Siku 120 gerezani Uyui: Magereza zimejaa mahabusu na wafungwa kupitia sheria mbovu

naomba kuuliza Dola la kiisilaumu na dola la jamuhuri lipi linatisha? Nyie watu mnapenda kujifanya mnajua mbovu sijui na majambia na karatw zenu. Hizi tabia za nchi za kiarabu zitawatokea puani. Nashauri wale wanaotaka kufanya Tz kuwa dola la kiislam tutawamiza na kufanya unyama zaidi hii hapa ulioandika na pengine haitaka kutokea. Nyie watu imani yenu ni problem kila pahala ati.
hujui chochote kuhusu uislam, wasiokuwa waislam hupenda kuwakandamiza waislam, mwengine yanawarud kwa watu wenu kuanza kupotea
 
Wewe ni muislamu. Hubiri uislamu. Huyu YESU tuachie sisi.
Wewe ni muislamu. Nguruwe na kafiri vinakuhusu nini ? Kwani kutaja nguruwe ndio kunakupeleka Mbinguni.
Jaribu tena na watazimia bangi kwenye hiyo 0 yako.
Ulishasikia wakristo kwenye mikutano yao wakimtaja Mohamed SAW ?
 
alikuwa anawakagua o zenu kama hivi
 

Attachments

  • 23517804_199937250551530_3116425708905157629_n.jpg
    23517804_199937250551530_3116425708905157629_n.jpg
    18.4 KB · Views: 38
cd724f779eb7adf1b82cfa53bb6ee898.jpg

UYUI ni miongoni mwa Magereza makubwa yaliopo nchini Tanzania, lipo katika mkoa wa Tabora. Gereza hili huchukuliwa kama gereza la kanda ya Magharibi yani hujumuisha magereza ya Kigoma, Shinyanga, na Tabora yenyewe.

UYUI ni katika magereza yenye ngome kubwa zaidi ukiondoa gereza la Segerea na Butimba mkoani Mwanza, hili ni miongoni mwa magereza ambayo yana msongamano mkubwa wa mahabusu na wafungwa na ni miongoni mwa magereza yenye kila aina ya vyumba vya mateso kwa watuhumiwa na wafungwa, ni gereza ambalo lina sero maalum kwa ajili ya kunyongea watu waliohukumiwa kifo. Pia kuna sero saba ambazo ni maalumu kwa ajili watu wenye kutuhumiwa makosa ya uhaini.

Hizi sero inasemekana zilijengwa miaka 70 baada ya Nyerere kujaribiwa kupinduliwa na wale aliowaita wahaini kwa kipindi kile hasa baada ya Sera zake ujamaa kushindwa na kuporomoka kwa shilingi dhidi ya $ kwa sababu nchi haikuwa na Sera ya vyama vingi kwa wakati ule yeyote aliepingana na Nyerere alichukuliwa kuwa ni mhaini na kushughulikiwa na vyombo vya Dola kwa kulinda mamlaka ya Ikulu.

Kipindi hicho zikatungwa nyimbo za kuwakejeli kina Kambona, Mapalala, na wengineo wengi kutokana na mitazamo yao ya kumpinga Nyerere hasa kwa namna alivyo kuwa akiipeleka nchi kwa misingi ya ukanda na udini ambao haukujificha katika teuzi zake pindi alipokuwa akiugawanya mkate wa Taifa.

Ilikuwa ni tarehe 19/09/1999 katika maeneo ya viwanja vya parking pale wilaya ya Nzega mida ya saa nne asubuhi ndipo nilipo kutana na gari aina ya 110 ikiwa imesheheni askari wa FFU huku bunduki zao zikiwa tayari kumlenga Shabaha yeyote ambae angekataa amri yao amri ambayo wao waliita kuwa ni halali japo ilijaa uvunjifu wa haki za binadamu.

Nilitii amri yao ilionitaka kunyoosha mikono juu huku nikiambiwa kuchuchumaa chini kabla ya kuzolewa na kutupwa katika defender lile huku nikikanyagwa mgongoni na sehemu za kichwa mithiLi ya myama.

Awali sikujua kosa langu japo baada ya kufikishwa kituo cha police pale Nzega mjini nilikuta kundi kubwa la wahubiri wa dini ya kiislam wakiwa chini ya ulinzi mkali wa police huku askari waliovalia mabomu ya machozi na bastola zao mikononi wakiwa wamezunguka eneo zima la kituo.

