Siku 572, Magufuli bado anaisuka Serikali yake

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
f07a4247f3696a6c888bd198ade594f1.jpg


[HASHTAG]#Tenguateua[/HASHTAG] mpaka lini?
kwa haki ilivyo sasa rais bado anapambana na kuunda serkali badala ya kujishughulisha kutatua kero za wananchi wake

Pia huenda asiishie katika kuunda serkali, bado Magufuli yupo na anaendelea na kampeni za uchaguzi kwa kuendelea kutoa ahadi mbalimbali huku akiwa ametumia muda wa siku 572 magogoni
 
Amelewa madaraka na hivyo kuyatumia vibaya madaraka yake kwa kuwafukuza kazi wengi ambao hawakustahili kufukuzwa kwa sababu hawakutenda kosa lolote lile. Aliyekuwa msajili wa hazina Lawrence Mafuru alifukuzwa kwa kusema kweli kwamba hakuna makosa yoyote kwa taasisi za Serikali kufungua fixed deposit na pia hakuna mfanyakazi Serikalini mwenye mshahara wa 40 million kwa mwezi. Nape alifukuzwa kazi kwa kulinda utawala wa sheria nchini dhidi ya yule muhuni na mkolomije na IGP naye kwa kuomba samahani waandishi wa habari. Hii ni mifano michache tu.

Na cha kustaajabisha Mkolomije wa Kolomije pamoja na kuidanganya Serikali kuhusu jina lake, kufoji vyeti na kuvamia Clouds bado anakingiwa kifua! Huyu kweli ni mchapa kazi! Hapa Ukolomije tu mbele kwa mbele.
 
Dhana ya kusema 'anaisuka serikali yake' kwenye hili gazeti niya kisiasa zaidi badala ya kisheria.

Kama Rais ataacha kuisuka serikali basi hata bunge litakuwa halina kazi.

Kuisuka serikali ni kazi endelevu kama ilivyo kwa bunge kutunga sheria ili zikaisuke serikali.

Rais Kikwete aliendelea kufanya teuzi mbalimbali (kuisuka serikali) wakati alibakiza siku kadhaa kuondoka madarakani.
 
Kuisuka serkali ndio kuteua viongozi na kuwaondoa kila siku?

Tena mbaya zaid anawateua mwenyewe

Kwanza, si kweli kwamba kila siku anateua viongozi na kuwaondoa.

Pili, kama hao wanaoteliuwa utendaji wao wa kazi hauridhishi, yeye Magu afanye nini sasa?

Hata ingekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo anavyofanya.

Mtu kama utendaji wake wa kazi hauridhisi, fukuza tu.
 
Tumempa miaka mitano aweke mambo sawa halaf miaka mitano mingine aanze kutekeleza sera za viwanda
 
Kwanza, si kweli kwamba kila siku anateua viongozi na kuwaondoa.

Pili, kama hao wanaoteliuwa utendaji wao wa kazi hauridhishi, yeye Magu afanye nini sasa?

Hata ingekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo anavyofanya.

Mtu kama utendaji wake wa kazi hauridhisi, fukuza tu.
Uko nchi gani mkuu?

Hizi teua tengua huzioni?

Suala la kuteua watendaji wasiomrizisha huo ndio udhaifu wake!
nchi ina personnel wengi waadilifu na wenye uwezo mkubea, shida yake ni "u mbao fc" katika teuzi zake nyingi, na kwa style hii hatafanikiwa!
 
Back
Top Bottom