Siku 3 Mahabusu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
234
MIEZI 4 KABLA

Siku hiyo nimekaa zangu katika internet café , kwa shuguli zangu za kawaida tu , na kwa kawaida napenda kwenda internet café siku za weekend ila niangalie zinavyofanya kazi yaani watu wanafanya nini haswa wanapokaa katika hizo computer , na kisha kukusanya taarifa hizi kwa ajili ya tafiti zangu zingine .

Hapo café nilipokaa , mtu mmoja akaja na laptop akanipitishia akasema laptop hiyo inauzwa , sikuwa nataka laptop wala nini lakini nikaanza kumdadisi kwa kumuuliza maswali laptop hiyo ni ya nani imepatikana wapi na kama na risiti za laptop hiyo na kwanini ameamua kuisambaza mitaani na asiende kutangaza katika classified za magazeti au tovuti maalumu kama advertising dar au vipeperushi maaalumu ?

Baadaye huyu jamaa akanipa jina lake pamoja na email ili niwasiliane nae kama nikitaka hiyo laptop , zikapita siku 3 hivi , mara nikaona tangazo katika jukwa Fulani mtandaoni dada anasema laptop yake imeibiwa , cha kufanya mimi nikawasiliana na yule dada kumuuliza zaidi na tukaonana nae .nikampa majina na anuani za mtu mwenye laptop ile ili waendelee kuwasiliana .

Tangia wakati huo sikuwasiliana tena na huyu dada ambaye amepoteza laptop yake maeneo ya millennium towers .

BAADA YA MIEZI 4

Wakati huo nilikuwa niko kijitonyama kuna shuguli ninafanya , nikapokea simu kutoka kwa mtu mmoja aliyejitambulisha kama J , akawa anataka nimtafutie laptop , nilipomuuliza amepata namba yangu wapi akasema ametoa toka kwa rafiki yangu mmoja hivi hakutaja jina .

Mara ya kwanza aliniomba nionane nae mchana huo pale Mayfair plaza , lakini nikashindwa kwenda kutokana na kutingwa na kazi , kwahiyo shuguli nzima tukakubaliana kesho yake jioni .

Jioni hiyo ndio ilikuwa siku ya jumatatu akaniambie yuko Corner Bar , sinza , kufika pale akabadilisha akasema yuko katika gari moja dogo ambalo lilikuwa limeegeshwa katika kituo cha kujazia mafuta hapo afrika sana .

Nikafika tukaonana na kukubaliana bei , kwahiyo sasa tukawa tunatoka kwenda kuchukuwa pesa , kufika mbele kidogo mara akaloki milango na akaniambia yeye ni polisi kuanzia saa hiyo niko chini ya ulinzi mpaka nitakapofika kituoni .

Usiku huo huo tukaenda mpaka kule ninakoishi na wenzake wakachukuwa laptop ninazotumia kwa kazi zangu nyingine na ambazo huwa nazitegemea sana kwa uhifadhi wa habari na mambo mengine , lakini ninashukuru huwa ninakopy 3 za vitu vinavyofanya , moja iko kazini , nyingine kule nyumbani kwa wazazi na nyingine huwa natembea nayo katika dvd kwahiyo chochote kikitokea ni ngumu kupoteza kazi , walipochukuwa hivyo vitu tukaanza kwenda polisi .

Kufika kituoni akanifunga pingu na nikaenda nae kuongea nae katika chumba maalumu , akaanza kuniuliza kuhusu laptop nyingi sana zilizopotea , watu wanaouza na kadhalika , tukatoka pale kwenda nyumba moja ya wageni ambapo kulikuwa na laptop nyingine nyingi tu niziwashe na kuona zipi zinafanya kazi na ambazo mbovu nikawasha na kumwonyesha zilizokuwa mbovu kisha tukarudi pale kituoni .

Tulipofika hapo kituoni huyu askari akaniambia nikiulizwa na maasikari wengine nimekuja kwanini pale niseme nimeiba simu nisiseme kwamba nimeletwa kwa masuala ya laptop kwasababu ni dili lake haliwahusu polisi wengine .

Baadaye kabla sijapelekwa rumande ndio akaniambia kuhusu huyu dada ambaye miezi 4 iliyopita nilimsaidia kumwonyesha watu waliokuwa na laptop yake na akanieleza bayana natakiwa niwaonyeshe hao watu , sikuweza kusema chochote kwa sababu huyu dada alikuwa anawasiliana na watuhumiwa wake mpaka yule dada mwenyewe aje kusema wamefikia wapi .
Mpaka hapo simu yangu ilikuwa imezimwa , sikuruhusiwa kuwasiliana na mtu wowote wa nje , ndugu jamaa na marafiki wala jamaa wa kazini kwangu nikaingizwa mahabusu kwenda kuketi mule ndani .

Kabda ya kuingizwa niliandikiwa vitu nilivyoacha pale mapokezi ya polisi , kwanza wakaandika pesa kidogo wakati mfukoni nilikuwa na pesa nyingi zaidi , pia hawakuandika kuhusu laptop nyingine ambazo ilikuwa katika gari ile ya polisi , hawakuandika vifaa vyangu vingine vya kazi ambavyo vilikuwa navyo katika gari hiyo ya polisi .

Nilipolalamika na kuuliza yule polisi alinilazimisha nichukuwe hiyo karatasi kama ilivyo niliendelea kukataa kuchukuwa ile karatasi bila orodha ya vitu vingine mara polisi akalazimisha kuingiza mfukoni mwangu halafu akachana shati yangu akanisukuma akataka kupigana na mimi .

Akanisukumia katika chumba Fulani hivi ili aanze kunipiga , nikamweleza kwamba hata akinipiga mimi nataka aandike vitu nilivyokuja navyo na kusaini hiyo karatasi asipofanya hivyo sikubali kwa lolote lile .

Mara mkuu wa kituo akafika na kuuliza nini kinachoendelea nikamweleza ndio yule askari akaamua kuandika vile vitu na kwenda kunitafutia shati lingine nivae na ndio nikakubali kwenda mahabusu lakini kwa shingo upande tu .

NDANI YA MAHABUSU

Tofauti na watu wengi wanavyofikiri mahabusu wanajazwa watu wote , hapana inategemea kama kituo nilichokuwa mimi mahabusu niliyowekwa mimi ilikuwa safi na nzuri kidogo sema haikuwa na kitanda lakini mambo mengine yote yalitia moyo kidogo lakini kukawa kuna vyumba vingine vya mahabusu ambako watu wanajisaidia na kulala humo humo .

Ndani ya chumba hicho nilikutana na baadhi ya watu kadhaa , mfano mmoja ni kijana ambaye ni raia wa Uganda anayeishi manzese , yeye alienda mlimani city akiwa na mastercard ambayo iliporwa kwa mtu siku za nyuma , alipofika pale alinunua vitu vya dhamani ya laki 8 na kutumia hiyo mastercard kama malipo lakini mwenye kadi hiyo alikuwa amesha ripoti kwa wahusika kwahiyo wakaiblock , pale dukani ikishindwa kufanya kazi .

Wakamchukuwa mpaka katika ATM , kijana akaambiwa aingize namba za siri akashindwa ndio wakamkamata na kumleta polisi , lakini muda mfupi baadaye yaani usiku huo huo jamaa zake walikuja kumtoa kwa dhamana , fikiria huyu ni raia wa kigeni amekuja bongo kufanya uhalifu ameshatoa kitu kidogo ameachiwa yuko mitaani anadunda .

Kuna wazee wengine 2 hawa wazee waliuza kiwanja cha mtu kwa mil 40 bila idhini ya mwenye kiwanja , aliyenunua akaamua kuja kuwashitaki hawa wazee na kuwakamata sasa walikuwa ndani mule mahabusu kwa muda wa siku 3 hivi , na walikuwa wanapata huduma zote za kuongea na ndugu zao na jamaa zao wengine .

Usiku huo mmoja wa wazee aliongea na polisi ambaye anashugulikia kesi yake , yule polisi akamwambia akienda mahakamani akubali makosa , halafu atoke kwa dhamana awe anamlipa yule aluenunua kiwanja pesa kidogo kidogo kwanza aanze kumpa mil 5 mwezi ujao amlipe mil 5 tena .

Na walipofika mahakamani ikawa hivyo hivyo jamaa aliyeuziwa kiwanja amabadilishiwa kibao , sasa imekuwa kesi ya madai na sio kesi ya utapeli tena wale wazee waliouza kiwanja wako nje wanapeta tu kwa raha zao na polisi yule nae amepata kitu kidogo kwahiyo hana wasi wasi hata kidogo .

Iliyotia fora zaidi ni ya kijana mwingine , ambaye alipewa vitu na rafiki yake akauze , kumbe walikuwa wanafuatiliwa na polisi mpaka walipouza hiyo mali na polisi wakajua walipouza hiyo mali lakini wakasita kuwakamata wakati wanafanya mauzo badala yake wakaanza kuwafuata majumbani mwao

Wakawakamata na kuwaleta pale mahabusu , polisi wakamwambia yule kijana waende nae kariakoo na wachague muhindi wowote yule mwenye pesa zake wambambiko hiyo kesi kwahiyo kijana amelazimishwa kumtaja mtu mwingine katika kesi hiyo kwa faida za polisi

Duru za uchunguzi zinasema kwamba polisi wale wakifika pale wanachukuwa vitu vyote kutoka katika duka hilo na vitakuja kutolewa kwa dhamana maalumu na pesa maalumu ambayo ni nje ya sheria kwahiyo kijana yule atakuwa huru .

SIKU YA PILI

Asubuhi ikafika polisi akaja kunichukuwa akaniambia nimpeleke kule niliponunua hiyo laptop na kwa watu ambao nimewahi kuwauzia , nikampeleka kwa wakwanza ambaye alinipa hiyo laptop wakamkamata na wakachukuwa siku yake kama akitaka kuwasiliana pale aweke loud speaker .

Yule jamaa akaletwa kituoni kisha tukaenda kwa mtu mwingine ambaye aliwahi kununua laptop toka kwangu yule nae akaja polisi na ile laptop , huyu polisi akawa analilazimisha mimi nimnganganie yule jamaa niliyemuuliza laptop akaniambia kwamba anataka hela kutoka kwa yule jamaa kwahiyo nisijaribu kumtetea .

Mpaka muda huo yule dada aliyelalamika kuhusu laptop yake hajaonekana na polisi hataki kuwasiliana nae ili naye aje pale na hata hivyo laptop tulizokuwa nazo sisi hazifanani hata kidogo na yake na hizi zilikuwa mpya kabisa hazijawahi kutumika sehemu yoyote .

Sasa jamaa niliyemuuliza laptop alipofika kituo akaambiwa ile laptop ni ya wizi aonyeshe risiti za laptop au visibitisho vyote kusema kama kweli ile laptop ni yake , sasa aliyekuwa na hiyo risiti hakwepo ndio atakuja jumatatu

Lakini laptop yangu risiti yake ililetwa na ndugu wa jamaa wa kwanza ambaye alinipa ile laptop nimsaidie kuuza , polisi bado akazidi kusema kwamba yeye anataka apatiwe na laki 2 zingine mpaka jumatatu ambako mambo yataendelea .

Ndio hiyo siku ya alhamisi asubuhi wale jamaa wakaja na risiti ya laptop moja pamoja na laki 2 , wakamwonyesha polisi , lakini ukweli ni kwamba ile risiti sio ya ile laptop , pia wakaja na pistol moja wakamwomba polisi awasaidie kuionsha .

Na ndio ilikuwa hiyo tukatoka asubuhi hiyo kwenda majumbani mwetu , mimi sikuweza kwenda nyumbani moja kwa moja kwanza nilitakiwa kwenda mjini kuongea na jamaa zangu wengine na kuandika sms kwa jamaa zangu wengine kuwaeleza kilichokuwa kinaendelea .

Leo asubuhi nafika hapa kazini nakutana na rafiki yangu mmoja ananiambia kwamba yule polisi ndio tabia yake hiyo , huwa anatafuta namba za watu wanaotengeneza laptop kama sisi halafu anakubambika kesi hata na yeye amewahi kubambikwa kesi na huyu polisi nilipoambiwa hiyo nikasema kweli kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake

SIKU YA IJUMAA

Niliamka asubuhi nikatakiwa kuwahi kwenda polisi , kufika pale kabla sijafika polisi akanipigia simu akaniomba nikaonane nae nyumba moja ya wageni , nikafika pale nyumba ya wageni , kufika pale akanionyesha laptop zingine zilizokamatwa lakini ambazo wenye nazo wamekimbia au kuziacha pale na zingine sijui wamezitoa wapi nikaziona na kumuonyesha ambazo ni nzima ili aweze kuziuza .

Ilikuwa maajabu sana kwanini polisi kama yule analala nyumba za wageni na vitu vya watu anaviweka nyumba za wageni kama mimi mali zangu aliziweka katika nyumba za wageni kwa dhamana ya nani ?

Muda kidogo polisi akaniambia nimwambie madili zaidi ya laptop pamoja na namba za watu wanaouza laptop mjini ili aweze kuwakamata ale pesa zao kwahilo sikuwa na maelezo yoyote hapo kabla nilishawaambia watu wangu wa karibu kuhusu huyu jamaa na mamba zake za simu ninazo .


SASA NIKO HURU

Lakini muda bado upo wa maongezi na muda wa kuendelea kumchunguza zaidi na nitatafuta njia nzuri na rahisi zaidi kuweza kumnasa huyu polisi kutokana na tabia yake hiii .

Mpaka sasa hivi ninavyomaliza kuandika email hii fupi , dada aliyepeleka kesi polisi hataki kupokea simu yake , ni kaka yake anayepokea simu anasema huyu dada amesafiri , sasa najiuliza kwanini anaanzisha vitu halafu anashindwa kuja mbele ya umaah kujitetea na kutoa maelezo ya ziada

Hapo chini kuna mfano wa email ambazo aliniandikia huyu dada jana mchana tafadhali soma halafu utafakari

Habari kaka
Mimi nashukuru kwa yote na bidii zako,lakini mimi ningefurahi sana jkama hata ungalinionyesha huyo M,kwasababu Mimi nilishawaambia kuwa naitaka na nitarudisha pesa,lakini naona mambo yanavyoenda hata sielewi kabisa,mpira unarushwa rushwa kama danadana.Any way.Kama you still need to help me ,I would really appreciate.Huyo amekuyeyusha I am hundres percent haijaibiwa na bado anayo kwani mimi ninaenda mara kwa mara pale sijasikia habari za kuibiwa tena kwa hiyo Lap top.

Samahani naomba nikuulize swali,Je huyo wamjua?Kama wamjua kwanini usinipeleke nionane nae nimuombe aniuzie ile laptop yangu tena.Mimi sitaki kuzunguka zunguka hata kama wameiuza dola 1200 ,mwambie mimi nitamrudishia sababu kuna kazi zangu nyingi mule kaka na ninaipenda sana ile laptop,maana hapa Tz hakuna zile latop .Sasa naona ni danadana tu,Please help me ,I will also help you,hii ni njia ya kujenga undugu kati yangu mimi na wewe na hata familia yangu.Please nakuomba unisaidia ,please ,please.Nilikuwa nikijaribu sana kumtafuta ,lakini hayupo mtu wa namna hiyo pale millenium tower .Hata huyo M wanasema hawamjui sasa mimi kama msichana inianiwia vigumu,chas msingi wewe nisaidie mimi,Nakuomba,Chonde chonde kaka yangu

Nakutakia weekend njema
 
...tumia akili kumkomesha huyo polisi na ikibidi kaongee na mkubwa wake wa kazi na umweleze uliyoeleza hapa nafikiri anaweza kufanya kitu cha maana kukomesha hiyo tabia
 
.....kijana ambaye ni raia wa Uganda anayeishi manzese , yeye alienda mlimani city akiwa na mastercard ambayo iliporwa kwa mtu siku za nyuma , alipofika pale alinunua vitu vya dhamani ya laki 8 na kutumia hiyo mastercard kama malipo lakini mwenye kadi hiyo alikuwa amesha ripoti kwa wahusika kwahiyo wakaiblock , pale dukani ikishindwa kufanya kazi....

Hivi nyumbani hakuna system ya kuomba Id kwa wanaotumia credit/debit card ku-validate identity?
 
Hivi nyumbani hakuna system ya kuomba Id kwa wanaotumia credit/debit card ku-validate identity?

QM,
sidhani kama wana hako kautamaduni........lakini pia kama umesaini nyuma na unasema ni debit huitaji ID, ila kama unasema credit na mara mingi kama hujasaini nyuma ya card hapo ndio lazima uwe na ID.
Pia kama unaweza kuchonga ID "kanjanja" huku "unyamwezini" basi bongo nadhani hiyo ni kama kuendesha baiskeli kwenye mteremko.
Bongo papo complicated sana yaani....................mie sijui kama nitaweza tena!!!.
 
Ndio maana nasema mlioko Majuu kaeni hukohuko, huku bongo nuksi. Pole sana Bw shy!
 
Wewe sijui nikuite jina gani ambalo litarandana na hii hadithi yako, Polish ya sasa hivi haiko hivyo unavyoihadithia, sidhani kama kuna askari Polish anayeweza kufanya upuuzi huu, isitoshe ulishindwa kulalamika hapo kituoni kwa wakubwa zake, pia kama unauchungu na huko ulichofanyiwa kwa nini usiweke hapa jina la huko kituo na hiyo askari wako anayeishi guesthouse.
 
Hii stor ya huyu jamaa nmeisoma hafu nikashangaa nashtuka kumbe ni story ya 2007 ..... Sishangai kwa kipindi hicho.

Kulikua na #manipulations nyingi sana kwenye vyombo vya usalama kipindi hicho.

Now after 13 yrs mambo kdg yamechange
 
Mbona yupo online?
Screenshot_20200723-215027.jpg
 
Back
Top Bottom