Siku CCM itakapotenganisha nafasi ya Rais wa JMT na Mwenyekiti basi itakufa hapohapo, Nyerere alijaribu akafeli!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Siku ambayo CCM watakubaliana kutenganisha nafasi ya Rais wa JMT na mwenyekiti wa CCM basi watakuwa wanajichimbia kaburi na watadumbukia mara baada ya kufunga mkutano kitakachobaki ni wananchi kufukia tu kwa mchanga.

Nyerere alijaribu hii wakati Rais Mwinyi alipoingia madarakani mwaka 1985 na mwaka 1987 wakati anatukabidhi kadi za CCM pale uwanja wa Samora mjini Iringa alisema "Ninyi ni wanachama wa mwisho kukabidhiwa kadi na mimi nikiwa mwenyekiti kwani nang'atuka haiwezekani kutenganisha kofia ya Rais na mwenyekiti"

Wakati huo ilikuwa enzi ya chama kimoja tena zilikuwa zinadumu fikra za mwenyekiti wa CCM, sembuse leo kina Mbowe na Zitto udenda unawatoka wakitamani madaraka?

Ramadhan kareem.

Kazi Iendelee!
 
Na hoja yenu hapo kwa namna ninavyofikiri akiwa na hivyo vyeo viwili ni rahisi kutumia vyombo vya serikali kwa maslahi ya chama mfano majeshi, tume ya uchaguzi nk. Ila ukitenganisha itakuwa vigumu kufanya na ni kweli kitakufa maana uwepo wa CCM unategemea serikali bila hivyo hicho chama kwa sasa ni sawa na Chauma tu.
 
... it tells that kuna watu hawataki SRuhusa awe mkiti, sasa inawaletea maumivu ya kichwa...teh

drama na ziendelee
 
Siku zote Mtego huu hutegewa Panya na walikuwa wanakamatika kweli kweli, lakini safari hii kibao kimegeuka, Paka ndio amenaswa na amekamatika haswaaa!!!
 
... kwa kuwa Mungu ameikabidhi Tanzania kwa CCM ili iitawale milele; ni sahihi kabisa. Hamna haja ya kutenganisha maana watakuwa wameenda kinyume na maagizo ya Mungu!
 
Siku ambayo CCM watakubaliana kutenganisha nafasi ya Rais wa JMT na mwenyekiti wa CCM basi watakuwa wanajichimbia kaburi na watadumbukia mara baada ya kufunga mkutano kitakachobaki ni wananchi kufukia tu kwa mchanga.

Nyerere alijaribu hii wakati Rais Mwinyi alipoingia madarakani mwaka 1985 na mwaka 1987 wakati anatukabidhi kadi za CCM pale uwanja wa Samora mjini Iringa alisema "Ninyi ni wanachama wa mwisho kukabidhiwa kadi na mimi nikiwa mwenyekiti kwani nang'atuka haiwezekani kutenganisha kofia ya Rais na mwenyekiti"

Wakati huo ilikuwa enzi ya chama kimoja tena zilikuwa zinadumu fikra za mwenyekiti wa CCM, sembuse leo kina Mbowe na Zitto udenda unawatoka wakitamani madaraka?

Ramadhan kareem.

Kazi Iendelee!
Umefunga mjadala kwa mfano halisi na siyo kwa porojo. Hongera johnthebaptist
 
Huu utaratibu nimzuri si kwa CCM tu Bali kwa chama chochote cha siasa kitakachopenda kudumu ktk dora, hasa kwa nyakati hizi za vyama vingi.
 
Mmoja ana nguvu za dola na mwingine ana nguvu za kisiasa, unadhani nani ata umia wakizinguana? Hao wote ni binadamu .
 
Mpiga zumari wa mama awamu hii ni mstaafu...ameshapiga kelele huko ....haifai kutenganisha
 
Kwa CCM Rais ndio Mwenyekiti wa ChamaDola
Ila kwa vyama ambayo hawashiki dola wabaki kimya tuu
 
Back
Top Bottom