Siku 30 Nzito za Maisha Yangu. ooh, Glory to God!!!

wapendwa,

niko chumani kwangu saa hizi na nahisi pumzi zinataka kukauka. nina mchanganyiko wa wasiwasi na matumaini, japo najiamini kwa hili ninalotarajia kulifanya, lakini tashwishi na mchecheto vinanizinga, nimeona niwashirikishe huenda nikapata tafu japo kidogo!!

ni kwamba baada ya siku 30 zijazo yaani jumatano ya tarehe 1 june 2011, nitamuarifu rasmi kijana mmoja kuwa nimemteua kuwa mchumba wangu!!!

ni uamuzi mgumu na mzito sana kwangu mimi binafsi. kijana huyu nimemfahamu tangu mwaka 2006 alipoanza kunitaka mapenzi, tumezunguka naye sana katika mitaa ya mapenzi huku nikihakikisha kuwa anaupata moyo wangu kikamilifu japo mwili wangu sikumruhusu kuufunua. kwa kweli tumehangaika naye sana na tumewahi "kukosana" naye mara kadhaa kisha tunarudiana. natumaini mnanielewa vyema ninaongea nini hasa ninaposema "kukosana"

baada ya misukosuko yote, hatimaye alinielewa vyema nami nikamuelewa, sasa kila kilichokuwa kinazuia sisi kuwa mwili mmoja kimeondoshwa kwa neema za Mungu. nimeamua kuwa June mosi nitamthibitishia kuwa ndiye mume wa ndoto zangu. naam, mume wa ujana wangu! kama hatakuwa na objection, siku ya jumamosi ya tarehe 4 June, nitamtambulisha nyumbani kwetu na kumtaka naye apange siku ya kunipeleka na kunitambulisha kwao. kama mambo yataenda kama ninavyoomba, ndoa itafungwa mwezi october au novemba 2011!!

sasa nadhani mnaweza kuuhisi wakati niliomo ni wa aina gani.

naomba maombi yenu wote tuweze kuvuka salama. mimi naanza maombi mazito mfululizo kumkabidhi Mungu siku hizi zote 30 (and beyond) aziratibu mwenyewe kwa kadiri ya wingi wa rehema na fadhili zake

Mungu awabariki sana

mpenzi wenu Miss Judith (Mrs mtarajiwa)

Glory to God!


Judith Mungu nimwema na fadhili zake ni za milele ingawa nimechelewa kuiona hii bado nina kanafasi cha uwakilishi hata kama sio Nec
Ndugu mpendwa Mungu awatie nguvu chochote mlichopanga kikafanikiwe ila safri ni ndefu sana sana na unaitaji divine intervation kwenye ndoa yako mungu akasimame nayo..kuna madada wametembea na huyo mtarajiwa na awajaolewa samhan yawezekana na wewe ulikuwa na umpendae ukamwacha zile zote ni roho na zinasema na pale zinapoongea ama kunungunika ma dear zina function.....sijui dini gan ila simama na Mungu sana sana ,Ndoa ni mpaka mwisho ...mnapokubaliana kuna kaka mmoja alihisi amelowa kanisan pale mkewe mtaraji alipokataa atoweza kuwa nae maisha yote na ndoa aikufungwa mpendwa..sio yeye ingawa baadae alijuta na kusema akujua alichosema lakini kwa Mungu imekula kwake daima...so hata wanaume nimefurah kama ajakuchezea bado maana kuna wengi wanaingia na gea za ndoa kumbe wanakufanya mpira wa kona kujaribishia siza za uume wao kwenye mwili wako na kukimbia mwisho unakuwa juza wa mapenzi........simama na Mungu sana sana zipo roho zinalia ulipotamka hili hadharani unaolewa na kwa kukusaidia jifunze kuwa msiri kwenye mafanikio yako sikukatazi kwa nini umetujuza la hasha akuna asiependa mafanikio yako vile vile sio wote wanaopenda uitwe MRS..