Nilitamani kuhoji kisa cha kukamatwa kwangu nikiwa barabarani lakini kabla ya kusikilizwa niliambulia shambulizi la hatari juu ya paji langu la uso virungu mfululizo vikiniandama mwilini kwangu huku matusi makubwa yakiwatoka wale maafande ambao walijipa Kazi ya kuniadhibu kabla ya mahakama kunihukumu.

Japo siku hiyo sikujua kosa la kuunganishwa na wale wahubiri wa dini ya kiislam lakini kesho yake asubuhi Mimi pamoja na wale mashekh tulikuwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Nzega.
Tuhuma dhidi yetu ilikuwa
1- Kufanya mkutano usio halali.
2- Kutoa Maneno ya kashifa dhidi ya Yesu kristo Mwana wa mungu.
3- Kuwaita wale wanao kula nyama ya nguruwe Makafiri.

Makosa haya yote mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa tulikuwa tumetenda makosa dhidi ya Jamhuri hivyo mlalamikaji alikuwa ni Jamhuri dhidi yetu tulikuwa watu 15.

PP aliiambia mahakama isitupe dhamana kwa kuwa Maneno tuliyokuwa tumeyatamka yalikuwa yameumiza hisia za watu wengi hivyo kama mahakama ingetupatia dhamana huenda tungedhurika.

Mahakama ikakubaliana na maelezo ya PP baada ya mahakama kukubali ombi la PP bwana PP aliiambia mahakama kuwa tulitakiwa kupelekwa Tabora kwa sababu ya usalama wetu Nzega palikuwa hapafai.

Kweli Jalada la kesi yetu lilihamia Tabora na sisi chini ya ulinzi mkali tulihamishiwa Tabora

Mapokezi Uyui
Ni saa Tisa mchana ving'ora vya FFU huku vikiongozwa na Leyland kubwa ya jeshi la police lilotengenezwa maalum kwa ajili ya kubeba wahalifu lilikuwa limepaki mbele ya Lango kubwa la kuingilia gerezani huku mitutu ya askari police na askari magereza ikiwekwa tayari kwa yeyote ambae wenge la utoro lingejaribu kumpanda.

Tulipokelewa kwa mateke na virungu kutoka kwa askari magereza wale heshima na utu havikuonekana tena machoni kwa wale askari.

Baada ya kuingia geti la pili pale gerezani amri ya kututaka kuvua nguo ndio ilikuwa amri ya kwanza kutoka kwa wale askari wa gereza.

Tulivua nguo zetu zote zilizokuwa zimeyaficha maungo yetu, Taswira ya umbile la uchanga tayari ilikuwa wazi mbele ya halaiki, heshima zetu mbele ya askari wa kike haikuwepo tena bali miili yetu ilipewa jina la uhalifu kila mtakatifu alienjoy kuhesabu michanjo iliojipanga juu ya ngozi zetu.

Tupu zetu kila mmoja alizihukumu kwa uwezo wa maono yake, naamini ndani ya macho takriban arobani ya askari wale kila jicho lilifurahia aina ya tupu zetu Mungu alivyo ziumba na kuzijaria kwa namna tofauti kulingana na uwezo wake Jarali.

Nilijawa na hofu pindi askari alipotuamuru kuinama huku tumeshika magoti na yeye akikagua O zetu utadhani dume la nyati.

Sikuweza kutambua sababu ya yeye kutukagua maeneo hayo huku wengine akiwawekea katika O zao kilungu chake cha mpingo.

Hakika ulikuwa ni udhalili wa hali ya juu dhidi yetu.

Baada ya ukaguzi ule tulitakiwa kuruka kichura chura hali tukiwa uchi, zoezi lilodumu kwa muda wa saa moja.

Office ya RCO
Hii office ilikuwa maeneo ya Boma karibu kabisa na ofisi za Mkuu wa mkoa ndani ya ofisi hii palikuwa na vyumba maalum kwa ajili ya mateso.

Niliingizwa katika chumba ambacho ndani yake palikuwa meza pamoja na kiti kimoja baada ya kuingia ndani ya chumba hiki mwili wangu ulianza kusisimka japo kilikuwa ni chumba kipana kidogo lakini ni dhahiri kilionekana ni chumba cha mauaji kwa mtuhumiwa ambae angeleta ukorofi kwa Afande husika.

