Siku 45 za mateso ya kupumua hatimaye nimepona, Utukufu kwa Mungu

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Tarehe 23 Mwezi wa nne ndio tatizo lilianza nikiwa kazini, yalianza kama mafua then jioni ikaja homa kali sana, ikabidi asubuhi niende kituo cha afya kupima wakaniambia nna Malaria na UTI pia so nikapewa mseto na Azuma nitumie, baada ya siku tatu sikuona nafuu yoyote mafua ndio yalikata tu ila homa ilikuwa inapanda na kushuka tu

Baada ya wiki moja Pua ikapoteza kabisa uwezo wa kunusa yani hata upulizie spray kali au perfumu kali sihisi chochote, Baada ya hapo taste ya chakula nayo ikapotea, hapo ndiopo uwoga ukawa mkubwa zaidi

Ikanibidi nijitenge mwenyewe sababu naishi peke yangu na sehem isiyochangia vitu na watu nikaona liwalo na liwe hata ndugu sikuwaambia chochote maana nilihofu kuwaletea majnga endapo nilikuwa nayo, na ukiangalia dawa hamna

Siku ya kumi ikawa ya kuogopesha zaidi maana kifua kikaanza kubana yaani pumzi inabana na mbavu zikawa zinabana pia, ukiangalia hapo hata hospitali kwenda niliona hamna msaada kutokana na habari nilizokuwa naziskia, nikaona ni heri nipambane mwenyewe

Nikaenda Dukani kutafuta Vitamin C, nikaambiwa hamna, moja kwa moja nikaanza kupambana na Tiba asili tu maana kwa zile dalili zilitosha kunipa alert kuwa ni nini kinachonisumbua maana kwa hali halisi ilikuwa inajulikana na wiki chache kabla ya kuumwa nilikuwa na mizunguko mingi ya mjini

Ilifika hatu nikaanza kuomba ushauri kwa Baadhi ya member jf
Screenshot_20200607-140813.jpg


Moja kwa moja nikaanza na Nyungu lakini ikawa inashusha homa baada ya mda inarudi, kilichofuata cha kutisha zaidi ni siku ya kumi na nne, ambapo nilianza kuona Dalili za baadhi ya sehem za mwili zinapooza kama mkono wa kushoto hadi mguu, Moja kwa moja nikahisi huenda ndio yale yaliyosemwa kuwa Ule ugonjwa unaleta athari za kuganda kwa Damu kwenye mwili hivyo hupelekea watu kupata stroke

Nikaanza tiba ya malimao, Tangawizi,Kitunguu swaumu vitunguu maji, Binzari nikawa nachanganya nakunywa kila baada ya masaa 4, ile hali ya kupooza ikapotea, nikawa nakula pia na mboga za majani kwa wingi

Pia kuna mtu akanishauri ninunue unga wa Ubuyu niweke kwenye maji ninywe kama juisi kwani una vitamin c ya kutosha zaidi ya Machungwa, nikawa natumia, Akanishauri pia nitumie unga wa mlonge, na Habatt soda nichanganye na asali nitumie kwani zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuboost kinga hivyo mwili utapambana na hali itakuwa nzuri

Baada ya siku kadhaa huo mchanganyiko umenisaidia na sasa niko imara kuliko mda wote, ila nimepungua sana tu sababu ya stress maana stress ndizo zinauwa watu wengi kuliko ugonjwa wenyewe, kwa sasa kifua kimeachia, kuhisi harufu kumerudi, ladha imerudi na mwili upo imara kabisa,

Nilijua nitakufa cz hata usingizi usiku nilikuwa sipati yani nikilalala naona majeneza lakini Mungu ni mkubwa, now tokea wiki iliyopita Namerudi kazini nikiwa imara zaidi, niwashukuru member wote wa jf walionipa ushauri wakati nipo katika kipindi kigumu

Pia nishauri yoyote atakayekutwa na hali hii, cha kwanza asiwe na stress maana stress zitaenda kutibua magonjwa mengine kama magonjwa ya moyo na kuathiri ufanyaji kazi wa kinga ya mwili wako hivyo Ugonjwa utakuondoa kirahisi

Pili aache kabisa kutembelea page za habari za kutisha, Habari za kutisha zinachangia kukatisha tamaa na utajihisi unaenda kufa lakini siyo