Kwenye baibo kuna mifano mingi tu ya watu waliotangaza baraka zako wakageuka watumwa Yussuf alioteshwa atakuwa waziri mkuu akaenda kwa ndugu na wazazi wake kumwambi mnajua mtakuwa chini yangu akuna aliekubali wala kumuelewa mwisho wa siku aliishia kuuzwa kabla ya kusudi la Mungu kutimia pengine asingesema ovyo wasingemtenda nduguze....jaribu kusoma neno la MUNGU sana kila wakati utaona mabo mengi katika ndoa ;ndoa si kipindi cha kibonde clouds unacheka siku imepita unasubiri kingine la hasha kuna mengi kwenye ndoa ntajaribu kukuttmia maandiko ya baibo kukusaidia hili

Yapo Mambo ya Kulaani na kukataa kabla ya ndoa yako

1)KUACHIKA AMA KUACHANA
Wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa na furaha ya ajabu lakini baada ya muda si mrefu wanaanza akufaraganyika na mwisho kuishi maisha ya ajabu amapo mmoja waoa anaona mwisho tangu mwanzo kwa kuamua kuacha kila kitu na kuanza maisha upya..nasema hivi sikutishi lakini si mpango wa Mungu kuachana ila kutokana na ufahamu wetu tunaishia kuachana...efe 4:6 Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...mwombe mungu akupe marifa ujue jinsi ya kuishi na mumeo utakaekuwa nae...Pili sasa hivi usikimbilie just ndan ya siku 30..nampa mtu moyo wangu hapanakuweka wazi

OMBA KUSUDI LA MUNGU KWENYE NDOA YAKO LITIMIE;;

USIONE UMEKAA NAE TANGU 2006 KUNA NDOA IMEVUNJWA WIKI 2 ZILIZOPITA WAMEKAA TANGU 1999 NIKIWA CHUO WAKAOANA MWAKA 2006....SO MUDA SIO TATIZO KABISA .MWAMBIE MUNGU AKUONYESHE KAMA ANAFAA KUWA NA WEEWE...INATAKIWA UMPATE MUME ATAKAEKUWA NA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKE;;UNAWEZA KUOMBA JUST MUME UKAPATA YOYOTE GAFLA AKAKWAMBIA NIMEKWAMBIA SITAKI KUSIKIA KWENDA KANISAN HATA SIKU MOJA;;UNARUDI KWA WAZAZI OOH HUYU KUMBE ALIKUWA SHETAN SHETAN WEWE ULIEMWINGIZA MYONI MWAKO NA KUMPA SIKU 30 ZA KUJIANDAA KUCHEZEA MOYO WAKO ...KWENYE BABIBO UTAONA KUSUDI LA NDOA NI FURAHA NA AMANI NA MUMTUKIE MUNGU;;MIMI NILITENDWA SANA KABLA YAA KUOA NA NIKAKUTANA NA MTU NIKAONA HUYU ANAFAA KUKLIKO WOTE DUNIAN BAADA YA MAMA WA YESU..NIKAMWOMBA MLOKOLE MMOJA ANIOMBEE ANYWAY KIPINDI HIKO SIKUWA NIMEOKOKA..NIKAMWOMBA BABA MWAKASEGE ANIOMBE AKANIPA MISTARII AKANI ALERT KWENYE MAOMBI KUNA MAWILI MI NAOMBA KUSUDI LA MUNGU NA SIOMBI JUST UOE OK??NIKAMWAMBIA SAWA MWISHO ALIONGEA NIKAUMIA AKASEMA KWENYE MAOMBI HAYA YAWEZEKANA UNA MWANAMKE UNAMWONA HUYO NDIE WAKO KAMA SI MAPENZI YA MUNGU ANAKWENDA KUPANGUA UHUSIANO NA HUTOKAA UMWONE MILELE..DUH..NIKAKAA WIKI NIKIJIULIZA NIMWAMBIE NINA HUU NIMEMPENDA AMA LAH...AKIWA MAOMBINI NDUGU USIMGUSE MUNGU MWEZI WA KWANZA WA PILI YULE BINTI AKAPATA VISA YA MAREKAN BILA HATA KUNJULISHA ANAONDOKA BAAYA YA WIKI AKANIFWATA HNY NAELEKEA USA SIJUI KAMA NTARUDI ILA NTAJARIBU TUANGALIE UJE SIWEZI BILA WEWE LAKINI MUNGU AKASEMA UTAWEZA UKIWA NA MIMI...NDUGU IKUMWONA TENA NIKAJA KUSOMA OPEN UNIV..NIKIWA NATOKA KWENYE MTIHAN NIKAWA NIMEPAKI NA BINTI PEMBEN GARI YAKE IMEARIBIKA AIWAKI NI MTUNDU WA MAGARI KIDOGO...NIKACHUKUA WAYA NIKAMWOMBA MTU ASHIKE UPANDE WA PILI NIKAWASHA GARI..UWEZI AMINI USIKU ULE AKAWA ANAFIKIRIA JINSI YA KWENDA KWAO KIPUNGUNI..NIKAMWAMBIA UTAENDESHA HII YANGU M NTAENDESHA YAKE MPAKA TUKAFIKA ..NIKIWA NJIAN ROHO WA MUNGU AKASEMA NIOMBE UPATANISHO NAE NA HUYO NDIE MKE WANGU MTARAJIWA NIKAWA NAJIONA KAMA CHIZI...NIAKAANZA KUSALI KWENYE ILE GARI MPAAKA NAFIKA NIKALILIA KUSUDI LA MUNGU...NIKAOMBA APPOINTMENT BAADA YA PAPER....NIKAJA KUKUTA NI BINTI AMEOKOKA ANAJIHESHIMU NA YEYE AKANIPA STORY ZAKE TUKAMLILIA MUNGU NA SASA NI MAMA WA MTOTO WANGU ,..SO KUNA MAMBO MENGI TU UNAKUMBANA NAYO UKITANGAZA NDOA MUNGU AKUREJESHHEE MUME WA UJANA WAKO

