Siku Dikteta Nikolae Ceausescu wa Romania hakuweza kuyaamini macho wala masikio yake!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,756
Nikolae Ceausescu alikuwa ni Rais wa Romania na Katibu Mkuu wa chama tawala aliyetawala kwa mkono wa chuma. Kauli yake ilikuwa ni sheria na ole wake aliyethubutu kuukosoa utendaji wake vyombo vya usalama vilimshukia kama mwewe anavyoshukia vifaranga vya kuku.

Baadhi ya wananchi wakiungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu walianzisha maandamano dhidi ya serikali yake. Walikuwa wakimuunga mkono kiongozi wa kidini, Laszio Tokes, aliyekuwa anapiga vita udikteta wakidai uhuru wa kutoa maoni na kulaani ubaguzi wa kikabila.

Tarehe 17 December 1989 wakiwa wanaandamana, vyombo vya usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi na Polisi vya nchi hiyo viliagizwa kuwashughulikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni kwani pamoja na ghasia kutulizwa wananchi wengi walipoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Siku nne baadaye tarehe 21 December1989, Caeausescu alifanya mkutano mkubwa jijini Bucharest kuonesha kwamba wananchi wa Romania walikuwa nyuma yake. Katikati ya hotuba tofauti na siku za nyuma ghafla miguno ilianza kusikika ikifuatiwa na zomea zomea!

Ceausescu hakuweza kuamini masikio yake wala macho yake kwa kilichokuwa kinatokea mbele yake! Mara vyombo vya habari kama TV na redio vilizimwa na kama kawaida vyombo vya usalama viliingia kazini na usiku kucha ilikuwa ni siku ya mapambano baina ya wananchi na polisi.

Kesho yake tarehe 22 December 1989 vyombo vya usalama vilianza kuzidiwa nguvu na wananchi baada ya baadhi yao kuweka silaha chini na kuungana na wananchi. Na siku hiyo ilibidi Ceausescu kuukimbia mji kwa helicopta iliyotua kwenye paa la nyumba walikojificha.

Somo hapa ni kwamba ukombozi huweza kucheleweshwa lakini kuna siku utapatikana tu na siku ikifika dikteta lazima akimbie atake asitake. Nicolae Ceausescu ingawa alitoroka siku hiyo lakini haikuchukua muda...alikuja kukamatwa na kurudishwa aweze kupata haki yake.

Update: Kwa ambao hawaamini kwamba Umma ukiamua hakuna risasi wala vifaru vinaweza kuwazuia, naweka hapa hotuba ya mwisho ya dikteta huyu siku ambayo ambalo halikutegemewa lilifanyika.

Hii hapa chini ni vvideo ambayo ni wachache waliiona siku hiyo huyo dikteta akizomewa...maneno aliyokuwa akiyasema kwa kugha yao yametafsiriwa, angalieni mshtuko alipoanza kuzomewa...!

Mwanzoni wanaonekana makada wamejipanga mbele wakimpigia makofi lakini ghafla umma unasema, hapana, hatutavumilia tena udikteta na kuanza kumzomea. Kama kawaida majeshi yanaanza kumimina risasi kuwaua wananchi. Lakini hatimaye nguvu ya Umma haizuiliki!
 
Kwani wamekuambia hawajasoma huo upupu wako?

Kuna watu wengine mnashangaza sana. Unajudge watu bila kufahamu undani wake badala ya kuji judge wewe.

People are trapped in history and history is trapped in them-James A. Baldwin
Kilaza kama kawaida...kweli unajua maana ya kusoma historia! Please read between the lines...kusoma historia kuna maana kubwa kuliko akili yako inavyokutuma!
 
Nimekuambia acha ku-judge watu ambao hata huwajui.

Kilaza ni yule anaye judge watu ambao hata hawajui.

Unaniambia nisome hiyo history, unajuaje kama sikushuhudia hilo tukio au sijasoma hiyo history?

Ondoka kwenye box la fikra finyu!
 
Nikolae Ceausescu alikuwa ni Rais wa Romania na Katibu Mkuu wa chama tawala aliyetawala kwa mkono wa chuma. Kauli yake ilikuwa ni sheria na ole wake aliyethubutu kuukosoa utendaji wake vyombo vya usalama vilimshukia kama mwewe anavyoshukia vifaranga vya kuku.

Baadhi ya wananchi wakiungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu walianzisha maandamano dhidi ya serikali yake. Walikuwa wakimuunga mkono kiongozi wa kidini, Laszio Tokes, aliyekuwa anapiga vita udikteta wakidai uhuru wa kutoa maoni na kulaani ubaguzi wa kikabila.

Tarehe 17 December 1989 wakiwa wanaandamana, vyombo vya usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi na Polisi vya nchi hiyo viliagizwa kuwashughulikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni kwani pamoja na ghasia kutulizwa wananchi wengi walipoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Siku nne baadaye tarehe 21 December1989, Caeausescu alifanya mkutano mkubwa jijini Bucharest kuonesha kwamba wananchi wa Romania walikuwa nyuma yake. Katikati ya hotuba tofauti na siku za nyuma ghafla miguno ilianza kusikika ikifuatiwa na zomea zomea!

Ceausescu hakuweza kuamini masikio yake wala macho yake kwa kilichokuwa kinatokea mbele yake! Mara vyombo vya habari kama TV na redio vilizimwa na kama kawaida vyombo vya usalama viliingia kazini na usiku kucha ilikuwa ni siku ya mapambano baina ya wananchi na polisi.

Kesho yake tarehe 22 December 1989 vyombo vya usalama vilianza kuzidiwa nguvu na wananchi baada ya baadhi yao kuweka silaha chini na kuungana na wananchi. Na siku hiyo ilibidi Ceausescu kuukimbia mji kwa helicopta iliyotua kwenye paa la nyumba walikojificha.

Somo hapa ni kwamba ukombozi huweza kucheleweshwa lakini kuna siku utapatikana tu na siku ikifika dikteta lazima akimbie atake asitake. Nicolae Ceausescu ingawa alitoroka siku hiyo lakini haikuchukua muda...alikuja kukamatwa na kurudishwa aweze kupata haki yake.

Unahangaika kweli we kibabu.
 
Back
Top Bottom