Siku Dikteta Nikolae Ceausescu wa Romania hakuweza kuyaamini macho wala masikio yake!

Kwani wamekuambia hawajasoma huo upupu wako?

Kuna watu wengine mnashangaza sana. Unajudge watu bila kufahamu undani wake badala ya kuji judge wewe.

People are trapped in history and history is trapped in them-James A. Baldwin
povu lote hilo la nini?
subirini haki yenu iko njiani, na wewe utakufa Kama nyoka, bastard!!!!!
 
Na kwa kawaida Madikteta huwa wanaponzwa na hawa wapambe wanaowashabikia kwa ajili ya kupata kitumbua. Huwa wanapiga ukelele kuwa hakuna tena kama wewe! Lakini yakiwafika hao madikteta huwa unakuwa ni mzigo wao na familia zao hawa wapambe kama Nyani ngabu au Msemajiukweli hutawaona kabisa eneo la tukio au kusema lolote. Na sio ajabu wanageuka kabisa na kumlaani kuwa hakuwa na maana.
Sasa ni wakati wa Jenny kumwambia John hatari ya hawa wapambe na kuwa msalaba wanaweza jikuta wanaubeba wao wenyewe siku blanket la ujinga likifunuliwa kwa wananchi.
 
Kwa takwimu
Polisi Tanzania nzima hawazidi 40000
Ukijumlisha vikosi vyote vya Majeshi Tanzania bara na Visiwani makadirio ni watu 300,000 hadi 400,000

Sasa je hilo kundi litaweza pambana na watu ikitokea watu wamechoka kabisa na wameamua liwalo na liwe
Iwe waue polisi au wao wauuawe?

Maandamano ya kudai haki huanza mioyoni
Watu wakichoka wanaanza onesha kuwa wamechoka
Wakionesha wamechoka watatenda kuchoka kwao
Wakifikia hapo hakuna atakae warudisha nyuma
Wataweka kambi kuhakikisha hakuna kulala hadi nia yao itimie

Naamini sisi ni wengi kuliko wao na ikitokea surprise attack ya maandamano polisi wenyewe wataogopa maana watakua wanaua ndugu zao kisa tu kiongozi ambae kwa kiburi amekua akiwakandamiza

Watawala wanapaswa soma alama za nyakati
Hii inaweza anzishwa na wanafunzi wa sekondari na mkiwaua tu kila mtu huyo anawaibukia
Mabomi ya machozi hayatawazuia watu
Live bullets zitasababisha Marekani aje Tanzania na vile tuna gesi hawezi kawia ni wiki 1 tu ya maandamano wao wanatia nanga
 
Naona wapo watu humu, labda kwa sababu ya umri, hawajui uhusiano na urafiki uliokuwepo kati ya nchi hizi mbili, Jamhuri ya Tanzania na Romania, toka mwaka 1967 Nicolae Ceausesku alipotwaa madaraka ya nchi hiyo.

Jamhuri ya Tanzania iliiona nchi ya Romania kama kaka yake mkubwa na hata Katiba na uongozi wa TANU ilitengenezwa kwa kuiga misingi iliyoshabahiana na chama tawala cha kikomunisti cha Romania ya chama kushika hatamu.

ceausescu-nicolae-2611918-25121989-romanian-politician-pcr-president-B4AAF2.jpg

Pichani Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Tanzania Rashidi Kawawa akiwa na Rais wa Romania Nikolae Ceausescu.
Upepo wa Mageuzi ulipoanza kuzikumba nchi za Kiafrika mwaka 1989, Katibu wa Organization wa CCM wakati huo, Kingunge Ngombali Mwiru, alitumwa kuitembelea nchi ya Romania na kujifunza walivyokabiliana na huu upepo.

Kingunge baada ya kukutana na Rais Ceausescu alirudi Tanzania na kuihakikishia serikali ya Ali Hasan Mwinyi kwamba nchi ya Romania imetulia na iko tayari kutusaidia kukabiliana na upepo huo wa mageuzi ulioanza kushika kasi.

Hata hivyo muda mfupi baadaye maandamano yalianza Romania na pamoja na uimara wa serikali ya nchi hiyo ikisaidiwa na vyombo vya ulinzi na usalama, nguvu ya umma, ilimlazimisha Rais Ceausescu kuikimbia Ikulu ya nchi hiyo.

Maandamano na machafuko nchini Romania yalimchanganya sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye ingawa alishang'atuka Urais na Uenyekiti wa chama tawala CCM bado alikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa.