BE BLESSED!!!
 
https://www.jamiiforums.com/members/miss-judith.html 17th January 2011 01:


icon1.png
Hebu Sikieni Furaha Yangu


leo nimepata furaha kubwa sana. kuna mkaka mmoja aliwahi kuniapproach miaka ya nyuma akitaka kunichumbia na aliniambia ukweli kuwa alishadivorce na alipata mtoto mmoja kabla ya hiyo talaka. siku moja nikampa mtihani kuwa ampigie mtalaka wake simu mbele yangu amwambie kuwa licha ya talaka yao, anaomba wazae mtoto mmoja zaidi kwani hapendi kuwa na watoto na wanawake tofauti. alisita sana kwani alisema mtalaka wake ana maneno makali sana tena saa nyingine ya kashfa na angeweza kumtukana. baada ya kumhakikishia kuwa kama atamtukana nitamkubalia ombi lake palepale, alikubali.

alipompigia, mkewe alikuwa tofauti na alivyomtarajia. alicheka kwanza kwa mzaha, baadaye akamuuliza "leo una nini wewe, kitu gani kimekupata hadi unafikiria hivyo? natamani nikuone leo nijue kilichokupata!" walipokata simu alishangaa sana kwa maongezi yale, nilimwambia kuwa Mungu akishaunganisha watu huwa hawawezi kutengana, nikamwambia aendelee kumpigia simu kama hizo na amtafute ila akimkataa, tutakubaliana kuoana. sasa leo kanipigia simu anasema kuwa kakubali kuzaa naye! wow. God is at work! i am soooooo happy wapendwa.

jamani ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANDAMU ASIKITENGANISHE please!!!!!!!!!!!!!​




JUDITH...
Are you sure si huyu jamaa aliyekuwa anataka kunanihii mara ya kwanza?


haha, kaka PJ umeamua kuzama kwenye archive!

sio yeye na kwa taaraifa yako ni kuwa hivi sasa ninavyoandika hapa hao watu wameisharudiana na wanaishi nyumba moja na mama ni mjamzito

asante kwa kutukumbusha kisa hiki kizuri cha ushuhuda

ubarikiwe
 

Mshahara....Mshahara...mShahara...money ....money....money!..money-love!...gooooosh!