Nne usilale amka fanya mazoezi tembea hata ndani hapo hapo , ukilala mda mrefu ndio unaupa nafasi ugonjwa kukuuwa, Inasemekana unapolala mda mrefu virusi ndio vinapata nafasi ya kushambulia Mapafu yako Na kugandisha damu kwenye mishipa kitu ambacho kitakupelekea kupata stroke, hivyo ukifanya mazoezi mara kwa mara unazuia kasi ya virusi kushambulia mwili na kugandisha Damu kwenye Mapafu kitu ambacho kitafanya mapafu yasiathirike na mwili uendelee kupambana

Tano, kula vizuri mlo kamili na matunda kwa wingi kama Machungwa,Machenza ,Parachichi,Papai,

Usijichanganye na wengine, Ukitoka vaa Barakoa yako ili kuwalinda wengine na pia ukipata nafuu au kupona, endelea kujulinda maana unaweza pata maambukizi mapya japo wanasayansi wanasema kuwa Hata vikirudi tena mashambulizi yake hayawezi kuwa makali kama ya mwanzo maana kinga ya mwili wako inakuwa ishajijengea uwezo wa kupambana na hao virusi.

Kumbuka si kila mwenye Huu ugonjwa Anakohoa au kuwa na Homa kali, wengine Dalili hazionekani hata joto la mwili linakuwa la wastani kitu ambacho kinafanya mtu asitambulike kirahisi, cha muhim endelea kuchukua Tahadhari zako binafi maana huu ugonjwa wengine ukiwakuta hawapati dalili kali, two weeks wanapona wenyewe na wengine ukiwakuta mtu hatoboi siku tatu, hivyo Tahadhari ni muhimu

Stay Safe everyone...
 
Kwa hio wewe bado ni mtotomtamu au kuna mabadiliko? Pole sana.
 
Pole sana boss.Nimefarijika kukuona tena.
Nadhani hofu yako pia ilichangiwa zaidi na wazee wa kutisha watu humu na matanzia na kuconclude kuwa wamekufa kwa koona.
Nami pia dalili zilinishika ila njia ulizotumia wewe nami nilitumia hizo hizo;kujifukiza,tangawizi,malimao,mazoezi na kula vizuri.Nashukuru Mungu nilivuka.
Siku nyingine tena chukua ushauri kwa watu waliopona au kuvuka kikwazo husika achana na porojo za baadhi ya walevi humu.
 
yaani zile tanzia ndio ziliniletea stress zaidi
Pole sana boss.Nimefarijika kukuona tena.
Nadhani hofu yako pia ilichangiwa zaidi na wazee wa kutisha watu humu na matanzia na kuconclude kuwa wamekufa kwa koona.
Nami pia dalili zilinishika ila njia ulizotumia wewe nami nilitumia hizo hizo;kujifukiza,tangawizi,malimao,mazoezi na kula vizuri.Nashukuru Mungu nilivuka.
Siku nyingine tena chukua ushauri kwa watu waliopona au kuvuka kikwazo husika achana na porojo za baadhi ya walevi humu.
 
Pole sana. Kama unamtegemea Mungu wa mbinguni anaandikwa hivi "Mungu", siyo "mungu". Ukishaandika "mungu" basi siyo wa mbinguni huyo.

Mungu ni mungu tu, kila jambo linaenda kwa nia, kama umemaanisha mungu toka moyoni ni mungu tu, hata uandike MUNGU lakini imani haipo nafsini haina maana!

Tusi”complicate” mambo mkuu.
 
Hata Abdallah huandikwa Abdallah na siyo abdallah, sembuse Mungu? Tatizo kuna wengine humu mliruka shule ya msingi na sekondari mkaenda chuo kikuu moja kwa moja. M kubwa na m ndogo zina tofauti sana. M kubwa ni kwa Mungu wa mbinguni. Na m ndogo ni kwa miungu. Kuandika kwa m ndogo unamaanisha miungu. Ndio ukweli huo. Kama hukusoma rudi shuleni.
Mungu ni mungu tu, kila jambo linaenda kwa nia, kama umemaanisha mungu toka moyoni ni mungu tu, hata uandike MUNGU lakini imani haipo nafsini haina maana!

Tusi”complicate” mambo mkuu.
 
Mkuu kuna jamaa yangu npo nae cku ya nne hii hasense harufu yyte,mm nlishikwa na mafua jana sema sion kama yananisumbua sanaa cz nafanya jogging hata mchana,sema jamaa hama ham ya kula wala hapat harufu ya kitu chochote,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom