Siku 7 za maombolezo tutafakari ombi la mwisho la Mkapa kutaka kuona Tume Huru ya Uchaguzi na upinzani kushirikishwa katika tume

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,547
2,000
IMG_20200724_090624.jpg

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amesema kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ni njia mojawapo ya kuondoa manung’uniko ya vyama vya siasa na kuimarisha demokrasia barani Afrika.

Mkapa, rais wa kwanza wa Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi, ameandika hayo katika kitabu chake cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kinazungumzia matukio na maamuzi aliyofanya katika utawala wake wa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, akijutia na kukubali kubeba lawama zote kwa baadhi ya matukio, huku akieleza somo alilopata.

Mkapa amesema ili kuwa na usawa katika mfumo wa vyama vingi nchini, ni muhimu kuwa na chombo huru kilichojumuisha vyama vyote.

“Kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na Vyama vyote vya Siasa ndio chachu ya kulea na kukuza demokrasia nchini,” anasema Mkapa, ambaye anasema alipata funzo kubwa la umuhimu wa kushirikiana na vyama vya siasa baada ya mauaji ya wafuasi 22 wa CUF yaliyofanywa na polisi kisiwani Pemba mwaka 2001.

Zaidi soma >Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
1,426
2,000
Kuuliza kwanini hakufanya hivyi wakati yupo madarakani ni swali zuri na la maaana.

Lakini swali hili haliondoi ukweli kuwa hayati alikuwa anajua uhitaji wa tume huru kwa ustawi wa demokrasia.

Utawasikia wanaoshiba leo kwenye hii awamu wakiuliza '' tume huru ya nini!?

Amini nawaambia baadhi yenu tayari swali hili linawatafuna sasa.

Membe
 
Jul 23, 2020
10
75
Rais mstaafu Mkapa alivyodai Tume huru ya uchaguzi.

BENJAMIN William Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehitimisha safari yake ya miaka 81 dunia.

Mkapa aliyeiongoza Tanzania kwa miaka kumi kati ya mwaka 1995-2005, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya Hospitali jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Taarifa za kifo chake, zimetolewa na Rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli saa 6 usiku wa kuamkia leo na tayari ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa afariki dunia.

JPM atangaza siku 7 za maombolezo, bendera nusu mlingoti.

Mkapa amefariki ikiwa ni takribani miezi tisa tangu kilipozinduliwa Kitabu chake cha “My Life, My Purpose” (Maisha Yangu, Kusudi Langu). Katika kitabu hicho, anajutia na kukubali kubeba lawama zote kwa baadhi ya matukio, huku akieleza somo alilopata.

Kitabu hicho kilizinduliwa na Rais Magufuli tarehe 12 Novemba 2019 siku aliyoadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwake, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. View attachment 1515464
 

Zegota

Senior Member
Jun 5, 2020
198
500
Unajua ndio naamka sasa hivi nawasha data nakutana na habari za kifo cha BWM hapa jamvini ni kweli kafa au propaganda zenu tu?

Maana mpaka sasa sielewi kama ni kweli au uzushi
 
  • Love
Reactions: BAK

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,398
2,000
Eeh tusihishie kusema RIP tu. Atapumzika kwa Aman tukiishi na kuyatenda Yale aliyoyaandika katika kitabu my life, my purpose . Na huu ndo upendo wa kweli . Ombi kwa serikali ni kuwa itimize kusudi lake.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,401
2,000
UTAIFA = CHADEMA + CCM + NCCR+ ACT+ CUF+ UDP.........+ WAPAGANI ....+ .....


Ili tufikie utaifa tunahitaji marais wastaafu wajuwe

1. CCM SIO WATANZANIA pekee

2. WATETEE WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI, sisiem nikasehemu tu

3. WASIKAE KIMYA WANAPONYANYASIKA WATANZANIA WASIO CCM na hapo ndipo tupowaona sio viongozi wakitaifa

UTAIFA NIKUTHAMINI UTANZANIA SIO KUTHAMINI UCCM NA KUPUUZA UTANZANIA wasio CCM

TANZANIA NA WATANZANIA NI ZAIDI YA CCM.

TANZANIA + WATANZANIA = UTAIFA

Mungu tubaliki watanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom