Siku gani ulichacha hutaisahau?

Me nakumbuka niko chuo nina jero tu mfukoni
Nikadaka zangu mkate wa jero nikaukata mara mbili moja nikala asubuh nyingine jion na maji siku ikapita
Kesho yake nikapata mia mbili kwa mwana tukachanga kama watani hv mia mbili mbili tukanunua dagaa wa buku tukagawana vidagaa vichache kila mmoja tukala na ugali


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilikuwa na miadi sehemu ndo siku ya kwanza kukutana, mfukoni sina kitu nikajipa matumaini nitakapofika nitatoa hela, kufika mitandao inasumbua hela haitoki, taarifa haiji, kuwapigia wakanambia kuna tatizo la kimtandao.Hapo ndani nasubiriwa.
Yani nilifedheheka sana siku hiyo, sitaisahau!..
 
Kuna siku nilikuwa na miadi sehemu ndo siku ya kwanza kukutana, mfukoni sina kitu nikajipa matumaini nitakapofika nitatoa hela, kufika mitandao inasumbua hela haitoki, taarifa haiji, kuwapigia wakanambia kuna tatizo la kimtandao.Hapo ndani nasubiriwa.
Yani nilifedheheka sana siku hiyo, sitaisahau!..
Apa ni sisi ambao tumechacha benk hamna ata hela ya kula hamna hujui utakula nini...,we kumbe atm imesumbua kwa masaa
 
Kuna siku niliamka sina hata mia, watoto wanataka kula ndani kuna unga wao wa uji tu kidogo...

Nikamwambia dada waogeshe watoto (wawili) nikawapikia uji wakanywa wakaoga, nikamwambia dada nendeni kwa babu ( wakati huo baba alikuwa anaishi mbali kidogo na kwangu kama 2km) mkashinde huko nitawafuata.

Hapo nimewaza waende kwa babu wakale mchana na jioni huku nitafute namna ya kupata hela ya kuamkia kesho yake. Hao wakaenda zao kumsalimia babu ( kumbe wanaenda kudoea msosi lol)

Basi nikaenda kwa rafiki yangu fundi simu nikamwambia hali halisi akasema we kaa hapa tutakachopata tutagawana. Tumekaa kuanzia saa nne asbh mpaka kumi jioni hakuna mteja dah sasa tufanyaje...

Mara katokea mzee amenunua simu sasa hawezi kuweka application basi fasta nikamwambia lete, nikamwekea zote na nikamwambia kuhusu truecaller akaipenda ikabidi nimdanganye hii inalipiwa mzee akasema hakuna shida.

Akatoa elf 10 ikabidi tugawane na mshkaji wangu, mie huyo nikaenda kufuata watoto, nikasubiri cha usiku tukala kabisa bajeti ya siku ikakamilika. Tukarudi zetu home kulala
 
Back
Top Bottom