Kuuawa kwa Rais Ceausescu kulimfanya Mwalimu asome alama za nyakati na hivyo kuiasa CCM kuyapokea mageuzi na ikiwezekana kuwa mstari wa mbele katika kuongoza mabadiliko hayo ambayo aliwaonya hayazuiliki.

Hata hivyo Rais na Mwenyekiti wa CCM Ali Hasan Mwinyi, Waziri Mkuu John Samwel Malecela na Waziri wa Mambo ya Ndani Agustino Lyatonga Mrema waliapa kuwa mfumo wa vyama vingi ungebakia ndoto tu nchini Tanzania.

Majeshi yetu ya Usalama yalitumika vilivyo kuzuia mabadiliko na jeshi letu la polisi na hasa FFU lilitumika kuwapiga, kuwatesa, kuwaumiza na kuwapa vilema vya maisha Watanzania wasio na hatia kwa kosa tu la kudai uhuru zaidi.

Hata hivyo kwa shinikizo nje ya uwezo wao CCM ililazimika kusalimu amri na kuyapokea mageuzi shingo upande. Toka wakati huo hadi leo jukumu kuu la jeshi la polisi limebadilika kutoka kuwalinda wananchi na kuwa kuwalinda viongozi.

Historia ni mwalimu na ingawa Nikolae Ceauseski naye aliisoma historia lakini kama ilivyo kawaida ya madikteta akatoka kapa. Kwa Afrika tumekuwa nao na tutaendelea kuwa nao ingawa mwisho wao haujawahi kuwa salama...

Bokasa, Nguema, Amin, Mobutu na wengine wengi tu, kama Ceausescu, mwisho wao haukuwa mzuri. Bado wanastawi akina Kagame, Museveni, Kabila na wengineo na historia inazidi kuandikwa...swali ni je somo linaeleweka?
 
Nyerere aliwahi kusema, Madikteta sasa "wanabaki zaidi Afrika", lkn mimi naona sasa wanabaki zaidi ktk hii inayojiita Jumuia ya Afrika Mashariki.

Ukiangalia Afrika Magharibi, ni Togo na Cameroon tu ndo bado kuna tawala za kibabe. Shida bado sana sana Afrika Mashariki na Kati.

Ila, with time, hii yote itakuwa historia kwani hiki kizazi cha sasa ndicho kitakuwa cha mwisho kwa tawala hizi zisizo za kidemokrasia ktk ukanda huu.
 
Un
Nikolae Ceausescu alikuwa ni Rais wa Romania na Katibu Mkuu wa chama tawala aliyetawala kwa mkono wa chuma. Kauli yake ilikuwa ni sheria na ole wake aliyethubutu kuukosoa utendaji wake vyombo vya usalama vilimshukia kama mwewe anavyoshukia vifaranga vya kuku.

Baadhi ya wananchi wakiungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu walianzisha maandamano dhidi ya serikali yake. Walikuwa wakimuunga mkono kiongozi wa kidini, Laszio Tokes, aliyekuwa anapiga vita udikteta wakidai uhuru wa kutoa maoni na kulaani ubaguzi wa kikabila.

Tarehe 17 December 1989 wakiwa wanaandamana, vyombo vya usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi na Polisi vya nchi hiyo viliagizwa kuwashughulikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni kwani pamoja na ghasia kutulizwa wananchi wengi walipoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Siku nne baadaye tarehe 21 December1989, Caeausescu alifanya mkutano mkubwa jijini Bucharest kuonesha kwamba wananchi wa Romania walikuwa nyuma yake. Katikati ya hotuba tofauti na siku za nyuma ghafla miguno ilianza kusikika ikifuatiwa na zomea zomea!

Ceausescu hakuweza kuamini masikio yake wala macho yake kwa kilichokuwa kinatokea mbele yake! Mara vyombo vya habari kama TV na redio vilizimwa na kama kawaida vyombo vya usalama viliingia kazini na usiku kucha ilikuwa ni siku ya mapambano baina ya wananchi na polisi.

Kesho yake tarehe 22 December 1989 vyombo vya usalama vilianza kuzidiwa nguvu na wananchi baada ya baadhi yao kuweka silaha chini na kuungana na wananchi. Na siku hiyo ilibidi Ceausescu kuukimbia mji kwa helicopta iliyotua kwenye paa la nyumba walikojificha.