Baada yakuingizwa ndani ya chumba kile niliamrishwa kuvua nguo zangu zote huku mikono yangu ikifungwa pingu maalumu, walikuja askari watatu ambao miili yao ilijengeka kwa mazoezi uso, ukionekana katili kuliko viumbe wa dunia hii, mmoja katika wale alitia Kofi la uso ghafla nyota zilianza kusherehekea ujio wangu ndani ya chumba kile.

Baada ya shambulio hilo niliamriwa kulala juu ya meza ndogo ilioletwa pale na ghafla aliingia Afande wa kike mkononi mwake alibeba packet ya sigara aina ya sport
Miguu yangu ikiwa imeninginia juu ya ile meza uume wangu ukijitenga na kordani, wale askari wa kiume walisimama sawia kumuangalia yule askari wa kike.

Ghafla yule askari wa kike alisogea pale nilipokuwa huku mdomoni mwake akivuta sigara, baada ya takribani dakika tatu kupita Yule askari wa kike alikuwa akizishika sehemu zangu za siri tena mikono yake ilikuwa laini mithiri ya ngozi ya swira.

Japo nilikuwa chini ya uangalizi wa mateso Mkia wangu haukujali kujitutumua mbele ya Afande yule jasiri kwa kitendo chake kile cha kushika Pentagon.

Kumbe lilikuwa kosa kubwa sana kwangu sababu baada ya kuonekana nilivyo jasiri pamoja na mateso yote niliokuwa nakumbana nayo eti bado nilikuwa na hisia juu ya ngono.

Maskini Mimi nilijuta hasa baada ya yule mwanamke kukigeuza kiume changu kuwa sehemu sahihi ya kuzimia sigara yake.

Hakika nilihisi maumivu makali ambayo mfano wake sijui labda katika ule ukurasa wa moto wa Jehanam.

Mateso mfululizo yaliendelea huku nikitakiwa kuwataja washirika wangu katika mtandao wa ugaidi, sikujua chochote kuhusu ugaidi na magaidi niliotakiwa kuwatambua siku hiyo.

Baada ya mwezi mmoja
RCO Nghoboko akiongozana na bwana SS walikuja magereza ya Uyui, Mimi na watuhumiwa wenzangu tulipelekwa katika chumba maalum ambako tuliweza kufanya maongezi kuhusu tuhuma zilizokuwa zikitukabili ndani ya maongezi hayo japo mimi niliongea kwa Jazba tofauti na wenzangu lakini RCO hakuonekana kukerwa na matamshi yangu japo miongoni mwa kauli zake alituomba kuwa na subira kwa sababu tuhuma dhidi yetu ilikuwa ni amri toka juu.

Hii juu haikujulikana kwetu wala kwa RCO Bali ilionekana wazi tuhuma zetu zilibebwa na ushahidi wa mashinikizo kutoka huko juu.

Japo mapambano ya dhamana ilikuwa ni sehemu Muhimu katika mustakbari wa kesi yetu lakini ilikuwa ni vigumu mahakama kutupatia dhamana siku ziliyoyoma na miezi ikaanza kuzeeka huku maisha ya gerezani tukianza kuyazoea kila siku ndani ya lile gereza ilikuwa na visa vyake huku matukio ya vifo kutokana na mlipuko wa magonjwa ya ngozi ukipukutisha idadi kubwa ya mahabusu na wafungwa.

Watu wengi walikuwa na ugonjwa wa utapyamulo kutokana na lishe duni iliokuwa ikipatikana pale gerezani Uyui, Unga wa dona ulichanganywa na pumba huku Mboga Muhimu ikiwa ni dagaa watatu katika kila bakuli la mfungwa na mahabusu Mkuu wa gereza wakati huo alipiga marufuku vyakula na Huduma kutoka nje ya magereza jambo lilopelekea watu kukosa mafuta na karanga vitu ambavyo huwa ni Muhimu kwa mtu alieko magereza.

Ushahidi mahakamani
Baada ya mwendesha mashitaka kuiambia mahakama kuwa alikuwa na vielelezo vya kesi husika mahakama ilimtaka kuvitaja ili viingie katika kumbukumbu za kimahakama PP alisema kuwa walifanikiwa kukamata mawe, Fimbo, na majambia. Silaha ambazo zilikuwa tishio kubwa dhidi ya binadamu na akaahidi kuwa vifaa hivyo vingeletwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi.

Pamoja na maelezo hayo PP ambae alikuwa ni bwana SS hakuweza kuiambia mahakama kuwa kuna aliedhurika na matendo yetu japo mimi awali sikuwa mfasi wa kundi lile kabla yakuunganishwa na watu wale.

Kesi yetu ya fika mahakama kuu kupinga mahakama ya mkoa kutunyima dhamana.

Wakili wa upande wetu alikuwa ni mzee Mussa Kwikima aliomba mahakama iweze kutoa amri ya dhamana dhidi yetu sababu tuhuma dhidi yetu zilikuwa ni za uongo sababu mlalamikaji ambae aliitwa Jamhuri hakuwahi kubainisha ubini wake mahakamani na wala hakuwahi kufika mahakamani na kuiambia kuwa sisi tulikuwa tumemkosea.

Hoja zilizoifanya mahakama kuu kumuuliza PP ubini wa Jamhuri sababu kulingana na taratibu za makosa ya jinai lazima kuwepo mlalamikaji alie dhulika na jinai husika na Jamhuri awe msimizi wa pande zote mbili (Respondent v/s Defendant) si Jamhuri kuwa mlalamikaji dhidi ya mtuhumiwa wakati Jamhuri hana ubini na wala baba yake hakuna amjuae.

Mahakama kuu ilikubaliana na hoja za advocate Kwikima na kutoa order ya dhamana kwa mahakama husika kweli baada ya miezi miwili tulipata dhamana binafsi siwezi kumsahau mzee Bilali Waikera mungu amrehemu huyu ndie alienidhamini katika kesi ile pamoja na waislam wengine wa viunga vya mji wa Tabora.

Hakika baada ya dhamana kesi yetu ilidumu kwa kipindi cha miaka minne na mahakama iliifuta kwa kukosekana mashahidi na kuzingatia hoja za msingi za advocate Kwikima.

Ndugu zangu nimeandika uzi huu kwa kuamini kabisa kabisa kuwa kuna idadi kubwa katika Jamii, Jamhuri amekuwa akiwabambikia kesi na hata wengine Jamhuri akiwaua kwa kuwatuhumu tu kuwa ni wahalifu huku RAIA wengine ndani ya nchi hii wakimtumia Jamhuri kuwaweka mahabusi yeyote wamtakae huku kauli za kesi haina dhamana zikitamalaki masikioni kwa watuhumiwa.

Hii ndio Tanzania ambayo babu zetu waliipigania kuondoa sheria za kikoloni lakini masikini walimuondoa mkoloni mwenye ngozi ya nguruwe mweupe wakamkabidhi mkoloni mwenye ngozi ya Nguruwe mweusi.

Akarithi Sheria na mamlaka zilezile ili kukilinda kizazi cha nguruwe katika uhai wa mwanadamu.

Pamoja na Uhuru wa rangi ya Bendera sheria zetu zimekuwa ni sheria Kandamizi mfumo wetu wa sheria ni mfumo wa kuwalinda wenye mamlaka kiongozi ndani ya nchi hii ni sehemu ya ufalme wa Mungu.

Haguswi kwa maamuzi yake kupitia sheria za nchi yetu yeye ni alpha nae ndie Omega juu ya mustakabali wa kila mtanzania, yeye ndio baba mwenye nyumba raia maskini kwake ni mithili ya panya katika nyumba yake, kelele zao hukumu yake ni maangamio hataki fyokofyoko kutoka familia ya panya kwa sababu kizazi chake ni kizazi cha nguruwe.. (The black Pig).

TBP ndio familia ilio wahifadhi mashekh wa Uamsho, TBP imewahifadhi katika sero viongozi wa vyama ambao wamejaribu kuisema vibaya hii familia ya TBP.

Magereza zimejaa mahabusu na wafungwa kupitia sheria mbovu zilizotungwa na hawa TBP, naamini umefika wakati wa kubadilika kutoka katika familia ya TBP ili tuweze kuwa huru kwa kuwa na sheria zinazoendana na misingi ya maana halisi ya Uhuru.

By. Nyamwera
pole xana mkuu kila mtu anakuwa na mapitio yake ya maisha
 
Back
Top Bottom