Siku basi la mwendokasi likilipuka na watu ndani ndio Serikali itaanza kuchukua tahadhari?

Mallia

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
322
1,000
Niko Magomeni hapa mwenye macho haambiwi ona kuwa huu mradi kwa sasa umelemewa na sio salama tena kwa afya za watu na usalama wao pia.

Gari 100 haziwezi kuwamudu watu wote wa Dar es salaam ambao wanatumia usafiri huu , magari yamechakaa na yanajaza watu kupitiliza kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa watu, huu mradi unatakiwa uwe na basi mpya haraka iwezekanavyo au ziruhusiwe daladala pembeni ziokoe jahazi.

Madereva wanafanya kazi kwa mazoea na hasira badala ya ukarimu na weledi yaani ni kama wanagawa lifti vile watu wanagombania dereva anafunga mlango kwa makusudi watu wanabanwa milangoni.

Huu mradi kama umewashinda wekeni daladala pembeni msiwape wananchi shida, msitake hadi siku gari lilipuke watu wafe ndio muanze kuchukua Tahadari hii hali sio nzuri.
 

Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
1,991
2,000
Inasubiriwa ajali iundwe tume. Hivi ile ya Morogoro tume ilishatoa majibu?
 

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
772
1,000
Kwanini kusiwe na basi kama hizo za private owned washindane na hao ambao wanakalia hiyo mwendokasi
Na lazima CEO ni mbongo
Hai make sense kwamba mradi mkubwa kama huo ushindwe kujiendesha
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
13,824
2,000
Kwanini kusiwe na basi kama hizo za private owned washindane na hao ambao wanakalia hiyo mwendokasi
Na lazima CEO ni mbongo
Hai make sense kwamba mradi mkubwa kama huo ushindwe kujiendesha
Kama uda ilikufa na ikarius sishangai hata huu ukifa.........waliona wakimpa mzee bakhressa atafaidi
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,002
2,000
Huu mradi wanakula wakubwa tu
Kuna tabia ya viongozi huwa wanajifanya eti ziara ya kushtukiza wakati wanajua yote yanayoendelea

Unafiki uliopitiliza kila siku wanavamiwa ila hakuna anaefungwa kwa WIZI

Anaambiwa miaka mitano hajanunua hata bus moja
Sasa hatua gani zimechukuliwa kwa hela zote walizokula miaka 5?

Huu mradi ungebinafsishwa hata kampuni tatu tofauti na Routes wakapangiwa
La sivyo miaka 50 baadae tutakuwa hapa hapa
 

Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,782
2,000
Kwanini kusiwe na basi kama hizo za private owned washindane na hao ambao wanakalia hiyo mwendokasi
Na lazima CEO ni mbongo
Hai make sense kwamba mradi mkubwa kama huo ushindwe kujiendesha
Mwendokasi tu unatushinda,hizo treni za umeme ndio itakua mzaha kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom