Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zimebainisha bado tatizo ni kubwa

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,197
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,197 2,000

Leo ni kilele cha siku 16 za kupinga vitendo vya mbalimbali vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto. Katika kipindi chote hicho matukio mbalimbali yametokea katika sehemu kadhaa nchini kuhusiana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto. Vile vile, mashirika na taasisi kadhaa zimetoa takwimu kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ni vigumu kupita siku nchini kwa sasa bila kusikia habari za kufanyiwa ukatili wa aina fulani watoto, hasa mabinti. Wapo wanaobakwa, kuingiliwa kinyume cha maumbile na watu wazima wengine wakiwa na umri sawa na babu zao; ilihali wengine wakifanyiwa vitendo vingine vya kikatili kama kupigwa na kuumizwa vibaya.

Matukio kwa mfano ya kuwajeruhi watoto wadogo, kuwaachisha masomo watoto wa kike kwa kuwapa mimba na ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike pia yaliripotiwa kwa kina na vyombo vya habari.

Takwimu zilizotolewa wakati wa maadhimisho hayo na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto zinaonyesha kuwa matukio ya ukeketeji wanawake na watoto yako juu kwa mfano, mkoa wa Manyara bado unaongoza kwa ukeketaji kwa asilimia 71 huku mkoa wa Tanga ambao una unafuu ni kwa asilimia 20.

Mikoa mingine ni Dodoma asilimia 64, Arusha 59, Singida 51, Mara 40 na Morogoro 21.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 kwa asilimia 44 wamefanyiwa ukatili na wenzi au waume zao huku asilimia 15 ya umri huo wanakeketwa.

Jambo linalotia matumaini ni kwamba serikali imeahidi kulishughulikia tatizo la ukeketaji kwa kusema inaendelea na jitihada mbalimbali ikiwamo kufanyia marekebisho sheria na kuweka sera, kuandaa mpango ili kusaidia kupunguza ukatili na kuunda kamati ya kitaifa ya kupinga ukatili wa aina zote.

Vitendo vya ukatili pia vimekuwa vikiongezeka dhidi ya watoto huku takwimu zikionyesha kuwa kwa kipindi cha miezi minane, wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, ilipokea watoto 257 waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na licha ya mashauri yote yaliyoripotiwa, ni kesi tatu tu ndizo zilizofikishwa mahakamani.

Uongozi wa wilaya hiyo unasema katika vitendo hivyo waliobakwa ni wanawake 20, watoto wa kike 100, waliolawitiwa wanaume ni 10 na watoto wa kiume 56. Watoto wa kike waliobakwa na kulawitiwa 11, waliopigwa watu wazima 33 na watoto 16, watoto waliochomwa moto watano pamoja na watoto sita waliotelekezwa.

Hatuwezi kueleza matukio yote yaliyotokea ndani ya siku 16 ya ukatili wa kijinsia, lakini inatosha kusema kuwa kuna tatizo kubwa ambalo linahitaji kushughulikiwa na jamii yetu kwa pamoja.

Jambo la kwanza linalopaswa kufanyika ni jamii kutambua haki za binadamu na kupitia elimu ambayo inapaswa kutolewa na serikali na wadau mbalimbali yakiwamo mashirika na wanaharakati.

Elimu hiyo itawawezesha wanajamii kufahamu haki zao za msingi hivyo kuvichukia. Hilo pia litawasukuma kuripoti matukio hayo kwa vyombo husika na kwa wakati mwafaka.

Baadhi ya mashirika kama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Mtandao wa Kijinsia Tanzania na (TGNP) mengine hadi sasa yamejitahidi kutoa elimu kuhusiana na ukatili wa kijinsia kupitia tafiti mbalimbali zikiwamo za kihabari na pia kutoa ushauri nasaha kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.

Tumefurahishwa na kauli ya Mwenyekiti wa tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento, akiwataka majaji na mahakimu nchini kutoa hukumu kwa mujibu wa matakwa ya sheria hasa katika kesi za jinai ili kuepuka malalamiko ya watu na ukiukwaji wa haki za binadamu zikiwamo zinazohusiana na ukatili wa kijinsia.

Ni matarajio yetu kuwa serikali itatekeleza ahadi zake za kuzifanyia marekebisho haraka sheria zilizoko pamoja na kutunga mpya kwa lengo ka kudhibiti vitendo hivyo.

Kwa kufanya hivyo, tunaamini kuwa zikitungwa sheria nzuri, vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya watu dhidi ya ukatili wa kijinsia na haki za binadamu kwa ujumla vitakoma kwa kuwa wahusika wataogopa mkono wa sheria.

Ni matumaini yetu kwamba leo wakati wa kuadhimisha siku ya haki za binadamu, mikakati kadhaa itatolewa kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu.
CHANZO: NIPASHE


 
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Messages
30,113
Points
2,000
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2010
30,113 2,000
Kwa mujibu wa takwimu hizo, wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 kwa asilimia 44 wamefanyiwa ukatili na wenzi au waume zao huku asilimia 15 ya umri huo wanakeketwa.

bado tuna changamoto ya takwimu nchini, nakumbukwa hii ilitolewa 2005 na WHO
 
Viva89

Viva89

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
1,256
Points
1,225
Viva89

Viva89

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2012
1,256 1,225
i find this issue to be very serious na watu wengine hawajui ukatili wa kijinsia nini...mazingira yetu ya kuishi kwa kiasi kikubwa bado ni yale yale kama zamani n hili suala sio kwa wanawake wa vijijini tu hata hapa mjini..tajiri kwa masikini...tuwafundishe kikazi hiki kuepusha matatizo haya kuendelea na mafunzo yanaanza nyumbani...tulifanyie kazi hili suala
 

Forum statistics

Threads 1,324,625
Members 508,740
Posts 32,168,330
Top