Somo hapa ni kwamba ukombozi huweza kucheleweshwa lakini kuna siku utapatikana tu na siku ikifika dikteta lazima akimbie atake asitake. Nicolae Ceausescu ingawa alitoroka siku hiyo lakini haikuchukua muda...alikuja kukamatwa na kurudishwa aweze kupata haki yake.
[/QUOTE

Unaota ndoto ambazo kamwe hazitatimia.Ni ndoto za Abunuas aliyejenga ghorofa angani na siku nyingine alipiga teke mayai yake halisi alipoota kuaga umaskini kwa kejeli.Kwenye sanduku la kura hamuoni upenyo wa kushinda.Mmenunua mno wa watoa maamuzi ndani ya CCM Mzee wa Msoga akawathibitishia yeye mtoto wa mjini kuliko ninyi.

Mkanunua upande wa pili fursa ya kulipiza kisasi cha maumivu ya hasara,mkaongeza hasara kwa kuwanunua boda boda na wafagia barabara.Tanzania hakuna dikteta wala mama yake dikteta uchwara.Kilichopo ni dili za kihuni zimedhibitiwa.Natamani walio jirani na JPM wamshauri awaruhusu wapuuzi wanaoishi kihuni ruhusa ya kusambaza uhuni wao ili Taifa lijue tuna kundi la aina gani.

Hawana hoja ya kushawishi yeyote aliye na kazi ya kufanya.Wameambiwa zungumzeni kwenye majimbo yenu hawana cha kusema.Wanataka kuzunguka nchi nzima kutangaza ACASIA hawajawahi kutuibia,JPM dikteta,maisha magumu.Wapeni ruhusa waseme ujinga wao ujibiwe sawa sawa wananchi wapime.

Wanaota kutwa kucha maandamano wapeni,sisi tutawataka wanaohimizwa kuandamana wawaombe wanaowashauri wawatangulize mbele wake zao,watoto wao na wazazi wao.Wakikataa tutawauliza walio salia je kuna matumizi sahihi ya akili na nia njema kwa nchi na wananchi
 
Nikolae Ceausescu alikuwa ni Rais wa Romania na Katibu Mkuu wa chama tawala aliyetawala kwa mkono wa chuma. Kauli yake ilikuwa ni sheria na ole wake aliyethubutu kuukosoa utendaji wake vyombo vya usalama vilimshukia kama mwewe anavyoshukia vifaranga vya kuku.

Baadhi ya wananchi wakiungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu walianzisha maandamano dhidi ya serikali yake. Walikuwa wakimuunga mkono kiongozi wa kidini, Laszio Tokes, aliyekuwa anapiga vita udikteta wakidai uhuru wa kutoa maoni na kulaani ubaguzi wa kikabila.

Tarehe 17 December 1989 wakiwa wanaandamana, vyombo vya usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi na Polisi vya nchi hiyo viliagizwa kuwashughulikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni kwani pamoja na ghasia kutulizwa wananchi wengi walipoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Siku nne baadaye tarehe 21 December1989, Caeausescu alifanya mkutano mkubwa jijini Bucharest kuonesha kwamba wananchi wa Romania walikuwa nyuma yake. Katikati ya hotuba tofauti na siku za nyuma ghafla miguno ilianza kusikika ikifuatiwa na zomea zomea!

Ceausescu hakuweza kuamini masikio yake wala macho yake kwa kilichokuwa kinatokea mbele yake! Mara vyombo vya habari kama TV na redio vilizimwa na kama kawaida vyombo vya usalama viliingia kazini na usiku kucha ilikuwa ni siku ya mapambano baina ya wananchi na polisi.

Kesho yake tarehe 22 December 1989 vyombo vya usalama vilianza kuzidiwa nguvu na wananchi baada ya baadhi yao kuweka silaha chini na kuungana na wananchi. Na siku hiyo ilibidi Ceausescu kuukimbia mji kwa helicopta iliyotua kwenye paa la nyumba walikojificha.

Somo hapa ni kwamba ukombozi huweza kucheleweshwa lakini kuna siku utapatikana tu na siku ikifika dikteta lazima akimbie atake asitake. Nicolae Ceausescu ingawa alitoroka siku hiyo lakini haikuchukua muda...alikuja kukamatwa na kurudishwa aweze kupata haki yake.

