Siku ambayo wajanja tulionekana washamba wa kutupwa

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,554
9,531
Awali ya yote nianze kumshukuru Mungu kwa kuniweka salama salimini
Kwa umri huu lengo la uzi huu
Ni kukumbushana wale tulionekana
Wajanja kumbe ni washamba wa wa kutukuka
Nianze kwa kusema tu katika maisha haya tunayoishi epuka sana kufanya
Mambo yako kijanja kijanja ipo siku
Isiyokuwa na jina wala tarehe utaumbuka amin
Tulikuwa wengi sana tuliofanya mambo yetu kijanja kijanja ila leo hii
Wengine tumehama mpaka mikoa
Kuepuka kuchekwa na tuliowaona
Washamba Hawajui kazi
Kuna wale Tulikuwa na vyeti feki vya kughushi vingine majina ya watu miaka na miaka tukijua ndiyo basi tena hakuna wa kutugusa kuna wafanya biashara tulikuwa wakwepa kodi miaka nenda rudi leo hii tumechunguzwa tukakutwa miaka 20 nyumaa hatulipi kodi kihalali ujanja ujanja tu leo hii tunalia kuna wengine ziwani tulikuwa na Serikali zetu leo hii tuulize kama tuna serikali zetu hatuna kuna wengine tulikuwa vishoka kwenye taasisi za nchi tukionekana Wajanja tumeshtukiwa ujanja wote kwisha wengine tulipata kazi kwa majina ya vigogo nao kumbe walikuwa Wajanja Wajanja leo hii tunalia kilio kimoja epuka sana ujanja ujanja mimi mwenyewe nilikuwa mfanyabiashara leseni moja miradi 6 leo hii nalia na moyo wangu
 
Kuna wengine walikua wanajilipa Posho za Ujanja Ujanja Chai wanakunywa South Afrika Lunch Dubai na Kulala Brussels lkn leo chalii.
Kuna Matoz huko shule walikuwa wanajifanya Ndio wajanja wajanja wa Shule kila wkend Mikadi Beach, Bagamoyo, Club nk leo hoiiiiii na Zero zao mtaaani. Walioshinda Tanganyika Library haoooo wamegeuka Maddon
 
Umetumwa kuanzisha thread kwa mbinu ya kijasusi lakini labda uwafumbe hao washamba wenzio wa Lumumba. Kuaminisha watu kwamba wanaofilisika wote walikuwa wafanyabiashara magumashi ni Uzuzu wa kiwango cha Magogoni. Hata huyo unayejipendekeza kwake unemsikia juzi Arusha analaumu TRA kuwa chanzo cha kufilisika wafanyabiashara kwa kuwekewa kodi zisizo rafiki kwa biashara zao. Wewe unayetegemea fedha ya kujikimu toka kwa Polepole usidhihaki watu waliofilisiwa na udhalimu wa serikali yenu ya Kinyama.
 
Hongera, umejitahidi. Umejitahidi sana, kuna wenzako hawakuwa na ujanja wowote lakini wamepigwa na wimbi. Wanalia pamoja na hao unaowasema walikuwa na silika za janja janja, je, wanaigiza?
 
Awamu ya nne ulikuwa wapi na unafanya nini? tuanzie hapo, Maana unaonekana unabisha usicho kijua. Mpaka kulikuwa na Mawaziri fake, Trafic fake kila kitu kilikuwa fake mpaka dawa za Kufubaza HIV fake.!! wewe hukuona ilo? Jitoe ufahamu kidogo sio unajitoa mazima
 
Wimbi lazima litokee maana Mzunguko wa Pesa ulikuwa Mchafu na msafi kwa wakati mmoja,

Binafsi nashukuru Mungu kwa kumleta Mr John.
 
