Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia: Ukatili kwenye Mitandao na madhara yake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kukua kwa Teknolojia ya kidigitali pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 umechangia mabadiliko ya mfumo wa kufanya kazi. Watu wengi wamekuwa wakitumia teknolojia ya TEHAMA na mitandao kama sehemu za kupata taarifa kukuza biashara zao, kufanya kazi na mawasiliano kwa ujumla. Hata hivyo, kwa upande mwingine ukuaji huu wa mitandao na matumizi ya TEHAMA yanaongeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kasi kubwa.

Je, ukatili wa kijinsia mitandaoni maana yake nini?
Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni ni aina ya udhalilishaji ambao unafanyika kwa njia ya mitandao. Ukatili huu ni pamoja na, ikiwemo lugha za matusi, kejeli, picha ama video za utupu.

Ukatili huu umekuwa ukiwaathiri wanawake, wasichana, viongozi wa nchi, wasanii pamoja na wanawake watetezi wa haki za wanawake na watu maarufu kwa jumla.

Kutokana na udhalilishaji huo umepelekea wanawake watetezi kunyamazishwa na kupunguza kasi zao za kutumia majukwaa ya mitandaoni kwa kuhofia kutwezwa utu wao na kupewa majina mabaya ya udhalilishaji. Mara kadhaa udhalilishaji huu umekuwa ukifanywa na wanaume ambao takwimu yao inaonesha kuwa watumiaji wakubwa wa mitandao kuliko wanawake

Madhara ya Ukatili Mitandaoni
Kama ilivyo kwenye aina nyinigine za ukatili, ukatili wa mitandaoni una madhara
yafuatayo;

1. Madhara kisaikolojia, unaweza kupeleke watendewa kupata msongo wa mawazo, kusababbish kujiua au kupoteza mwelekeo katika maisha

2. Kupelekea wanawake hasa wanawake watetezi kupoteza dira za harakati zao za utetezi wa haki za binadamu hususani haki za wanawake na watoto pamoja na makundi ya pembezoni

3. Inajenga hofu na kuvunja moyo kwa wanawake kushiriki kwenye ngazi za uongozi na maamuzi wakihofia kudhalilishwa na kutwezwa utu wao

Je, Sheria inasemaje?
Sharia zinazolinda na kuzuia ukatili wa kijinsia mitandaoni ni pamoja na;

1. Sharia ya Maudhui ya Mitandaoni (Online Content Regulation) 2020 ambayo inakataza na kutoa adhabu kurusha maudhui ya udhalilishaji ikiwamo picha/video za utupu, lugha za udhalilishaji zinazokwenda kinyume na utamaduni wa Mtanzania.

2. Sharia ya Kimakosa ya Mitandao 2015 (Cyber Crime Act) ambapo Kifungu cha 23 kinakataza na kupinga uonevu mtandaoni kuwa ni kosa kisharia kwa mtu yoyote kufanya uonevu wa aina yoyote kwa kutumia njia za kieleketroniki na kufanya hivyo ni kosa kisharia, a yeyote atakayekutwa na kosa hili atatumikia kifungo, kisichozidi miaka 3 jela au zaidi, au kulipa faini isyopungua milioni tano (5) au vyote kwa pamoja

Je, kwanini ukatili wa mitandaoni unazidi kukithiri pamoja na sharia kuwepo
Sababu zinazopelekea ukatili wa mitandaoni kuendelea kukithiri ni kama zifuatazo;

1. Uelewa mdogo kwa wananchi juu ya sharia zinazozuia na kukataza ukatili wa kijinsia mitandaoni

2. Hofu ya kuendelea kudhalilika hasa pale kesi zinapotaka kwenda mahakamani

3. Tamaduni ya jamii nyingi kwenye mitandao kukaa kimya badala ya kukemea wanapoona vitendo vya uaktili kwenye mitandao

4. Mapungufu katika utaratibu wa ripoti kwa vyombo husika

Hivyo basi, katika kipindi hiki cha Siku 16 za Vanaharakati, tunatumia kampeni hii kupaza sauti na kukemea ukatili wa kijinsia mitandaoni.

WiLDAF TANZANIA
 
Hivi mafanikio ya hizi siku yamefanikiwa kweli? au ndio hivyo matamasha ya mchongo tu kila siku watu wapige hela wapite hivi?

Maana kiuhalisia wiki chache zilizopita matukio ya ukatili bado yanaongezeka
 
Miss Natafuta , kitendo chako cha kwenda migombani wewe na watoto na kuniacha nyumbani, mimi na House girl tu, ni ukatili wa hali ya juu wa kijinsia.
Hebu fikiria mvua kubwa inanyesha, saa mbili na nusu usiku, dada katoka kukinga vyombo nje, anarudi na kanga moja imelowa na kuushika mwili wake barabaraa.

Mungu anakuona haya unayonifanyia
 
Pole Sana yaani amekufanyia ukatili wa kijinsia.
 
Vita dhidi ya ukatili huo ianze na wanawake wenyewe.
-waache kucheza muziki uchi kwenye vigodoro
-Kucheza nusu utupu kwenye video za muziki (utakuta mwanaume kavaa suti mwanamke kavaa chupi)
.Tubaki na hizi video za kuingilia privacy.
.Wakijiheshimu tutapunguza majanga haya,tuko pamoja
 
Back
Top Bottom