Siku CHADEMA wakichukua nchi, tutarajie haya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku CHADEMA wakichukua nchi, tutarajie haya...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, May 2, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Naamini CDM ni chama kitakachotawala kwa haki, na kuhakikisha kila nafasi ya utumishi wa umma inakuwa na mtu mwenye credibily. Kutokana na serikali ya CCM kuzitumia nafasi za kiutendaji serikalini kisiasa, ni wazi kabisa itakuwa ngumu kuendelea na watu wengi nchi itakapokombolewa. Kwa mantiki hiyo, CDM wakichukua nchi

  Ni majaji wachache sana watakaoqualify kuendelea...
  Ni Wakurugenzi wa wilaya wachache sana watakaoqualify kuendelea...
  Ni makamanda wachache sana wa polisi wa mikoa na ma-OCD watakaoqualify kuendelea...
  Ni mahakimu wachache sana watakaoqualify kuendelea...
  Ni makatibu wakuu wa wizara wachache sna watakaoendelea,
  Ni wakuu wa nyuo, wakurugenzi wa mashirika na maidara, wenyeviti wa bodi, makatibu tawala wachache sana watakaoqualify kuendelea...
  Wakuu wote wa wilaya na mikoa watakuwa discontinued...
  Majority ya usalama wa taifa na takukuru watakuwa discontinued...
  Nafasi ya Dk Hosea itakuwa wazi, ya msajili wa vyama itakuwa wazi, ya IGP itakuwa wazi, ya Manumba itakuwa wazi, za makamishna wote wa polisi zitakuwa wazi...

  Je CHADEMA kitapata watu wenye credibility wa kutosha kujaza nafasi hizo???
   
 2. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Watu wapo wengi sana wenye uwezo ,ni ukweli kwamba siasa intawala kuwaajiri/kuteua watendaji .Pindi mambo yatakapobadilika unaweza staajabu hawa wataalamu walikuwa wapi.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tuko;

  Ni muhimu tukawa tunajitathmini kama tuna uwezo wa kuzitetea Thread zetu kabla hatujazirusha. Nyadhifa nyingi ulizotaja mkuu hapo juu kuzipata hazitegemeaji na siasa, Jaji, Mkuu wa Chuo, Hakimu na nyingine nyingi ni taaluma za watu hizo. Sasa kama sifa ya kupata ajira Tanzania itakuwa ni kuwa na KADI ya CHADEMA hicho ni kitu kingine.

  Hivi unategemea Hakimu aliyeajiriwa kwa sheria ya ajira na waraka wa utumishi wa umaa, CDMA kimfukuze kazi kwa kipengele kipi? au unataka kuonesha umbumbu mbu wa kutoelewa mambo? Hakika huu ni uvundo wa mawazo duh, sijawahi kusikia Nchi ambayo sifa ya mtu kuajiriwa ni Kadi ya CHAMA tawala.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  Thubutuu watakaochaguliwa ni wa kujenga chama
   
 5. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mwanajamii

  Umemjibu vyema kabisa, wale watakao kimbia ni wale walioingia kwenye nyazifa zao kiujanja ujanja.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  wakichukua nchi CDM "which is far away from reality " utaulizwa we dini gani..? unatokea mkoa gani... ndio mambo mengine yataendelea ..
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwenye bold Only in Tanzania.
   
 8. sembo

  sembo JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 3,350
  Likes Received: 1,202
  Trophy Points: 280
  Mi napiga jaramba kujaza nafasi ya EDWARD HOSEAH,
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nafasi zote ulizotaja ni za kuomba kazi ila ccm walijua wakizitangaza watakosa sehemu za kupeleka ndugu zao na rushwa za hela na ngono.

  Kifupi chadema itazalisha ajira za kutosha kwa magraduate.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini wasipate watu wa kuajiri? wakati kuna Vyuo Vikuu Vinawanafunzi wanao graduate?

  Au, Una Maana wengi wa CCM watakimbilia Vijijini kulima?
   
 11. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kweli we njiwa.
   
 12. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  upotofu wa fikra.
   
 13. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  tusihoji je kuna mtu wa kuchukua nafasi zao tu. HOJI PIA JE HAO WALIOPO NAFASI ZAO WANAZITUMIKIA WAPASAVYO? WANAFAA KUENDELEA, HAPO NDU CHUKUA MAAMUZI. BORA UFUNGE DUKA KULIKO KUMWEKA MUUZAJI MWIZI.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nafasi nyingi zilizotajwa ni za kuteuliwa. Kuanzia majaji, wakuu wa mikoa, mkuu wa PCCB, IGP, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurgenzi, nk. Lakini pia si jambo la kutegemea kwamba CDM wakichukua nchi wata overhaul government yote na kuanza upya. Hapo ndipo ugomvi unapoanzia kwani utakuta watu wakidhani kwamba chama chako kikichukua nchi basi wewe automatically unachukua nafasi serikalini. Kuna mchakato hapo. Mfano huwezi kuamka tu na kumfuta jaji kazi. Kuna hawa mabaunsa wa chama nadhani wengine wanadhani CDM ikichukua nchi basi nao watakuwa wanaendele kuwalinda viongozi wa serikali. Haitakuwa hivyo basi hapo wataanza kukishutumu chama chao. Kutengeneza serikali ni mchakato.
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  tatizo la nchi yetu, ni sera na mifumo ya ccm iliyowekwa.

  na mbaya zaidi, ni kuharibu katika kuchagua nani anafaa wapi na kwa nini. CCM wanafanya ni mazoea.
  CHADEMA, ilani yao iko wazi, watendaji wa serikali watapatikana kwa utaratibu ambao utawafanya wawe wawajibikaji kwa wananchi wenyewe, na kiongozi kama RAIS, ni kusimamia uwajibikaji wao
   
 16. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Maana ya mleta mada inapotoshwa kwa maksudi.

  Hoja yake ni pendekezo kuwa iikiwa CHADEMA itachukua nchi mwaka 2015 ,nafasi zote za utumishi wa umma ziangaliwe upya kwa lengo la kuona uwezekano wa kuzifanya mabadiliko.

  Sasa swali ni kuwa hili linawezekanaje?Mabadiliko hayo ,yanaweza tu kutokea kwa kufanya mabadiliko ya sheria na / au katiba.
  Lengo la mabadiliko hayo ni kuona kuwa nafasi zote za utawala wa umma zinashikwa na watu waadilifu,wenye umahiri katika maeneo yao ya kitaaluma,wenye historia ya uchapa kazi na ambao historia za maisha maisha yao nje ya taaluma haina utata wa kimaadili.

  Hili limeweza kufanyika nchini Kenya kwa umakini & ufanisi. Nafasi kama za Jaji Mkuu iliishindaniwa, kwanza kwa kuitangaza nafasi hiyo kwa watu kutuma maombi ikifuatiwa na mchakato wa usaili kwa waombaji, kwa uwazi kabisa huku Wakenya wakifuatilia moja kwa moja kupitia televisheni,na hatimaye mshindi alipatikana.

  Vivyo hivyo kwa nafasi kama Mwanadheria Mkuu wa Serikali na Naibu wake.

  Hata majaji wote wa mahakama ya Kenya pamoja na mahakimu wote waliomba upya nafasi zao na kufanyiwa usaili na chombo maaalumu.Wapo ambao walishindwa kurejea katika nafasi zao!!

  Kwa kifupi nafasi zote nyeti za umma nchini Kenya kwa sasa zinakaliwa kwa kigezo cha meritocracy na sio patronage (connections za kidini ,kikabila,kijinsia ,kirangi na kieneo...

  Swali la msingi ni kuwa iwapo hili linaweza kuwa replicated hapa nchini.
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Wacha uongo wewe.

  hakimu, nakubaliana na wewe, lakini jaji, kamanda wa polisi, wakuu wa vyuo vya umma, wote wana harufu ya siasa pamoja na kwamba wana taaluma zao tena nzuri.

  1. Chukua mfano wa udsm, Mkandala aliteuliwa katika nafasi yake ya sasa akitokea REDET. Ni kupitia REDET alikuwa na kawaida ya kukisifia CCM, na ndiye anayetajwa kuunda ilani ya uchaguzi 2005. Baada ya J.K kupita, alipewa kama asante, na Mathew Luhanga akarudishwa COET kuwa mkuu wa kitivo. Siasa ndo ilifanya kazi.
  2. Majaji wote, pamoja na taaluma walizonazo, lakini mtu huwi jaji mpaka uteuliwe na uapishwe na RAIS.
  3. Makamanda wa polisi, wote file zao ziko ikulu, na kuchaguliwa kwao, lazima kuwa na uhusiano wa karibu sana na IJP, ambaye ni mteule wa Rais, hivyo kwa maneno mengine wanategemea hali ya siasa katika kazi zao. Ndio maana kwa baadhi ya maeneo, wamekuwa wakihamishwa mara moja ikiwa wameharibu michakato miovu ya CCM.
  4. Wakuu wa wilaya, hata mwenyewe unajua wanapatikanaje, wacha uvivu wa kufikiria.
  5. wakurugenzi, ni wateule wa TAMISEM-waziri husika. hivyo nao huharibu hata chaguzi nyingi kwa sababu hiyo. kwa maneno mengine ni wenye kadi za CCM
  6. Makatibu wa wizara wote wanateuliwa na kuapishwa na rais, ndo maana ni wachache walo safi. wana harufu ya CCM
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mkuu haya mambo ya kufuata protocal wakati mwingine ndiyo yanachelewesha maendeleo... kuna watu wakufukuzwa mara moja na wengine wa kujadiliwa.. angalia huyu police chief wa Malawi alifukuzwa siku mbili tu baada ya Banda kuwa rais, ina maana makosa yake yalikuwa yanajulikana before. Hata sisi kuna watendaji wa serikali watakaotimuliwa au kujiuzulu siku chache tu kama CDM itafanikiwa kutwaa madaraka na wanajijua kabisa.

  New Malawi president fires police chief

  Malawi's new President Joyce Banda has fired the nation's police chief and hired a new one,
  her office said on Monday, two days after she took office following her predecessor's death.

  Banda has "appointed commissioner Lot Dzonzi as the new inspector general of police with effect
  from April 8", replacing former top cop Peter Mukhito, said a statement from the office of the
  president and cabinet.
   
 19. k

  kamau ngilisho Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  idara kma USALAMA WA TAIFA MAHAKAMA POLISI hazifanyi kazi wala kujihusisha na siasa bali kwa mujibu wa sheria.
   
 20. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  ccm NAYO ILIZIDI KUWEKA SIASA MBELE KULIKO KUJENGA TAIFA. unajua wakati wa chama chashika hatamu karibia wakuu wa wilaya wote walikuwa darasa la saba? Sifa za mabalozi nchi za nje hazikuzingatia uwezo wa kielimu wa intenatinal relation bali unapendwa vipi kichama, Tazama sifa za Nyang'anyi na Daudi hussein d mwakawago.

  kikwete ndiye aliye wafukuza wakuu wa wilaya wote waliokuwa ma elimu ya darasa la saba na kuteuwa wasomi wa hali ya juu kuongoza wilaya zetu. Tanzania bado nchi inayoyotoa ajira kwa sifa za kisiasa mpaka leo. Nigeria, Kenya, Zambia na Ghana hawajafanya hivyo hata mara moja na ona sasa walipo ki uchumi.
   
Loading...