Hahahahahaha mkuu hawa vijana Hawajui tu tulifanya mengi nyuma ya pazia ni ujanja ujanja tu
 
A
Awamu ya nne ulikuwa wapi na unafanya nini? tuanzie hapo, Maana unaonekana unabisha usicho kijua. Mpaka kulikuwa na Mawaziri fake, Trafic fake kila kitu kilikuwa fake mpaka dawa za Kufubaza HIV fake.!! wewe hukuona ilo? Jitoe ufahamu kidogo sio unajitoa mazima
Alikuwa anaishi kwao mkuu ujanja uja tumeanza awamu ya mzee wa ruksa ila leo hii mambo hadharani
 
Hongera, umejitahidi. Umejitahidi sana, kuna wenzako hawakuwa na ujanja wowote lakini wamepigwa na wimbi. Wanalia pamoja na hao unaowasema walikuwa na silika za janja janja, je, wanaigiza?
Hao kama walipitiwa basi ni msafara wa mamba mpaka mijusi wamo sisi magwiji wa ujanja ujanja ndiyo tunajua ni wapi tulianzia
 
Umetumwa kuanzisha thread kwa mbinu ya kijasusi lakini labda uwafumbe hao washamba wenzio wa Lumumba. Kuaminisha watu kwamba wanaofilisika wote walikuwa wafanyabiashara magumashi ni Uzuzu wa kiwango cha Magogoni. Hata huyo unayejipendekeza kwake unemsikia juzi Arusha analaumu TRA kuwa chanzo cha kufilisika wafanyabiashara kwa kuwekewa kodi zisizo rafiki kwa biashara zao. Wewe unayetegemea fedha ya kujikimu toka kwa Polepole usidhihaki watu waliofilisiwa na udhalimu wa serikali yenu ya Kinyama.
Na umri huu nitumwe kweli wewe kama ulifanya mambo yako kijanja kijanja njoo tuungane tu
 
Awali ya yote nianze kumshukuru Mungu kwa kuniweka salama salimini
Kwa umri huu lengo la uzi huu
Ni kukumbushana wale tulionekana
Wajanja kumbe ni washamba wa wa kutukuka
Nianze kwa kusema tu katika maisha haya tunayoishi epuka sana kufanya
Mambo yako kijanja kijanja ipo siku
Isiyokuwa na jina wala tarehe utaumbuka amin
Tulikuwa wengi sana tuliofanya mambo yetu kijanja kijanja ila leo hii
Wengine tumehama mpaka mikoa
Kuepuka kuchekwa na tuliowaona
Washamba Hawajui kazi
Kuna wale Tulikuwa na vyeti feki vya kughushi vingine majina ya watu miaka na miaka tukijua ndiyo basi tena hakuna wa kutugusa kuna wafanya biashara tulikuwa wakwepa kodi miaka nenda rudi leo hii tumechunguzwa tukakutwa miaka 20 nyumaa hatulipi kodi kihalali ujanja ujanja tu leo hii tunalia kuna wengine ziwani tulikuwa na Serikali zetu leo hii tuulize kama tuna serikali zetu hatuna kuna wengine tulikuwa vishoka kwenye taasisi za nchi tukionekana Wajanja tumeshtukiwa ujanja wote kwisha wengine tulipata kazi kwa majina ya vigogo nao kumbe walikuwa Wajanja Wajanja leo hii tunalia kilio kimoja epuka sana ujanja ujanja mimi mwenyewe nilikuwa mfanyabiashara leseni moja miradi 6 leo hii nalia na moyo wangu
Omba Mungu akili zako ulizozitupa ili upate mkate wa kila siku kwa kulamba miguu ya ngosha zirudi kabla ya 2020!!
 
Wewe ndiyo uombe na siyo mimi hatua niliyonayo itakuchukua wewe miaka 37 kuifikia
 
Hakika huu Uzi unaonekana umeandikwa na mjanjamjanja na ni wakijanjajanja lakn kiuhalisia una maana kubwa sana. John Magu kapindua meza ya matokeo tena uwanja wa ugenini bila timu mwenyeji kutarajia!
 
Wimbi lazima litokee maana Mzunguko wa Pesa ulikuwa Mchafu na msafi kwa wakati mmoja,

Binafsi nashukuru Mungu kwa kumleta Mr John.
Ujinga na upumbavu ni sifa mbaya tulizonazo wanaadam. Lakini no afadhali ya mjinga aweza kubadirika toka kwenye ujinga wake akapata werevu,ambayo no sifa njema. Lakini mpumbavu biblia inasema hata ukimtwanga kinuni pamoja na ngano,ngano itaiva mpumbavu atatoka kama alivoingizwa. Kama unakiri uliishi kiujanja ujanja na kufurahia maisha,Leo umegwukeje na kukurahia ukata uliopo au ulionao. Daah! Tanzanian
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom