• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Siku Aisha ''Daisy'' Sykes alipofuatana na baba yake Msasani kwa Mwalimu Nyerere kuhusu Historia ya TANU 1968

Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,342
Points
2,000
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,342 2,000
SIKU AISHA ''DAISY'' SYKES ALIPOFUATANA NA BABA YAKE MSASANI KWA MWALIMU NYERERE KUHUSU HISTORIA YA TANU 1968

Hakika wengi wangependa kama historia hii niliyoandika isingekuwa kweli na watu hawa niliowarejesha kwenye historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na uhuru wa Tanganyika baada ya kufutwa wangekuwa hawakuwapo bali ni hadithi ya mtunga hadithi hodari.

Lakini watu hawa walikuwapo na wanafahamika na mmoja wa watu hawa ni babu yangu, Salum Abdallah ambae nimeeleza historia yake kwa ushahidi wa historia yenyewe na picha.

Daisy ameeleza historia ya baba yake wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika na katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake aliandika makala ambayo mimi nimeiandikia utangulizi.

Nakuwekea kipande cha makala hiyo na utangulizi wangu kukudhihirishia kuwa haya nikwaambiayo ni kweli:

Utangulizi

Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku ni binti ya Abdulwahid Sykes mmoja kati ya wazalendo 17 waliounda chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Daisy kama anavyofahamika zaidi kwa jina hili, ni msichana wa kwanza Mwafrika kusoma Shule ya Wasichana ya Aga Khan mwanzoni mwa miaka ya 1950 na msichana wa pili kuingia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1960.

Daisy amefahamiana na wazalendo wengi mmoja wapo akiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na machifu mashuhuri kama Mangi Mkuu Thomas Marealle waliokuwa wakifika nyumbani kwa baba yake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha baba yake, Daisy ameandika makala haya kukumbuka siku zile zilizojenga haiba ya baba yake na ya wazalendo walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa miaka mingi Daisy amekuwa akiishi na kufanya kazi nje ya Tanzania:

BABA YANGU ABDULWAHID SYKES KAMA NINAVYOMKUMBUKA
Na Daisy Sykes Buruku

''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.

Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar- es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes.

Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.

Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.

Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.

Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.

Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.

Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.

Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''

2197568_DAISY_POTRAIT.jpg

Picha 1. Daisy Sykes Buruku

2197569_WAASISI_WA_TANU_1.jpg

2. Waasisi wa TANU 1954

2197570_JOHN_ILIFFE.jpg

3. John Iliffe​
 
M

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,888
Points
2,000
M

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,888 2,000

View attachment 1248206

Picha 1. Daisy Sykes Buruku

View attachment 1248207
2. Waasisi wa TANU 1954

View attachment 1248208
3. John Iliffe​

Shk Mohamed said, tunashukuru kwa historia hii, jee itaendelea au ndiyo mwisho??.
 
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
5,930
Points
2,000
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
5,930 2,000
Mzee wa historia za kubumba
 
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,342
Points
2,000
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,342 2,000
Anamaanisha eti za uongo
Shark,
Angeniambia sababu ya kusema kuwa sisemi kweli angenisaidia sana.

Historia hii niandikayo ni kweli kabisa na ukweli wake umethibitishwa na wasomi wa African History katika vyuo tofauti Marekani na Ulaya na kitabu nilichoandika sasa ni kitabu cha rejea kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Haya nishayaeleza hapa mara nyingi kuwa baada ya kitabu hiki nimealikwa kwenye vyuo Marekani Ulaya na Afrika na nimezungumza.

Vilevile nimetiwa katika miradi miwili ya historia ya Afrika ya Oxford University Press Nairobi na Oxford University Press, New York wakishirikiana na Harvard na nimeandika na kazi zangu zote mbili zimechapwa.

Lakini simlaumu.

Kitabu nilichandika kimebadili historia nzima ya TANU, uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.

Wapo waliofurahishwa na kazi hii yangu na pia wako walioghadhibika na akili zao zinakataa kuamini kuwa historia waliyosomeshwa siyo yenyewe.
 
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Messages
1,348
Points
2,000
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2013
1,348 2,000
kwanini anatumia jina la kikristo(daisy) badala ya kiislamu(aisha)?. aliamua kuachana na uislamu?.
2201000_IMG_20191102_084759.jpeg
 
LIKE

LIKE

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Messages
3,641
Points
2,000
LIKE

LIKE

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2013
3,641 2,000
Heshima kwako

kiini cha maandiko yako ni akina Sykes na wazee wako..

ilikuwaje hadi hao wazee hawapo kwenye historia ya nchi.?

na Je kulikuwepo na figisu figisu walizitenda kama za akina Kasanga Tumbo au Kambona.?
 
Forum statistics

Threads 1,405,595
Members 532,049
Posts 34,490,026
Top