Siku 21 Za Mafanikio Mwaka 2015, Usikose Nafasi Hii Muhimu Ya Kuboresha Maisha Yako

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Mwaka 2014 ndio unaisha hivi, najua kama ungekuwa na uwezo wa kusimamisha muda usiende ungefanya hivyo ili uweze kukamilisha baadhi ya mambo uliyopanga kukamilisha mwaka huu 2014. Lakini hakuna mtu mwenye uwezo huo wa kusimamisha muda, tupende tusipende muda utaendelea kwenda kama unavyokwenda.

Hii ina maana kwamba tatizo lolote ambalo tunalipata kutokana na kukosa muda sio kwa sababu ya upungufu wa muda ila ni kwa sababu ya matumizi yetu mabaya ya muda. Katika muda huu huu wa masaa 24 kwa siku kuna ambao wanafanya mambo makubwa sana na pia kuna ambao wanaendelea kusukuma siku na wasielewe ni wapi wanaelekea.

Pamoja na changamoto hii ya muda ambayo huenda unaipitia, kuna kitu kizuri sana kuhusu muda. Kitu hiko ni kwamba huwezi kukopa muda, yaani hata ukitumia muda wako wa leo vibaya kiasi gani, bado huwezi kukopa muda wa kesho ukautumia leo. Kesho ni siku nyingine mpya ambapo unaweza kuitumia vizuri kuliko ulivyotumia siku ya leo na ukabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.

Mwaka huu na miaka mingine iliyopita umekuwa ukijiwekea malengo mazuri sana kwenye maisha yako. Umekuwa unaweka mipango ambayo kwa hakika kama ungeweza kuikamilisha leo hii maisha yako yangekuwa bora sana. Lakini kwa sababu ambazo unaweza kuwa hujazijua bado kila mwaka unashangaa unaisha lakini malengo na mipango yako huwezi kuifikia.

Ulishaweka malengo kwamba unataka kuachana na kazi inayokusumbua na kuingia kwenye biashara ili uweze kusimamia maisha yako, ila siku zinayoyoma na huoni dalili za kufanya hilo.

Ulishaweka malengo ya kukuza biashara yako na kuitanua zaidi lakini kila siku inayokuja unajikuta na changamoto zaidi na hivyo kushindwa kutekeleza mipango yako.

Umeshaweka mipango mizuri sana na maisha yako, ila kila siku yanatokea mambo ambayo yanakufanya ushindwe kutekeleza mipango yako.

Ni jambo la kusikitisha sana pale ambapo unaona miaka inakatika na hakuna mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye maisha yako.

Habari njema kwako

Pamoja na changamoto zote ulizopitia kwenye maisha yako mpaka kufikia leo, hata kama umepoteza muda kiasi gani nina habari njema kwako. Habari njema ni kwamba muda uliotumia ni muda uliopita tu, muda wa kesho bado ni mpya kabisa na wala hujaugusa. Pamoja na kwamba muda wa kesho ni mpya, kama utautumia kama ulivyotumia muda wa jana na wa leo utarudi kule kule kwenye kupoteza muda na maisha yako hayawezi kuwa na tofauti kubwa.

Pamoja na kwamba mwaka huu 2014 umeisha na huoni mabadiliko makubwa uliyotarajia, mwaka 2015 bado ni mpya kabisa kwako na unaweza kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako. Mabadiliko hayo hayaji kwa bahati mbaya, bali yanatokana na mipango mizuri ambayo utajiwekea kwa mwaka huo 2015. Na pia mipango tu haitoshi, bali unahitaji mbinu bora za kuitekeleza mipango yako.

Kutokana na umuhimu huo wa kuweka malengo, mipango na mbinu za kufikia malengo hayo, AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina hii inajulikana kama SIKU 21 ZA MAFANIKIO MWAKA 2015. Kupitia semina hii utajifunza mambo mengi sana, baadhi ya mambo hayo ni jinsi ya kuweka malengo makubwa utakayoweza kuyafikia, jinsi ya kushika hatamu ya maisha yako, jinsi ya kuwa bora kwenye kile unachofanya, jinsi ya kutumia muda wako vizuri, jinsi ya kuongeza ubunifu wako na jinsi ya kuifanya kila siku kuwa ya maana kwako.

Mambo yote haya utakayojifunza ni muhimu sana ili kuweza kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.

Semina hii itaendeshwa kwa siku 21 ambapo kila siku utatumiwa email yenye somo husika lililoelezwa vizuri na kukupa hatua ya kuchukua. Utaweza kuuliza swali au kuomba ufafanuzi katika wakati huo wa semina. Pia kama zoezi la kuweka malengo ni gumu kwako tutasaidiana hatua kwa hatua jinsi ya kufanya zoezi hilo.

Semina hii itaanza jumatatu ya tarehe 05/01/2015 mpaka jumapili ya tarehe 25/01/2015. Kama utapenda kushiriki semina hii tuma email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Usikose nafasi hii muhimu ya kuuanza mwaka 2015 kwa mtazamo mpya na utakaoweza kukufikiasha kwneye mafanikio makubwa unayotamani kila siku.

Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ya siku 21, usipange kuyakosa, hutayapata tena wakati mwingine na wala hutaweza kuyapata sehemu nyingine.

Nakutakia kila la kheri katika siku chache zilizobaki ili kumaliza mwaka huu 2014,

Tupo pamoja.
 
Kuna gharama yeyote kwa kushiriki semina kwa njia ya mtandao ?
NI VEMA KUWEKA WAZI GHARAMA KABLA MTU HAJAWAPA EMAIL !
 
Kuna gharama yeyote kwa kushiriki semina kwa njia ya mtandao ?
NI VEMA KUWEKA WAZI GHARAMA KABLA MTU HAJAWAPA EMAIL !

Habari mkuu, tuma email na utapewa details zote za ushiriki. Mambo mengine hayajawekwa hapa kutokana na vigezo na masharti ya JF.
Karibu sana.
 
Back
Top Bottom