Siku 1900+ za JK Ikulu: Amefanikiwa nini? Ameshindwa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku 1900+ za JK Ikulu: Amefanikiwa nini? Ameshindwa nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Jan 16, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uongozi wa nchi si suala wala jukumu dogo. Ni jukumu la kila mwezi, kila wiki, kila siku, kila saa, kila dakika na kila sekunde kwa kipindi cha miaka mitano!! Utendaji wa kiongozi unapimwa hivyo hivyo. Kuna mafanikio ya muda mrefu na muda mfupi.

  Mafanikio ya JK kama Raisi yalitajwa sana wakati wa kampeni zake za uraisi. Aliyoshindwa yalitajwa sana na wagombea wengine wa upinzani. Wakati wa kampeni JK alitaja zaidi mafanikio yake wapinzani wakataja zaidi aliyoshindwa. Kampeni zimeisha, uchaguzi umemalizika. WanaJF hawaombwi kura, ni watu wenye uelewa na wanaishi katika jamii ya watanzania. WanaJF wana nafasi ya 'kumhukumu' kwa haki JK.

  Kwa kutambua uelewa, umakini na nafasi ya JF katika jamii namleta kwenu JK mumtolee hukumu ya haki. Kwa siku 1900+ tangu achaguliwe kuwa Raisi amefanikiwa nini? Ameshindwa nini?

  Hukumu ya wanaJF katika mfumo wa tathmini ya mafanikio au kushindwa kwake katika Elimu, Afya, MIUNDOMBINU, KILIMO, USALAMA WA RAIA, AJIRA, MICHEZO, RUSHWA N.K itasaidia kutoa mwanga tunatoka wapi na tunaelekea wapi kama nchi. Pia itasaidia kujua tunatakiwa tufanye nini kama wanaJF. Tushauri, tukosoe na tutoe suluhisho.

  CCM wasijitetee, CDM na vyama vingine wasikosoe pekee. Lengo liwe kutoa suluhisho la kudumu kwa matatizo ya nchi yetu au kutoa msukumo zaidi kwa yale yaliyofanikiwa.

  Hatuwezi kusubiri mpaka 2015 kujikwamua tulipokwama au kujipongeza kwa tulipofikia. Kila sekunde, kila saa, kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka ni lazima tuendelee au turudi nyuma! Umasikini au utajiri wetu unapotea au unaongezeka kwa kila sekunde sio kwa miaka 5. Miaka 5 ni majumuisho!!
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,797
  Trophy Points: 280
  kaandaa sherehe ya mabalozi ikulu
  [​IMG]
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah, Ivuga sina cha kusema zaidi ya kupongeza kwa kutoa ushahidi katika 'hukumu' yako. Nadhani wakati wa majumuisho tutajua kama ni mafanikio au kushindwa!

  Kwa kiasi kikubwa you have made my day. Nimerudia post yako mara mbili tatu! Nimecheka sana!
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Alifanikiwa kuwalipa richmond/dowans zaidi ya 150m kila siku kwa zaidi ya mwaka pasipo kazi yoyote iliyofanyika, na bado anashinikiza wapewe golden handshake ya 94bn.
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  JK alikuwa amejipanga dili ya DOWANS sema imekataa na sidhani kama itatik
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kafanikiwa kumfanya mwanye riz 1 kuwa rais msaidizi wa tz
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa udongo umeanza kuzeeka? Kwa nini isitiki? Umesahau kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala? Dowans ni historia. Hapa tunapiga story tu lakini kuhusu kulipa maamuzi yashafanywa kabla hata ya kesi yenyewe.

  Richmond ilisemwa ni kampuni feki, ililipwa fedha nyingi tu, ikahamishia 'mkataba' kwa Dowans nao tukawalipa na tunawalipa. Hakuna aliyechukuliwa hatua kwa ujinga huu. Kujiuzulu ni adhabu?

  Hakuna aliyehoji mpaka sasa! Story zinaendelea kupigwa. Hiyo dili imeshatiki watu wapanga nyingine kiongozi!
  lakini
   
 8. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,797
  Likes Received: 6,307
  Trophy Points: 280
  Sawa sawa.

  Wakati TANESCO wanataka kuvunja mkataba na DOWANS, Pinda aliwasifia sana REX attorneys kwamba wana uzoefu wa kimataifa na ''wametushauri'' kwamba ule mkataba uvunjwe.

  Sasa ni hao hao REX wanashauri TANESCO iilipe DOWANS kwa kuwa uamuzi wa ICC ni halali!!

  Kama ingekuwa ushauri wa mwanzo tulipewa na shekhe Yahya, labda sasa hivi angetwambia nyota zimetukalia vibaya. Sasa REX nao je? wali-base wapi hapo mwanzoni?? zile basics zimekuwaje? usanii? Pinda alidanganywa au na yeye ni part of it?
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa najiuliza mbona hawa viongozi wetu hawajiulizi? Au wanamajibu gani ambayo mimi na wewe hatuyajui?

  Tunawezaje kuibiwa na kutapeliwa mchana kweupe? Tumelogwa?
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Amefanikiwa sana tu kwani kupitia yeye kamleta maximo, alitaka ailete madrid hamuoni kama ni mafanikio?

  Hajui kwa nini watanzania ni maskini wakati utajiri tunao si mafanikio hayo?
  Alisema atawatoa watz hapa na kuwapeleka kule na amefanikiwa wkt alitukuta tuna uwezo kidogo kipindi cha mkapa lkn sasa tumekuwa masikini sana tu(dola ilikuwa chini, sukari bei rahisi, mafuta yote yamepanda) ni mafanikio hayo jamani
   
 11. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kusema kweli alichofanya kwamaendeleo ya waTanzania sijui labda kuwafurahisha maswahiba wake . nashidwa kuelewa hili la dowans halioni? inamanana walikubali kuvunja wakijua wataja pata hela zaidi baadae ?mbona enzi zile Mwalimu aliweza taifisha majengo na shule za dini leo inashindikana nini ? lazima mkwere anahusika na ndiomaana yupo kimya
   
Loading...