Siku 21 za Ngeleja: Taifa linaelekea gizani rasmi

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Siku 21 za Ngeleja: Taifa linaelekea Gizani Rasmi

Nashtushwa sana na mbinu za serikali kuendelea kulifanya suala la upatikanaji wa Nishati ya Uhakika ya Umeme kuwa la kisiasa zaidi kuliko kupata ufumbuzi wa kdumu na kuwaeleza watanzania nafasi yake na uwezo tulionao katika kushughulikia tatizo hili.

Tunaendelea kukwama kwa kasi ya ajabu kwa kuendelea kutegemea kudra ya Mungu kuendesha Nchi, huku kasi ya maovu nayo ikishamiri. Kwa mtaji huu wa maovu mengi kuliko mema kudra za Muunba zinatoka wapi kwa kizazi kilichomuasi? Huu ni mchezo wa kuigiza na ndotoza alinacha kuukwaa utajiri kwa mauzo ya kapu la vioo.

Serikali inasisitiza kuwa haitasimamisha uzalishaji wa Umeme katika bwawa la Mtera kama ilivyofanya mwaka 2006, haya yanazungumzwa huku kiwango cha chini cha uzalishaji umeme katika bwawa hilo kinapigania roho kwa poniti zaidi ya 90 zilizosalia katika uwezo wake wa juu wa 698.50 mpaka kiwango cha chini cha 690 na ujazo wa hivi karibuni ni mita za ujazo 690.74.

Vyanzo vyetu vingine ambavyo vinazalisha umeme vyote vipo taaban na vinafanya kazi chini ya kiwango na katika hatua zake za lala salama kabla ya kusitisha shughuli zake kutokana na kutokuwa na maji ya kutosha na hii ni kwa kiwango cha karibu zaidi ya asilimia 100 chini ya kiwango cha kawaida

Kihansi kwa sasa ni MW 90 badala ya MW 180, Kidatu MW 40 badala ya 204, New Pangani MW 20 badala ya MW168 na Nyumba ya Mungu ni MW3.5 badala ya MW 8.

Mamlaka ya Hali ya hewa haijatabiri kuwepo na Mvua katika chanzo chochote kati ya vyanzo vinavyokusanya maji kuelekea mabwawa haya si Ruaha Mkubwa wala Ruaha Mdogo na Kisigo wakati ambavyo hukusanya maji mengi kwa ajili ya bwawa la Mtera wakti wa kipindi cha masika.

Sipati picha kwa kasi hii ya ongezeko la ukame ambao unashamiri tuna miujiza gani ya kupata nishati ya uhakika na ambayo haitakuwa inaelekea kukoma kabisa ndani ya siku 21 za Waziri Ngeleja alizopewa kusahihisha mapungufu yake katika Bajeti ya Nishati na Madini.

Nashawishika kabisa kuamini kuwa baada ya kipindi si kirefu tunaelekea gizani jumla kama taifa hakuna cha mgawo wala jenereta kutoka vituo vya TANESCO kanda ambayo mengi kati ya hayo yamesimama muda mrefu kutokana na hitilafu za kiufundi na kukosekana kwa vipuri vya kuyakarabati.

Tunaomba Neema za Muumba Mvua zinyeshe katika vyanzo hivi Taifa lisifike huko, maana kama tutafika huko. Mimi na wewe hatujui nini hasa itakuwa hatima ya Taifa letu.

ADIOS
 
mvua za vuli unazoongelea wewe kwa kawaida huwa ni mwezi wa tisa. Ni lazima tuwe gizani li watanzania tuzinduke toka kwenye dimbwi hili la kutokubali mabadiliko.

waziri mkuu kasema anakuja na mkakati wa serikali, sisi wenye akili tunajua kama wameshindwa kuja na mikakati miaka zaidi ya 4 iliyopita, hii wiki tatu watakuja na nini? endelea kuishi kwa matumaini yasiyokuwepo eee Mtanzania usiyekuwa na hatia.
 
Sijui atakuja na Mkakati gani?
 
Misimu ya mvua Tanzania inajulikana na hili halihitaji mjadala sana. Tanesco, Wizara na watu wote wanajua kuwa Tanzania kuna misimu miwili tu ya mvua. Vuli (kwa maeneo yanayopata mvua za za vuli) ambayo huwa ni October to December. Masika huwa ni March hadi May/June. Maeneo yale yenye mvua nyingi hupata mvua October/November continuusly hadi May/June. Julai hadi October katika eneo lote la nchi ni miezi ya kiangazi na hatutarajii mvua.

Suala la kuangalia vyanzo vya maji na mamlaka ya hali ya hewa kutoa utabiri wa mvua huwa ni wakati wa Masika .... si Kiangazi kama sasa. Kwa hiyo ikiwa mvua zilinyesha kidogo wakati wa msimu wa mvua, haziwezi kunyesha wakati wa kiangazi, tusubiri Mwakani; yaani msimu ujao wa mvua kuanzia mwezi October/November. Huwezi kuzungumzia mvua Tanzania hii katikati ya Juni na October, haipo!

Mgawo wa umeme nchi hii hausababishwi na ukosefu wa mvua au ukame kama alivyonukuliwa mheshimiwa rais akiwa huko South Africa. Mgawo wa umeme unasababishwa na uozo uliopo ndani ya Tanesco/Serikali. Uozo huo hauwezi kumalizwa na mvua! Hata kama mvua zikinyesha mwaka mzima umeme hautakuwepo kwa sababu mifumo yote ya uendeshaji wa nchi imevurugika na kazi hazifanyiki vile inavyotakiwa. Mvua zikinyesha sana mgawo utakuja tu tutaambiwa mitambo ni ya zamani na imechoka. Umesahau mwaka jana ulikuja mgawo kipindi ambacho mabwawa yalikuwa yamejaa maji na tukaambiwa sababu ni kuharibika kwa mashine za kuzalisha umeme wa Gesi pale ubungo?

Unaweza kuficha udhaifu, huwezi kuficha matokeo ya udhaifu wako. Serikali inaweza kuficha ukweli kuwa rushwa na ufisadi vimesambaratisha mfumo wa utendaji kazi serikalini; lakini serikali haiwezi kuficha matokeo ya Rushwa na ufisadi serikalini.

Matatizo ya umeme nchi hii yalianza siku ile tuliposema tuwape wengine kazi ya kuzalisha umeme kwani sisi tumeshindwa! Mwanaume mzembe na mpumbavu kabisa ni yule anayeweza kusema kuwa "mke wangu kanishinda, nampa rafiki yangu amlee; ila nataka niendelee kupata haki yangu kama mme". Watanzania tulikubali kuwa Mambo makubwa hatuyawezi, tukasema ni lazima tuwape wengine kazi ya kutuzalishia umeme. Lakini wakati huo huo tukasema tunataka umeme ambao tunaweza kuudhibiti gharama zake!

Toka ilipoingia kampuni ya IPTL, ikiwa ndo mara ya kwanza kwa serikali kutangaza kuwa inawapa independent power suppliers; kilichofuata imekuwa ni mfululizo wa habari za kutisha za vitendo vya ufisadi na rushwa kwenye sekta ya umeme. Wazalishaji binafsi wa umeme hawaji kutulelea wake zetu ili wake zetu wanawiri na wapendeze halafu watuhudumie sisi. Wazalishaji binafsi wanakubali tu kubeba jukumu la kutuzalishia umeme, pale tutakapowahakikishia faida kubwa isiyo na mgogoro (risk free profits). Na kwa hiyo walikuja na masharti kibao pamoja na bei zisizolipika nyingine zikiwa ni za kulipia hata kama hawazalishi (capacity charges).

Hayo ndo matokeo ya kutaka mtelemko wa kuzalishiwa umeme bila kutoa jasho la kuvisumbua vichwa vyetu kufikiri. Wazalishaji binafsi wanataka faida kubwa na kwa muda mfupi iwezekanavyo! Sisi tukalalama bei zao kubwa, .... ebo nini kimetushinda sisi kuzalisha umeme ikiwa inawezekana kuzalisha kwa gharama nafuu? Kwa hiyo toka kuingia kwa wazalishaji binafsi, mapato yote ya Tanesco yanaishia kwao! Tanesco imebaki ni jibwa kubwa lisilo na meno. Sasa kazi yao ni kukusanya fedha na kuwapa wazalishaji umeme binafsi.

Tukitaka umeme wa uhakika, tufanye mapinduzi. Tuiondoe serikali iliyoko madarakani. Serikali itakayokuja tuiambie kuwa haimalizi miaka mitano kama haitupi umeme wa uhakika. Vinginevyo itakuwa hadithi ni zile zile miaka nenda, rudi.
 
Nakubaliana na Mawazo yako Mkuu. Tatizo hapa tumefikishwa kuamini dhahiri kuwa hakuna chanzo cha Nishati Nchini zaidi ya HYDRO-ELECTRIC Power, Gas imebaki kuwa hadith na makaa ya mawe ni simulizi jingine jipya.

Katika mpango wa sera ya CCM ya Mwaka 1981 umeme wa Upepo unatajwa kama moja ya njia mbadala za mpango wa muda mrefu wa kuwezesha upatikanaji wa Nishati ya Uhakika ya Umeme Nchini, lakini ni miaka mingapi tokea Mwaka 1981?

Utakuwa mpango wa muda mrefu uliopitiliza kwa maneno mengine. Kwa nadharia hii ya kutegemea Mvua kama hakuna maarifa mengine tumeingia gizani jumla.
 
Taarifa si za kuridhisha sana kutoka vyanzo vya uzalishaji wa Nishati ya Nguvu za maporomoko ya Maji. Mabwawa yote tajwa hapo juu yanendesha shughuli zake kwa nukta chache tu chini ya Kiwango.

Wasimaizi katika mabwawa haya wanahesabu tu siki kadhaa kabla ya kuamua kuzima mitambo rasmi kutokana na kiwango cha Maji kushuka kupita kiasi katika vyanzo hivi.

Hii inamaanisha Ndoto hii ambayo ni mbaya kabisa huenda ikatimia, Na tunamuomba Mungu alinusuru Taifa tusifike huko, Licha ya Taarifa hizi za awali zinatoa hadhari kubwa kuwa kama una mradi wako ambao umeme ni nyenzo Muhimu hakikisha Generator yako inafanya kazi mapema.

TANESCO wametangaza sasa kutokuwa na Ratiba ya Mago tena, maana haitekelezeki nafasi ikipatikana wanauwasha katika maeneo kulingana na Umuhimu.

Taifa linanyemelea Gizani sasa.
 
udhibiti wa maji yanayoingia na kutoka kwenye haya mabwawa ukoje nafikiri hapa ndiyo kwenye tatizo la msingi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Napenda kabisaaa ili akose full umeme hata 1.5V wa betry... tumekuwa wazembe mno tunaishia kusema sema tu bila action!
 
udhibiti wa maji yanayoingia na kutoka kwenye haya mabwawa ukoje nafikiri hapa ndiyo kwenye tatizo la msingi.

Pia kiwango cha Tope ni kwa kiasi gani maana fedha za kuondosha tope huwa zinaongeza tope katika matumbo ya watu mara kadhaa kwa hiyo hata kina kushuka kama mvua zimesimama katika msimu huwa ni jambo la muda mfupi tu.

Hapa ipo namna kwa watendaji katika Gridi ya Taifa
 
Wadau kiukweli kama taifa hatua tunayoiendea ni mbaya kuliko hata tunavyofikiria,na hili halikwepeki kutokana na hali halisi iliyopo hakuna mvua na wala sio leo kuzipata mvua za kuweza kujaza mabwawa yetu. Hivyo tunaelekea gizani.
Na Tanesco wako hivi walivyo kwasababu wakubwa wanataka wawe hivi ili kuweza kutimiza ya kwao maana ukisikiliza watu walioko Tanesco ndani ndio utajua vizuri ni kwanini umeme haupatikani,siasa za nchi yetu zinazidi kutupeleka kubaya kama nchi na tukufika huko itatuchukua muda gani kutoka??!!
Tuombe Mungu atusaidie sana maana hali hii si njema kabisa!
 
Narudia tena,serikali inayoendesha mambo yake kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa karne hii ya 21,imekosa uhalali wa kuendelea kuwepo!
 
Wamefanikiwa kutuaminisha kuwa source pekee ya Umeme ni Hydro Electric Power!!!!
 
Pia kiwango cha Tope ni kwa kiasi gani maana fedha za kuondosha tope huwa zinaongeza tope katika matumbo ya watu mara kadhaa kwa hiyo hata kina kushuka kama mvua zimesimama katika msimu huwa ni jambo la muda mfupi tu.

Hapa ipo namna kwa watendaji katika Gridi ya Taifa

GR hili swala la tope kwa nini tanesco hawalisemi wakati ndio chanzo kikuu cha uhaba wa maji. Mimi sidhani kama serekali ilikubali kujenga mradi mkubwa kama wa kidatu na kihansi chenye uwezo wa kuhifadhi maji kwa miezi mitatu tu. Maana mvua za masika zimeisha mwezi june sasa mwishoni mwa july tunadai maji yamepungua hivi kweli inaingia akilini? Matope yasipotolewa mgao utakuwa ni wa kudumu !
 
tatazo ni nani wa kumfunga paka kengele?, wenzetu Namibia walilianzisha kwa sababu hii hii ya umeme. Malawi wamechoka hawana muda wameingia street. muda utatufundisha tu jinsi ya kuhangaika na serikali zisizo sikivu kama hii.
 
Very sad kuwa na sirikali mbovu namna hii, ila ni mbaya zaidi kuwa na wananchi wapole hata kwa mambo ya msingi.
 
Mimi naipenda sana hali hii ya giza tororo, watanzania ni vyema tukateseka sana tena sana mpaka pale tutakapoona haja ya kuamka katika usingizi huu wa kudanganywa na hawa wapuuzi, mara ooh, subirini, ooh, mradi unakuja etc. upupu tuu. Ngoja tuumie kwanza ndo tutajua umuhimu wa kuiondoa CCM madarakani
 
Mkuu..kuhusu tope nilibahatika kuonge na mtaalam mmoja pale Mtera akanieleza kwamba kutokana lilivyojengwa tope kuingia ni baada ya about 20 yrs. morever mtera haikukusudiwa kuwa power plant ila reserve ya stigle. ilikuwa lisupply stigle wakati wa situations kama hizi za ukame. Pesa ziliandaliwa, ground work ilifanyika makabrasha yapo ......vipi mambo yalibadilika i don't know
 
Wamefanikiwa kutuaminisha kuwa source pekee ya Umeme ni Hydro Electric Power!!!!

Hapana, wamefanikiwa kutufanya tufikirie kuwa Hydro Power ni mbaya. Hydro power ndiyo the best kwa Tanzania ukizingatia kuwa sis ni nchi pekee duniani iliyozungukwa na maji bila ya kuwa kisiwa. Tanzania ina mito mikubwa mingi kuliko nchi yeyote Africa isipokuwa Congo.

Tatizo ni kuwa tumelazimishwa kufikiri kuwa Hydro Power = Mtera and Kidatu. Hii ni miradi midogo sana. Tunachohitaji ni mradi wa Steigler's Gorge (4,000MW) na Malagarasi.

Hii miradi ya gesi, mafuta n.k. ni miradi midogo midogo sana na ina mianya mingi ya ufujaji.
 
GR hili swala la tope kwa nini tanesco hawalisemi wakati ndio chanzo kikuu cha uhaba wa maji. Mimi sidhani kama serekali ilikubali kujenga mradi mkubwa kama wa kidatu na kihansi chenye uwezo wa kuhifadhi maji kwa miezi mitatu tu. Maana mvua za masika zimeisha mwezi june sasa mwishoni mwa july tunadai maji yamepungua hivi kweli inaingia akilini? Matope yasipotolewa mgao utakuwa ni wa kudumu !

Hapa ndio ile hadith ya Ukinikanyaga tu......
 
Napenda kabisaaa ili akose full umeme hata 1.5V wa betry... tumekuwa wazembe mno tunaishia kusema sema tu bila action!

Hii watoto wa town wanasema ndio mkome na wewe unajijumlisha humo humo, Ila imetulia teh teh teh
 
Back
Top Bottom