Mapenzi ya fedha na vitu haya!
Yaani hii michezo ya HELA ndio umeona mfano mzuri wa kueleza kwenye PUBLIC?...My hairs!
Nilitegemea kuwa ungesema anawaheshimu wazazi wako, au wakati mmojawapoa anaumwa mnatunzana, au the way mnavyobehave katika matatizo mengineyo ya social?

Sasa asingekuwa na kazi angekufurahisha na nini?....Wasanii wakubwa nyie NA hayo maigizo yenu ya payslip!
Acheni comediez za kwenye video hizo!...
Anywayz, hii ni script nzuri sana ambayo akiipata film-maker ataamka tajiri kama RIZ-1.
To my view, umebakiza siku 29 kuingia kwenye heart-break na heart-attack!

we hujachoka tu kupingana na maombi yangu?

haha, anyway ubarikiwe
 
we hujachoka tu kupingana na maombi yangu?

haha, anyway ubarikiwe
hapana Judith,
Sipingani na sala zako!
Nataka ujue jinsi iliyo bora ya kuomba!
Usiombe upate mume tu,..kumbuka kujiombea mwnyewe, maana kuna mambo ambayo ni lazima uyabadilishe kwako binafsi.la sivyo..utajilaumu!



African_American_Bride_and_Groom_Royalty_Free_Clipart_Picture_081101-215807-197050.jpg
 
dada lizzy nakushukuru sana.

naomba kuweka sawa hapo kwenye bold. kijana huyu ninayemzungumzia ndiye aliyenitaka na kuniomba tena wakati nikiwa mwanafunzi na bila hata kuwa na mbele wala nyuma ya maisha!, mimi kwa sababu ya ratiba ya maisha yangu sikuweza kumkubalia ombi lake kwa miaka hiyo na leo ratiba zangu zote zimekamilika na ndio maana nasema kwa sasa sioni sababu kwa nini tusiungane na kuwa mwili mmoja!

hatujawahi kukata mawasiliano wala kuyapunguza, baadhi ya ndugu na tafiki zangu wanamjua na pia baadhi ya ndugu na rafiki zake wananijua. so sisi ni marafiki wakubwa sana hadi sasa nitakachokifanya ni ku-confirm tu kuwa nimekubali ombi lake kama ambavyo wanawake wengi wanafanya kila siku.

itakuwa ni kupotosha ukweli ikionekana hapa kuwa nimeamua "kuvunja ukimya" baada ya kuona nazeeka bila ndoa japo sioni ubaya wowote kwa mwanamke kumomba mwanaume kufunga naye ndoa iwe ni kwa sababu ya kuzeeka au nyingine yoyote.

naamini nimeeleweka.

asante

ubarikiwe na Bwana.

mie shida yangu ni hapo unapopanga kila kitu wewe bila kumshirikisha mwenzio, unajuaje kama ukimshtukizia atakuwa tayari kwa namna yoyote ile kutimiza unachotaka? unaonaje ukae nae chini mapnge mipangilio yenu na kuafikiana kwanza kabla hujapatwa na butwaa?(nadhani ulokole umekufanya ucwajue wanaume vzr wewe)...na wadada humu ndani kauli ya "kuvunja ukimya" ckubaliani nayo kabisa, kesho na keshokutwa ndio unaambiwa wewe mwenyewe c ndio ulitaka ndoa mie nilikuwa na mipango na yuster...cjui labda na utandawazi huu, mwanaume atakaekuomba mwenyewe uchumba atakuheshimu/kuthamini, Judith yupo kama ameshachagua chagua weeee akaona hapana ngoja arudie awali, kwani kulikuwa na tatizo gani kumkubalia uchumba hata mlipokuwa skul? ingebadilisha nn kwako? mipangilio yako ingeenda kama ulivyopanga zaidi ingejulikana tu Judith ni mchumba wa mtu....nina mashaka kdog but GOODLUCK...karibu kwenye game.
 
Kuna kitu nakifikiria,
Hivi JUdy ikatokea ukaenda kumwambia sasa nimekubali ombi lako.
Akakuambia sawa mama, lakini mimi nilishaamua kuendelea mbele, nina mtu mwingine ninayempenda.
Utafanya nini?
 
Judith ....mwendo mdundo. Ng'ombe ushamla mzima atakushindaje mkia! Mwambie tu mwaya na kila kitu jipangie, sio mbaya kwa mwanamme kujibadili yeye kwaajili ya mwanamke mara moja moja hasa kwa mambo madogo madogo yasiyobadili kitu.

Besides ulishakuja na tungo hapa kuwa lazima mwaka huu (?) upate mume kwa hiyo ili hiyo 'lazima' itimie, wewe mpangie tu kila kitu. Akisua sua mwambie mahari utamsamehe (kwani hayamo kwenye Biblia anyway), na sherehe mtafanya siku za mbele huko mkipata pesa, muhimu ndani ya mwaka huu msaini makaratasi.

Kila la kheir na ndoa
 
Judith ....mwendo mdundo. Ng'ombe ushamla mzima atakushindaje mkia! Mwambie tu mwaya na kila kitu jipangie, sio mbaya kwa mwanamme kujibadili yeye kwaajili ya mwanamke mara moja moja hasa kwa mambo madogo madogo yasiyobadili kitu.

Besides ulishakuja na tungo hapa kuwa lazima mwaka huu (?) upate mume kwa hiyo ili hiyo 'lazima' itimie, wewe mpangie tu kila kitu. Akisua sua mwambie mahari utamsamehe (kwani hayamo kwenye Biblia anyway), na sherehe mtafanya siku za mbele huko mkipata pesa, muhimu ndani ya mwaka huu msaini makaratasi.

Kila la kheir na ndoa

We mdanganye mwenzio tu. Akija hapa kulialia usimkimbie.

Hujambo lakini rafiki?
 
Namwonea huruma sana mume mtarajiwa wa Miss Judy.

Kwa nini babu?
Mpe ushauri nasaha babu ili akapate kuwa mke mwema.
Ni kweli Judy, anahitaji kitu fulani kijengeke ndani yake.

Sijui kama yeye mwenyewe ananiliona hilo, lakini ingefaa mkafungua visima vyenu vya hekima wakati huu babu.
Ili walau, ajitambue, au aelewe vizuri, kile tunacho maanisha.
 
Kuna kitu nakifikiria,
Hivi JUdy ikatokea ukaenda kumwambia sasa nimekubali ombi lako.
Akakuambia sawa mama, lakini mimi nilishaamua kuendelea mbele, nina mtu mwingine ninayempenda.
Utafanya nini?

kuna mengi sana kwenye hii post ya Judy, kuna mapungufu/anatakiwa arekebishe mambo kibao, nimeshindwa hata kumuelewa kwa kweli lakini sote binadamu hatujui Mungu kampangia nn.
 
We mdanganye mwenzio tu. Akija hapa kulialia usimkimbie.

Hujambo lakini rafiki?

Aaah hii dhamira kaianza zamani, unafikiri itabadilishwa na mie na wewe leo hii? (japo Judy alisema hana mtu wala hajampata kipindi kile ....kumbe holla yupo miaka mitano!).

Besides naamini mtu kama Judith hawezi kuja hapa kulalamika :D

Sijambo habari za siku nyingi mno .........tumesalimika humu ndani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom