Siku gani katika juma watu huamini ni siku yenye mikosi au nuksi?

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,070
3,705
Hapo vipi!

Nimeshakutana na watu wenye kuamini baadhi ya siku kwenye juma zina mikosi, hivyo hufunga hata kazi zao.

Je, hizi siku zipo na je kuna ukweli?
 
Jumanne, sababu kubwa ya siku hii kuwa mbaya ni kutawaliwa na nyota ya Mirihi ambayo ni moto. Ni siku inayotumika kufanya mambo mabaya hasa ya kishirikina na muda wake m'baya zaidi ni saa moja asubuhi na nane mchana.

walozi hutumia siku hii kutumia watu majini na uchawi kufarakanisha watu, kuwapa watu maradhi, kuwasababishia ajali, ufukara wa maisha nk.

Na bado jumamosi nayo pia hutumika kama siku mbadala kulingana na habari zake.

Yote haya yanabaki kuwa imani ya wenye kuamini kama ilivyo dunia kila mtu na yake.
 
Ijumaa ni siku moja mbaya sana. We fika Kariakoo siku ya Ijumaa, utaona wafanyabiashara wengi wanafunga maduka na kutoa sadaka ya damu kwa misukule yao huku wakichoma udi na ubani kabla ya kwenda misikitini kushukuru.
 
Kuna siri kubwa sana katika siku..
 
Jumanne, sababu kubwa ya siku hii kuwa mbaya ni kutawaliwa na nyota ya Mirihi ambayo ni moto. Ni siku inayotumika kufanya mambo mabaya hasa ya kishirikina na muda wake m'baya zaidi ni saa moja asubuhi na nane mchana.

walozi hutumia siku hii kutumia watu majini na uchawi kufarakanisha watu, kuwapa watu maradhi, kuwasababishia ajali, ufukara wa maisha nk.

Na bado jumamosi nayo pia hutumika kama siku mbadala kulingana na habari zake.

Yote haya yanabaki kuwa imani ya wenye kuamini kama ilivyo dunia kila mtu na yake.

Ni Siku ya huyu jamaa
 
Tangu tunakua miaka ile tuliaminishwa siku ya jumanne ni siku ya mikosi na nuksi. Na kweli siku hiyo hatukuruhusiwa kusafiri.

Kwangu binafsi nikipitiaga matukio mabaya hasa ajali karibu zote nimewahi pata siku ya jumanne. Huwa naiangalia hii siku kwa umakini mno.
 
Back
Top Bottom