the ultimatum
JF-Expert Member
- Dec 16, 2012
- 401
- 104
Ni matarajio ya wana CCM wote kuona CHADEMA inasambaratika. Mbinu nyingi sana zinatumika na ambazo zimekwishatumika ili kuisambaratisha CHADEMA. Mbinu nyingi ambazo zimetumika CHADEMA wameweza kuzibaini na kusonga mbele kitu ambacho kilitia na kinaendelea kutilia shaka mipango ovu inayofanywa na CCM dhidi ya CHADEMA.
Suala la kuvuliwa uongozi kwa Zitto na wenzake katika chama ni kete nyingine na ambayo ni ya juu kabisa kwa wana CCM ya kujaribu kuitumia ili kuisamabaratisha CHADEMA.
Kinachotokea ni kwamba kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 kuna hatari kubwa sana ya kutokea mpasuko wa makundi ya urais ndani ya CCM hivyo kuicha CHADEMA iende kwenye uchaguzi mkuu kwa nguvu na kasi hii kunahatari kubwa sana ya CHADEMA kuchukua dola.
Kinachonifanya niamini kuwa ipo siku wana CCM wataumbuka ni kwamba; kwakuwa wao wanaamini kwa suala la Zitto CHADEMA imeshajichimbia kaburi, na kwakuwa tumeshaona jitihada kadha wa kadha zinazofanya na baadhi ya makada waliowahi kutimuliwa CHADEMA katika kuuaminisha umma kuwa maamuzi ya kamati kuu ya kuwavua uongozi Zitto na wenzake hayakuwa sahihi na kwakuwa kuna kila dalili za kuamini kuwa watu hawa wanatumiwa na CCM ili kutimiza malengo yao ya kuisambaratisha CHADEMA, siku ambayo wataumbuka ni kama ifuatavyo.
Ni siku ambayo aidha Zitto hatavuliwa uanachama na kamati kuu labda kutokana na utetezi wake aliotakiwa auwasilishe ndani ya siku 14 yeye pamoja na wenzake. Ni siku ambayo Zitto atakili pamoja na mapungufu ya kibinadamu kuwa mikakati ambayo walikuwa wakiifanya haikuwa na nia ya kuleta umoja wa kichama bali kudhoofisha. Ni siku ambayo kiongozi Zitto Zuberi kabwe pamoja na kutambua umuhimu wa kuiondosha CCM madarakani kwa wakati huu wenye uhitaji mkubwa kwa watanzania, akaamua kuungana kwa nguvu zote kwenye M4C ya chama, ikiwa ni pamaoja na kufanya mikutano mikubwa ya pamoja na viongozi wote wa chama akiwemo Mbowe, Slaa na wengine katika ukanda ambapo Zitto ametokea na maeneo mengine kote nchini.
Hakika kama hili hilatatokea litakuwa ni pigo kubwa sana kwa CCM na vibaraka wake na kiama cha CCM kitakuwa kimetimia.