Hujui historia ya Romania umeokoteza kisehemu tu cha habari na kukiwasilisha kwenye jukwaa kutafuta wajinga wakuunge mkono
 
Hujui historia ya Romania umeokoteza kisehemu tu cha habari na kukiwasilisha kwenye jukwaa kutafuta wajinga wakuunge mkono

Flashback: The New York Times, December 24th 1989

The last speech of Ceausescu - Bucharest, Romania

"In addition, reports said hundreds of citizens have been killed in Bucharest since mass demonstrations against the regime began there on Thursday, when President Ceausescu was booed and shouted into a stunned silence for three minutes as he tried to deliver a speech a day after his return from a three-day state visit to Iran. Security police opened fire on the jeering crowd. "

The event, a political rally organized by the Communist Party, was meant to show support for Ceausescu following the arrest of Rev. Laszlo Tokes, a dissident minister who had been sermonizing against Ceausescu in the city of Timisoara. Romanian television carried the rally live and broadcast it throughout Romania.

Eight minutes into his speech, something went wrong. Chants of "Shut Up!" and "Timisoara! Timisoara!" rang louder and louder throughout the square. A visibly stunned Ceausescu, unaccustomed to such blatant acts of defiance, stopped in mid-sentence.

The shock on his face was seen across the country, and later, around the world. It was the last speech he ever made. Within days, his regime had ended, and he would be hastily tried and brutally executed. The suddenness of his fall shocked the world.

monomotapa, yawezekana ulikuwa hujazaliwa lakini nakuomba uwe na heshima japo kidogo unapotumia JF. Nikolae Ceausescu hakufikiria inaweza kutokea siku wananchi waliomuona kama mungumtu wakamzomea akitoa hotuba. Ni siku ambayo hakuisahau hadi muda risasi zikimiminwa mwilini mwake, yeye pamoja na mkewe Elena.

Wewe unaeijua si ungeiweka ili kupingana nae! Hoja inapingwa na hoja na maandiko kwa maandiko weka yako yenye ukweli tuyapime sio kuhoroja km chizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuongezea tu nampa video ambayo ni wachache waliiona siku hiyo huyo dikteta akizomewa...maneno aliyokuwa akiyasema kwa kugha yao yametafsiriwa, angalieni mshtuko alipoanza kuzomewa...!

Mwanzoni wanaonekana makada wamejipanga mbele wakimpigia makofi lakini ghafla umma unasema hapana, hatutavumilia tena udikteta na kuanza kumzomea. Kama kawaida majeshi yanaanza kumimina risasi kuwaua wananchi. Lakini hatimaye nguvu ya Umma haizuiliki!

1-300x226.jpg

Dikteta Ceausescu hakuamini macho yake wala masikio yake!
 
Flashback: The New York Times, December 24th 1989

The last speech of Ceausescu - Bucharest, Romania

"In addition, reports said hundreds of citizens have been killed in Bucharest since mass demonstrations against the regime began there on Thursday, when President Ceausescu was booed and shouted into a stunned silence for three minutes as he tried to deliver a speech a day after his return from a three-day state visit to Iran. Security police opened fire on the jeering crowd. "

The event, a political rally organized by the Communist Party, was meant to show support for Ceausescu following the arrest of Rev. Laszlo Tokes, a dissident minister who had been sermonizing against Ceausescu in the city of Timisoara. Romanian television carried the rally live and broadcast it throughout Romania.

Eight minutes into his speech, something went wrong. Chants of "Shut Up!" and "Timisoara! Timisoara!" rang louder and louder throughout the square. A visibly stunned Ceausescu, unaccustomed to such blatant acts of defiance, stopped in mid-sentence.

The shock on his face was seen across the country, and later, around the world. It was the last speech he ever made. Within days, his regime had ended, and he would be hastily tried and brutally executed. The suddenness of his fall shocked the world.

monomotapa, yawezekana ulikuwa hujazaliwa lakini nakuomba uwe na heshima japo kidogo unapotumia JF. Nikolae Ceausescu hakufikiria inaweza kutokea siku wananchi waliomuona kama mungumtu wakamzomea akitoa hotuba. Ni siku ambayo hakuisahau hadi muda risasi zikimiminwa mwilini mwake, yeye pamoja na mkewe Elena.

Kwa kifupi tatizo la Romania la wakati huo lilikuwa ni kutaka kujenga taifa la kikomunist basi. Kwa nchi za za magharibi definition number one ya communism ni dictatorship, kama ilivyokuwa USSR enzi hizo na sasa Russia baada ya perestroika, east Germany enzi hizo, north korea kama ilivyo sasa. Kuna nchi kama Libya kwa defitinition ya nchi za magharibi enzi za Gadafi ni dictator leadership......
The 1989 Romanian Revolution and the Fall of Ceausescu - Association for Diplomatic Studies and Training
 
Back
Top Bottom