Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Kitendo cha chadema kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame(orodha ya aibu ya mafisadi papa ) ya chadema kiliumiza wengi na kuonyesha wazi kuwa chama kuongozwa na aliyepata zero form six ni hasara tupu.
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Duh? Bado unasherehekea tu?
 
Leo una m miss. Ha ha ha ha
 
Ukisoma michango ya wakereketwa wa chamadola utagundua hata wao wanaamini ni bora Msoga kuliko Chato.
 
Haka kajamaa saa hii kapo tayari kumpigia JK kampeni nchi nzima ili arudi awe rais tena!

Ni bavicha hata kwenye familia zao hawana misimamo. Ni kama mashoga.

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika watu niliotokea kuwadharau ndani ya JF, mmoja wao ni huyu jamaa mwenye hili bandiko, yaani hako kacheo alichonacho katika chama chake kimemfanya awe mtu wa kusikitisha sana,ingawaje mwenyewe anajiona akili kubwa.
 
Katika watu niliotokea kuwadharau ndani ya JF ,mmoja wao ni huyu jamaa mwenye hili bandiko,yaani hako kacheo alichonacho katika chama chake kimemfanya awe mtu wa kusikitisha sana,ingawaje mwenyewe anajiona akili kubwa.
Lakini unamsoma na kumjibu inatosha.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom