwenye kununua dawa unarudi njaa inauma dawa zenyewe pengine umepata pungufu ya ulizoandikiwa

Tatizo ni nini mbona hospitalini hakuna dawa?
pole kwa tatizo uliloliona
USHAURI WANGU....
1. Kama una BIMA ya Taifa, ukifika Hospitali wakakuambia hawana baadhi ya dawa; waambie wakujazie fomu ya kuchukua dawa hizo zilizokosekana kwenye duka la dawa lililosajiliwa. Kwa sasa maeneo yote ya mijini na mengi ya vijijini kuna maduka ya dawa yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutoa dawa zilizokosekana BILA MALIPO (jaribu kuulizia eneo lako utajulishwa.
2. Ukienda Hospitali ukiwa na Bima ya Taifa na Kujuzwa kuwa kipimo flani utalipia au dawa flani ipo ila utalipia, maana yake ni kuwa hospitali au zahanati uliyoenda haina mamlaka (haijakidhi viwango) vya kutoa hicho kipimo au hiyo dawa hivyo unashauriwa uende hospitali kubwa zaidi kama kituo cha Afya ambapo utapata hivyo vipimo na dawa bila malipo
 
Hapa nimeongeza maarifa kwa kiasi kikubwa sana... kumbe ndivyo ilivyo!
Hapa nakumbuka nilivyotokwa arobaini bila kutarajia eti ya miwani halafu zipo hapohapo hospitalini kumuuliza inakuwaje wakati nina bima ya afya ya taifa nikajibiwa "hizi ni za kwangu mimi; za serikali unaweza kupata lakini mlolongo wake utakukatisha tamaa maana lazima tuweke order wilayani wilayani nao mkoani mkoa ndo wapewe kutoka Dar kwahiyo inaweza kuchukua hata mwaka na kitu au miwili". Nilipopewa hilo jibu nikaona ananicheleweshea tu bure na anavutia biashara
 
Kama hata panadol hakuna wanasubiri nini kuzifunga
Mimi Pia nimeshangaa hili swala Kuna zahanati nne niliwahi fika zote hazina dawa, cha kushangaza mpaka panadol hakuna
 
Tatizo la ukosefu wa dawa katika hospital za umma ni la kiufundi sana(very techinical issue). Ni kwamba sera ya wizara au agizo la serikali awamu ya tano ni kwamba wanunue dawa MSD kwa pesa taslimu, ni marufuku MSD kukopesha dawa hata kwenye taasisisi za serikali. Serikali hiyo hiyo haipeleki pesa kwenye taasisi zake kwa wakati na kama inapeleka inakuwa imechelewa sana ili taasisi hizo ziwezo kutumia pesa hizo kununua dawa MSD kwa pesa cash.

Matokeo yake MSD dawa zimejaa, mahospitalini hasa ya serikali dawa hakuna kisa wanakuwa hawajapewa pesa za kununua dawa MSD Kwa hela cash.
Sasa wa kulaumiwa kwa nini akose kwa tatizo lililopo wazi kabisa namna hiyo?

Watu wapo kufikiria njama ama mbinu za upigaji tu, bila kujali wanalipwa marupurupu manono kiasi gani kwa ajili ya utungaji na usimamizi wa sera!
 
Back
Top Bottom